Kila mwaka baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha nne, hatua inayofuata kwa wanafunzi waliofaulu ni kupangiwa shule za sekondari za kidato cha tano au vyuo vya ufundi. Hii ni sehemu muhimu ya mpito kutoka elimu ya sekondari ya chini kwenda sekondari ya juu. Mwaka huu wa 2025, wazazi na wanafunzi wanasubiri kwa hamu majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano, maarufu kama Form Five Selections 2025.
Majina ya Selection za Form Five 2025 Yanatoka Lini?
Kwa kawaida, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MoEST) hutangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano miezi miwili hadi mitatu baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha nne.
Matarajio ya kutolewa kwa selection za Form Five 2025 ni kati ya mwezi Mei na Juni 2025.
Kwa hivyo, ni muhimu wanafunzi na wazazi kufuatilia tovuti rasmi ya NECTA (www.necta.go.tz) au TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz) kwa taarifa rasmi.
Vigezo Vilivyotumika Kupangiwa Shule
Wanafunzi hupangiwa shule za kidato cha tano au vyuo vya ufundi kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
Alama za ufaulu (divisions na point za masomo)
Tahasusi (combination) aliyochagua wakati wa fomu ya uchaguzi
Uwepo wa nafasi katika shule au chuo alichoomba
Usawa wa kijiografia – ili wanafunzi wasipangiwe shule mbali sana na walipo
Ushindani wa shule husika – shule bora huwa na ushindani mkubwa zaidi
Jinsia – baadhi ya shule ni maalum kwa jinsia moja
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Form Five 2025
Wanafunzi wanaweza kuangalia majina yao kupitia hatua hizi rahisi:
Njia #1: Kupitia Tovuti ya TAMISEMI
Tembelea tovuti: www.tamisemi.go.tz .kiungo https://selform.tamisemi.go.tz/content/selection-and-allocation/
Bonyeza sehemu iliyoandikwa “Form Five Selection 2025”
Chagua mkoa → halmashauri → shule ya sekondari ya mwanafunzi
Tafuta jina la mwanafunzi kwenye orodha
Njia #2: Kupitia Link za Moja kwa Moja
Wakati mwingine TAMISEMI huweka link ya haraka (direct link) ambayo inakupeleka moja kwa moja kuangalia shule uliyochaguliwa.
Kupitia Linki za Mikoa hii itakuwezesha kuona matokeo ya uchaguzi moja kwa moja na kwa urahisi zaidi.
Fomu za Maelezo ya Shule (Form five Joining Instructions)
Baada ya mwanafunzi kupangiwa shule, anapaswa kupakua fomu ya maelezo ya kujiunga (Joining Instructions) ya shule hiyo.
Maelezo ya Joining Instruction ni pamoja na:
Tarehe ya kuripoti shuleni
Vifaa vinavyotakiwa (mavazi, vitabu, mashuka, nk.)
Ada au michango ya shule
Kanuni na taratibu za shule
Mahitaji ya kiafya (chanjo, taarifa ya daktari, nk.)
Kupakua Fomu:
Tembelea tovuti ya TAMISEMI au shule husika
Pakua PDF ya fomu ya shule uliyochaguliwa
Chapa (print) na iwasilishwe pamoja na mwanafunzi siku ya kuripoti
Soma Hii : Tamisemi Selform MIS Jinsi ya Kubadilisha Combination za Form five
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ) Kuhusu Form Five Selections
1. Nifanyeje kama sijachaguliwa Form Five?
Unaweza kuomba nafasi kwenye vyuo vya ufundi au kozi za VETA.
TAMISEMI pia hutoa awamu ya pili ya uchaguzi (Second Selection).
2. Naweza kubadilisha shule niliyochaguliwa?
Kwa kawaida hapana, lakini kuna utaratibu maalum wa Transfer kwa sababu maalum kama afya au umbali.
3. Je, naweza kuona majina ya wengine?
Ndiyo. Majina yote huwekwa wazi kulingana na shule au halmashauri.
4. Joining Instructions lazima nichukue wapi?
Kupitia tovuti ya TAMISEMI au tovuti ya shule husika.
5. Nikikosa kuripoti kwa wakati, nitatolewa?
Ndio, unaweza kupoteza nafasi yako. Ni muhimu kuripoti ndani ya muda uliopangwa.