Baada ya kumaliza kidato cha nne, wanafunzi wengi hupangiwa tahasusi (combination) za masomo kwa kidato cha tano kulingana na matokeo yao ya mtihani wa taifa (NECTA). Hata hivyo, kuna wakati wanafunzi wanatamani kubadilisha tahasusi au kozi zao kwa sababu mbalimbali kama vile:
Sababu zinazoeza Kumpelekea Mwanafunzi kubadilisha Tahasusi
Kutopenda tahasusi waliyopewa
Kutaka kuhamia shule nyingine
Kuendana na malengo yao ya baadaye katika taaluma au kazi
Kuwa na changamoto katika masomo fulani
Ikiwa unataka kubadili tahasusi yako au kozi za kidato cha tano, makala hii itakuelezea hatua za kufuata na mambo muhimu ya kuzingatia.
Masharti ya Kubadili Tahasusi na Kozi
Kabla ya kuomba kubadilisha tahasusi, ni muhimu kuzingatia masharti yafuatayo:
Lazima uwe na sifa za tahasusi unayotaka kuhamia – Matokeo yako lazima yaendane na vigezo vya kujiunga na tahasusi mpya.
Kubadilisha tahasusi kunategemea nafasi katika shule husika – Shule zote zina idadi maalum ya wanafunzi wanaoweza kupokea kwa kila tahasusi.
Kuruhusiwa na Wizara ya Elimu au Mamlaka za Shule – Mabadiliko haya lazima yaidhinishwe na mamlaka husika.
Kubadilisha ndani ya muda ulioruhusiwa – Mara nyingi, mabadiliko yanaruhusiwa ndani ya wiki chache baada ya kuripoti shule.
Hatua za Kufanya Ombi la Kubadili Tahasusi
1:NAMNA YA KUINGIA KWENYE MFUMO WA SELFORM
- Ukiwa kwenye internet, fungua kivinjari chako (browser mfano, chrome), andika anuani ifuatayo selform.tamisemi.go.tz kupata dirisha la kujaza taarifa zako za kujisajili kama inavyoonekana hapo chini.
- Bofya Menu ya chini kabisa iliyoandikwa For Candidates, Click here to Register kama mtumiaji ni mara yake ya kwanza.
Kisha, ujaze taarifa zinazohusika za Index Number kwa format ya Mfano
S0101.0020.2018, Jibu swali utakaloulizwa, Jina la Ukoo na Mwaka wa kuzaliwa kama inavyoonekana hapo chini.
Kisha dirisha litafunguka na kutaka ujaze Password utakayoitumia siku zote. Dirisha lifuatalo litafunguka;
Ukishaandika Password, mfumo utaonekana katika sura hii kuonesha umefanikiwa kubadili Password;
Ukishabadili Password, utaitumia kuingia kwa mara nyingine kwa kuandika username mfano S0101.0002.2018 na Password uliyoibadili.
2.PART A: TAARIFA BINAFSI ZA MWANAFUNZI
Ukishaingia kwenye mfumo, dirisha lifuatalo litafunguka na sehemu zilizozungushiwa tu ndio utaweza kubadili taarifa binafsi. Ukimaliza kujaza bofya Save and Next hapo chini ili kuendelea mbele.
3.PART B1: STUDENT GENERAL CHOICES
Bofya katika sehemu hii ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo.
4.PART B2: ALTERNATIVE OPTIONS
Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya vyuo vya Kisekta. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT.
5.PART C1: FORM V STUDENT DETAILED CHOICES
Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya shule za form V na tahsusi zake: KUMBUKA– Mwanafunzi ataona Possible combinations tu na shule kutokana na ufaulu wa matokeo yake kwa lengo la kubadilisha. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.
6.PART C2: TECHNICAL EDUCATION
Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya Vyuo vya Technical na Tahsusi zake: KUMBUKA– Mwanafunzi lazima awe na ufaulu wa Tahsusi
ya PCM katika matokeo yake kwa ajili ya kubadilisha eneo hili. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.
7.PART C3: HEALTH EDUCATION
Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya Vyuo vya Afya na Tahsusi zake. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.
8.PART C4: DIPLOMA EDUCATION
Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya Vyuo vya Elimu na Tahsusi zake. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.
9.PART C5: OTHER COLLEGES
Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya Vyuo Vinginevyo na Tahsusi zake. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.
Je, Unaweza Kubadili Shule Pia?
Ndiyo! Ikiwa shule uliyopewa haifundishi tahasusi unayotaka, unaweza kuhamia shule nyingine. Hii inahusisha:
Kuomba ruhusa ya kuhama kutoka shule yako ya sasa
Kutafuta shule nyingine yenye nafasi kwa tahasusi unayotaka
Kuwasilisha barua ya uhamisho kwa TAMISEMI au Wizara ya Elimu kwa idhini rasmi
Tahasusi Zinazopatikana Kidato cha Tano Tanzania
Tahasusi mbalimbali zinapatikana kwa kidato cha tano, ikiwemo:
📘 Sayansi (Science Combinations)
PCB (Physics, Chemistry, Biology)
PCM (Physics, Chemistry, Mathematics)
CBG (Chemistry, Biology, Geography)
EGM (Economics, Geography, Mathematics)
PGM (Physics, Geography, Mathematics)
📕 Sanaa (Arts Combinations)
HGL (History, Geography, Language)
HGK (History, Geography, Kiswahili)
HGE (History, Geography, Economics)
HKL (History, Kiswahili, Language)
📗 Biashara (Business Combinations)
ECA (Economics, Commerce, Accounting)
HGE (History, Geography, Economics)
CBA (Commerce, Bookkeeping, Accounting)
Tahadhari na Changamoto za Kubadili Tahasusi
Muda wa kuomba ni mfupi – Ni muhimu mwanafunzi afanye maamuzi haraka kwani muda wa kuruhusu mabadiliko huwa mwanzoni mwa muhula wa kwanza.
Shule nyingi hazina nafasi za kutosha – Baadhi ya shule zina nafasi chache katika tahasusi fulani, hivyo ombi la kubadilisha linaweza kutolewa lakini lisifanikiwe kwa sababu ya ukosefu wa nafasi.
Baadhi ya shule zinakataa ombi la kubadilisha tahasusi – Ikiwa shule ina msimamo mkali kuhusu kubadilisha tahasusi, mwanafunzi anaweza kulazimika kuendelea na tahasusi aliyopangiwa.
Mwanafunzi anaweza kuchelewa kufidia masomo mapya – Kubadilisha tahasusi kunamaanisha kwamba mwanafunzi atahitaji kufanya juhudi zaidi kufidia masomo aliyokosa tangu mwanzo wa muhula.
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQs)
Naweza kubadili tahasusi baada ya muda gani?
Unapaswa kuomba ndani ya wiki chache za kwanza baada ya kuripoti shuleni. Baada ya muda huo, inaweza kuwa vigumu kuruhusiwa kubadilisha.
Je, kila mtu anaweza kubadili tahasusi?
Hapana. Ni lazima upate idhini ya shule na uhakikishe unakidhi vigezo vya tahasusi unayotaka.
Je, naweza kubadilisha tahasusi kutoka masomo ya sayansi kwenda biashara au sanaa?
Ndiyo, lakini lazima uwe na sifa zinazohitajika kwa tahasusi unayotaka kujiunga nayo.
Kubadili tahasusi kunaathiri matokeo yangu ya mwisho?
Inaweza kuathiri ikiwa utachelewa kuanza masomo mapya. Ni muhimu kuhakikisha unajifunza haraka na kufanya juhudi za ziada.
1 Comment
Nafasi ni chache sanaa