Baada ya kutangazwa kwa matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne 2024, hatua inayofuata kwa wanafunzi waliofaulu ni kupangiwa shule za Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi (Form Five and Technical Colleges Selection). Mkoa wa Kilimanjaro ukiwa moja ya mikoa ya Tanzania yenye shule bora, umepokea wanafunzi wengi waliopangiwa kuendelea na elimu ya sekondari ya juu (Advance Level).
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano Mkoani Kilimanjaro
Majina ya wanafunzi waliopangiwa kujiunga na Kidato cha Tano hutolewa kupitia tovuti ya TAMISEMI.
Hatua kwa Hatua:
Tembelea tovuti:
https://selform.tamisemi.go.tzBonyeza sehemu ya “Selection Kidato cha Tano 2025”
Chagua Mkoa – Kilimanjaro
Chagua Halmashauri unayohitaji (kwa mfano: Moshi Municipal, Hai, Mwanga, nk.)
Tafuta jina lako kwa kutumia:
Jina kamili
Au namba ya mtihani wa Kidato cha Nne
Kwa njia hii utaweza kuona shule uliyopangiwa pamoja na tahasusi (combination) uliyochaguliwa.
Halmashauri za Mkoa wa Kilimanjaro
Mkoa wa Kilimanjaro una halmashauri saba (7) ambazo zinasimamia shule za sekondari ikiwemo zile za Kidato cha Tano.
Orodha ya Halmashauri:
Moshi Municipal Council
Moshi District Council
Hai District Council
Rombo District Council
Mwanga District Council
Same District Council
Siha District Council
Kila halmashauri ina shule zake zinazopokea wanafunzi wa Advance Level kulingana na nafasi na tahasusi zao.
Shule za Advance za Mkoa wa Kilimanjaro
Kilimanjaro ni miongoni mwa mikoa inayojivunia kuwa na shule za sekondari za Advance zenye viwango vya juu vya ufaulu.
Baadhi ya Shule za Kidato cha Tano Kilimanjaro:
Old Moshi Secondary School – Moshi DC
Weruweru Girls Secondary School – Hai DC
Umbwe Secondary School – Moshi DC
Same Secondary School – Same DC
Kibosho Girls Secondary School – Moshi DC
Ashira Girls Secondary School – Moshi MC
Mkuu Secondary School – Rombo DC
Mwanga Secondary School – Mwanga DC
Shule hizi zinatoa tahasusi mbalimbali kama PCM, PCB, EGM, HGL, HKL n.k., na zimekuwa zikifanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa.
Jinsi ya Kupata Form Five Joining Instruction Shule za Mkoani Kilimanjaro
Joining Instruction ni fomu muhimu inayomwelekeza mwanafunzi:
Tarehe ya kuripoti
Mahitaji ya shule (sare, madaftari, vifaa vya tahasusi)
Ada na michango
Kanuni na taratibu za shule
Mawasiliano ya shule
Hatua za Kupata Joining Instructions:
Tembelea tovuti ya TAMISEMI:
https://selform.tamisemi.go.tz/Content/selection-and-joining-instructionsChagua Mkoa – Kilimanjaro
Tafuta jina la shule aliyopewa mwanafunzi
Pakua Joining Instruction kwenye mfumo wa PDF na uchapishe au hifadhi kwenye kifaa chako
Hakikisha unaisoma fomu hiyo vizuri pamoja na mzazi au mlezi ili kujiandaa kikamilifu.