JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

Vidonge vya uzazi wa mpango, pia vinavyojulikana kama vidonge vya majira (oral contraceptives), ni mojawapo ya njia maarufu za kuzuia ujauzito. Hizi ni dawa za mfululizo zinazotumika kila siku ili kudhibiti mzunguko wa homoni mwilini, na hivyo kuzuia mimba. Kutumia vidonge vya uzazi wa mpango kwa usahihi ni muhimu ili kuzuia ujauzito na kupunguza madhara yanayoweza kutokea.

Aina za Vidonge vya Uzazi wa Mpango

Vidonge vya uzazi wa mpango vinapatikana katika aina mbili kuu:

  • Vidonge vya mchanganyiko: Hivi ni vidonge vinavyojumuisha homoni mbili, estrogeni na progestin. Hii ni aina ya kawaida na hutumika kwa wanawake wengi.

  • Vidonge vya progestin pekee: Hivi ni vidonge ambavyo vina progestin pekee, bila estrogeni. Hii ni bora kwa wanawake ambao hawawezi kutumia estrogeni kutokana na matatizo ya kiafya.

Njia zingine za kuanza matumizi ya vidonge vya majira

Kuna njia nyingine mbili za kuanza kutumia vidonge mchanganyiko vya majira ni ambazo ni;

Kuanza jumapili

Kama umechagua kuanza jumapili, unapswa usubiri ifike jumapili ya kwanza tangu umeanza ona hedhi kisha anza kunywa dawa kama kwenye hatua ya pili na endelea kwenye hatua zinazofuata kama ilivyoandikwa hapo juu. Kama unachangua njia hii, utapaswa ongeza njia nyingine ya uzazi wa mpango (kondomu au viua manii) kwa siku 7 za mwanzoni mwa mzunguko tu.

Kuanza leo

Kama umeshiriki ngono isiyo salama kwenye hedhi yako ya mwisho, unapaswa pima ujauzito kwanza kabla ya kuanza matumizi ya vidonge vya majira. Kama huna ujauzito, anza vidonge vya majira na fuata hatua namba 2 na kuendelea. Utapaswa ongeza njia nyingine ya uzazi wa mpango (kondomu au viua manii) kwa muda wa siku 7 mfululizo tangu umeanza kutumia vidonge hivi ili kuzuia uwezekano wa kupata mimba.

Faida za Vidonge vya Uzazi wa Mpango

  • Ufanisi wa Juu: Vidonge vya uzazi wa mpango ni vyenye ufanisi mkubwa, na ikiwa vitachukuliwa kwa usahihi, hutoa kinga ya asilimia 99 dhidi ya mimba.

  • Kudhibiti Mzunguko wa Hedhi: Vidonge vinasaidia kudhibiti mzunguko wa hedhi, na hivyo kusaidia wanawake wenye matatizo ya hedhi isiyo ya kawaida.

  • Kupunguza Maumivu ya Hedhi: Kwa wanawake wenye maumivu makali ya hedhi, vidonge vya uzazi wa mpango vinaweza kusaidia kupunguza maumivu hayo.

  • Faida kwa Ngozi: Vidonge vya uzazi wa mpango vinaweza kusaidia kupunguza chunusi na matatizo mengine ya ngozi kwa baadhi ya wanawake.

Soma hii :Madhara ya kitanzi Cha Uzazi wa Mpango

 Madhara na Hatari za Vidonge vya Uzazi wa Mpango

Vidonge vya uzazi wa mpango ni salama kwa wanawake wengi, lakini kuna madhara yanayoweza kutokea, ikiwa ni pamoja na:

  • Maumivu ya kichwa, kichefuchefu, au kizunguzungu: Haya ni madhara ya kawaida kwa baadhi ya wanawake, hasa mwanzoni mwa matumizi.

  • Mabadiliko ya mood: Wanawake wengine wanaweza kujihisi mabadiliko ya kihisia kama huzuni au hasira.

  • Hatari ya kuongezeka kwa shinikizo la damu: Vidonge vya uzazi wa mpango vinaweza kuathiri shinikizo la damu, hivyo wanawake wenye shinikizo la damu la juu wanapaswa kuwa waangalifu.

Maswali yanayouizwa Mara kwa Mara dhidi ya vidonge vya Majira FAQS

Je unapaswa kutumia njia zingine za uzazi wa mpango?

 

Ndio unashauriwa kutumia njia zingine za uzazi wa mpango kwa muda wa mwezi mmoja toka umeanza kutumia vidonge vya majira ili kuzuia uwezekano wa kupata ujauzito. Baada ya kutumia majira kwa mwezi mmoja mfululizo, unaweza acha njia nyingine(kondomu) na kuendelea na majira.

Je kama umetapika au kuharisha ufanyaje?

Kama umetapika dawa ndani ya masaa 3 baada ya kunywa vidonge vya majira, unapaswa kunywa kidonge kingine haraka iwezekanavyo kisha endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa.

Kama ukiendelea kutapika, unashauriwa kutumia njia nyingine ya uzazi wa mpango mpaka pale utakapoweza kutumia dawa kwa siku 7 mfululizo bila kutapika.

Kama unaharisha sana (mara 6 hadi 8 kwa siku) hii humaanisha unapoteza maji mengi na kiasi cha dawa kinachofyonzwa hupungua pia na kinachoingia kinaweza kutozuia ujauzito. Kama ukipatwa na hali hii, endelea kutumia vidonge vya majira na njia nyingine ya uzazi wa mpango kwa siku mbili zaidi toka umefunga kuharisha.

Kama umesahau kutumia kidonge cha majira ufanyaje?

Unaweza kupata maelezo haya kwenye vidonge vya majira katika mada za dawa za ulyclinic.

Dalili za hatari kwa mtumiaji wa vidonge vya majira

Kama utapata dalili zifuatazo, acha kunywa vidonge vya majira na wasiliana na daktari wako mara moja;

  • Maumivu makali ya kichwa au maumivu endelevu

  • Maumivu kwenye machp au uono hafifu

  • Maumivu makali kwenye vigimbi vya miguu (misuli ya miguu)

  • Maumivu makali ndani ya kifua au maumivu wakati wa kupumua

  • Kupooza au ganzi kwenye mikono, miguu au uso

JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA
Share.

Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati

Leave A Reply