Batiki ni sanaa ya kipekee ya kupamba vitambaa kwa kutumia rangi na wax (nta). Sanaa hii imekuwepo kwa muda mrefu na inajulikana kwa muundo wake wa kuvutia na rangi zinazong’aa. Ikiwa unataka kutengeneza batiki nzuri zenye ubora wa hali ya juu, fuata mwongozo huu wa hatua kwa hatua.
Malighafi zinazotumika kutengeneza batiki
Kitambaa kiwe cha pamba
Sodium hydrosulfet
Caustic soda
Rangi
Mkasi
Kamba
Maski
Gloves
SOMA HII : Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Mche (Sabuni ya Kipande)
Baadhi ya mauwa yatokanayo na batiki ya kufunga kwa kamba:
Nyota
Kashata
Sambusa
Mji kati
Misalaba
Misalaba ndani ya drafti
Miraba
Mbavu
JINSI YA KUTENGENEZA.
(a)JINSI YA KUGONGA MISHUMAA:
Chemsha mshumaa uchemke sawasawa kisha ipua upoekidogo.Andaa kitambaa cha cotton na kukitandika mezani,chovya kibao chenye picha kwenye mshumaa kisha gonga kwenye kitambaa na kuacha nafasi kidogo.Endelea kugonga picha hizo mpaka kitambaa kiishe.
(b)JINSI YA KUWEKA RANGI:
Chemsha maji ya moto yachemke sawa sawa kisha pima lita tano mpaka sita.Baada ya hapo pima caustic soda vijiko3 na sodium hydrosulphate vijiko vinne mpaka vitano.Changanya na maji ya moto,weka rangi kijiko kimoja.Baada ya hapo pima maji lita kumi na tano na changanya na mchanganyiko wa madawa ili maji yawe vuguvugu.Tumbukiza vitambaa vya vinne vya mita tatu kwa wakati mmoja na kuvigeuzageuza viingie rangi kwa dakika kumi mpaka kumi na tano.Suuza kwa maji baridi na uanike kwenye kivuri ili mshumaa usiyeyuke.
(c)KUWEKA RANGI YA PILI:
Katika kuweka rangi hii kinachofanyika ni kuongeza vipimo vya ranagi tu.Ongeza vipimo vya rangi viwili na zaidi ya mala ya kwanza,maji,mudani uleule,
Weka mshumaa sehemu ambayo haina mshumaa kwa kutumia urembo uleule.Pima rangi kwa kufuata hatua zilezile.Tumbukiza vitambaa vitatu,geuza kwa mda uleule kisha anika.
(d)JINSI YA UFUA MSHUMAA:
Chemsha maji yachemke vizuri,changanya na sabuni ya unga jikoni,tumbukiza kitambaa kimoja kimoja jikoni ili kutoa mshumaa,geuza kwa mti,suuza kwenye maji ya baridi yaliyochanganywa na maji.