Usajili wa Jina au kampuni Brela kunamuwesha mfanyabiashara kulinda hatimiliki ya jina au kampuni yake ili isitumiwe au kusajiliwa na mtu mwingine yeyote,Makala hii itakupa muongozo na gharama za usajili wa kampuni au Jina la kampuni Brela.
Hatua muhimu za kufuata wakati wa kufanya usajili wa kampuni au jina la biashara
- Kulipia angalau 60% ya malipo yote, Kutuma taarifa zinazotakiwa (taarifa za kampuni, wenye hisa, wakurugenzi, katibu, hisa nk) – siku ya kwanza
- Utengenezaji wa nyaraka muhimu za usajili, utiaji saini na kupigwa muhuri wa mwanasheria – siku ya pili
- Kuanza mchakato wa maombi masafa na kupakia taarifa kwenye mtandao – siku ya tatu
- Kufanya malipo ya usajili BRELA na kutuma maombi – siku ya tatu
- BRELA kuyafanyia kazi maombi kwa kuhakiki na kutoa mapendekezo kama yapo – siku ya nne, saa nyingine hapa huchukua siku nyingi zaidi hadi 3 au zaidi ya hapo
- Kuyafanyia kazi mapendekezo ya BRELA kama yapo kama hayapo ndio mwisho. Kama marekebisho yapo, mchakato unarudi pale marekebisho yalipofanyikia. mfano kama marekebisho yamefanyikia hatua ya kwanza, mchakato wote unaanzia hapo nk – siku ya tano
- Kumalizia malipo 40% na kukabidhiwa vyeti na MemArt katika mfumo wa PDF
Kumb:
- Mchakato wote huchukua siku tano (5) kama BRELA hawakupendekeza marekebisho
- Siku za mchakato zinaweza kupungua kutoka siku tano (5) hadi siku tatu (3) kama taarifa zilizoletwa na mteja ni sahihi, zinajitosheleza na zimeletwa kwa kuwahi.
- Ikiwa BRELA watarudisha marekebisho ya jina au taarifa zingine, mzunguko wa mchakato utarudi na kuanzia pale marekebisho yamefanyika. mfano kama marekebisho ni ya jina basi mchakato utarudi na kuanzia kwenye hatua ya kwanza japo utekelezaji wake utaenda kwa haraka zaidi kwa sababu ni marekebisho tu. Kama marekebisho ni ya ujazaji wa fomu za BRELA tu basi mchakato utarudi kwenye hatua ya tatu nk.
- Mteja atalazimika kupendekeza majina ya kipekee (Unique names) matatu (3) kwa ajili ya usajili na jina la kwanza likibeba uzito zaidi ya jina la pili na kadhalika jina la pili likibeba uzito zaidi ya jina la tatu.
- Idadi ya marekebisho ya jina inayoruhusiwa kwa ada ile ile ni matatu tu, zaidi yahapo mteja atawajibika kulipa Shilingi elfu ishirini (Shs. 20,000) kwa kila jina linaloongezeka.
Hatua za Kusajili Kampuni Kupitia Website ya BRELA
Hatua #1: Taarifa za msajili
Ili kutumia mfumo huu mpya wa ORS mteja (msajili) anayetaka kusajili jina la kampuni anatakiwa kuwa na taarifa za msajili (msajili anaweza kuwa ni mmoja wa wakurugenzi, Katibu au Wanachama/Wenye hisa wa Kampuni tarajiwa).
Taarifa zenyewe ni:-
- Kitambulisho cha Taifa kwa wenyeji na Passport kwa wageni
- Simu ya kiganjani
- Barua pepe yaani email
Hatua #2: Taarifa za kampuni
Taarifa za kampuni zinazotakiwa ni:-
- Aina ya kampuni kama ni ya hisa au isiyo na hisa, ya binafsi au ya uma nk
- Jina la kampuni
- Tarehe ya kufunga mahesabu – mfano 31 Desemba
- Kumbuka: TIN No., Namba ya usajili zitawekwa na mfumo automatically
Hatua #3: Ofisi za kampuni
Taarifa za ilipo au itakapokuwa ofisi za kampuni ambazo ni:-
- Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
- Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
- Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, kitalu na nyumba,
- Sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
- Region: Arusha
- District: Arusha CBD
- Ward: Unga Limited
- Postal: code 23107
- Mtaa: Viwandani,
- Kitongoji: Olevolosi
- Karibu na kiwanda cha ATOZ
- Region: Arusha
- District: Arusha CBD
- Ward: Kati
- Postal code: 23102
- Street: New Livingstone Street
- Road: New Livingstone Road
- Plot number: 91
- Block number: F
- House number: 704
Hatua #4: Shughuli za Kampuni
- Taja shughuli za kampuni kama ilivyoorodheshwa kwenye mfumo wa ISIC Classification
Hatua #5: Taarifa za wakurugenzi
Taarifa zinazotakiwa za Wakurugenzi ni:-
- Aina ya mkurugenzi kama ni mtu au taasisi
- Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
- Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
- TIN
- Simu ya kiganjani
- Barua pepe yaani email
- Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
- Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
- Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
- Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
- Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, kitalu na nyumba,
- Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
- Simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
Hatua #6: Taarifa za katibu wa kampuni
Taarifa za katibu wa kampuni (company secretary) zinazotakiwa ni:-
- Aina ya mtu kama ni mtu asili au taasisi
- Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
- Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
- Simu
- Barua pepe – email
- Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
- Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
- Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
- Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
- Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, kitalu na nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
- Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
- Simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email na (sanduku la posta kwa ajili ya memart)
Hatua #7: Taarifa za wanachama/wenye hisa
Taarifa za wanachama au wenye hisa zinazotakiwa ni:-
- Aina ya mtu kama ni mtu au taasisi
- Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
- Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
- Simu
- Barua pepe – email
- Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
- Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
- Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
- Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
- Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, kitalu na nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
- Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
- Simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email na (sanduku la posta kwa ajili ya memart)
- Thamani ya hisa za mtaji mfano mil 20
- Mgawanyo wa hisa kwa wanachama kwa namba au asilimia( mfano hisa za Mil. 20M halafu mwenye hisa wa kwanaza 60% na wa pili 40%= mgawanyo utakuwa hivi. Asume kila hisa itakuwa na thamani ya 100,000 na kwa hiza za Mil 20 utakuwa na jumla ya hisa 200, wa kwanza atapata hisa 120 (60%) na wa pili atapata hisa 80 (40%))
Hatua #8: Viambatanisho
Viambatanisho vinavyotakiwa kuambatanisha kwenye maombi (zote katika pdf) ni:-
- Memorandum and articles of association iliyosainiwa na wanachama/wenye hisa pamoja na mwanasheria wa uma (Notary Public)
- Form 14b iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi na mwanasheria wa uma (Notary Public)
- Ethics and Integrity Forms iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi
- Company consolidated form iliyosainiwa wakurugenzi wote na katibu wa kampuni
Hatua #9: Ada za usajili na kufaili
Malipo ya ada ni kama ilivyoonyeshwa hapa chini
- Kusajili kampuni
- Kuhifadhi nyaraka na
- Stamp Duty
Hatua #10: Namna ya kulipa ada
Malipo ya ada yanafanyika kwa njia kuu mbili ambazo ni
- Simu ya mkononi kwa kutumia akaunti za MPESA, Tigo Pesa, Airtel Money, HaloPesa
- Kulipa moja kwa moja benki kwenye akaunti zilizopo CRDB au NMB
Kumbuka: Utaratibu wa malipo aidha kwa simu au benki utapewa ukishafikia hatua husika ya malipo
Hatua za Kusajili Biashara Kupitia Website ya BRELA
Hatua #1: Taarifa za msajili, mmiliki au wamiliki wa biashara
- Kitambulisho cha Taifa kwa wenyeji na Passport kwa wageni
- Simu ya kiganjani
- Barua pepe yaani email
Hatua #2: Taarifa za biashara
- Aina ya biashara mtu binafsi, washirika au shirika
- Jina la biashara
Hatua #3: Ofisi ya biashara (Business Location)
- Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
- Kama halijapimwa tayarisha anuanii ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa.
- Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, namba ya kitalu na namba ya nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe (email)
- Region: Arusha
- District: Arusha CBD
- Ward: Unga Limited
- Postal: code 23107
- Mtaa: Viwandani,
- Kitongoji: Olevolosi
- Karibu na kiwanda cha ATOZ
- Region: Arusha
- District: Arusha CBD
- Ward: Kati
- Postal code: 23102
- Street: New Livingstone Street
- Road: New Livingstone Road
- Plot number: 91
- Block number: F
- House number: 704
Hatua #4: Shughuli za Biashara (Business Activities)
- Taja shughuli za biashara kama ilivyoorodheshwa kwenye mfumo wa ISIC Classification
Hatua #5: Taarifa za Wamiliki (Business Owner’s Information) pamoja na Akaunti ya Benki kama ipo
- Aina ya mmiliki kama ni mtu au taasisi
- Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
- Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
- TIN
- Simu ya kiganjani
- Barua pepe yaani email
- Anuani ya makazi kwa kila mmiliki kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
Hatua #6: Taarifa za Akaunti ya Benki Zingine kama ipo (Business Bank Account Information)
- Aina ya mmiliki kama ni mtu au taasisi
- Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
- Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
- TIN
- Simu ya kiganjani
- Barua pepe yaani email
- Anuani ya makazi kwa kila mmiliki kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
Hatua #7: Taarifa za Wawakilishi (Person who can update ORS Information)
- Aina ya mmiliki kama ni mtu au taasisi
- Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
- Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
- TIN
- Simu ya kiganjani
- Barua pepe yaani email
- Anuani ya makazi kwa kila mmiliki kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
Hatua #8: Viambatanisho (Attachments in PDF)
Viambatanisho vinavyotakiwa kuambatanisha kwenye maombi (zote katika pdf) ni:-
- Consolidated form iliyosainiwa wamiliki wote wa biashara
- Viambatanisho vingine vinakuja
Hatua #9: Ada za usajili na kufaili (Different Fees)
Aina za ada ni kama ilivyoonyeshwa hapa chini
- Kusajili biashara = TZS. 15,000
- Kuhifadhi nyaraka na = TZS. 5,000/mwaka
- Stamp Duty = TZS. 500
Hatua #10: Namna ya kulipa ada (Payment Methods)
Malipo ya ada yanafanyika kwa njia kuu tatu ambazo ni
- Kuweka Benki: Kwa njia ya kuweka Fedha kwenye Tawi la Benki /Wakala wa Benki
Nenda kwenye Tawi lolote la Benki / Wakala wa Benki ya CRDB /NMB kwa kutumia Namba ya Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako - Kwa njia ya Simu ya Mkononi: Tumia mtandao wa simu wa AirTell Money / Tigopesa/ MPesa/ HalloPesa kwa kuweka namba ya Kampuni 888999 na Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
- Kwa njia ya Kuhamisha Fedha: Unaweza kuhamisha Fedha moja kwa moja kutoka katika Benki yoyote kwenda kwenye Akaunti zetu zilizoko katika Benki ya NMB/ CRDB kwa njia ya TISS /SWIFT kwa kujaza: Namba ya Akaunti na Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
Kumbuka: Utaratibu wa malipo aidha kwa simu au benki utapewa ukishafikia hatua husika ya malipo