Jinsi ya Kupata kadi ya CCM (Kadi ya Uanachama chama cha Mapinduzi)

Jinsi ya Kupata kadi ya CCM (Kadi ya Uanachama chama cha Mapinduzi)
Jinsi ya Kupata kadi ya CCM (Kadi ya Uanachama chama cha Mapinduzi)

Watu wengi Vijana kwa wazee wanautiwa kujiunga na Chama cha mapinduzi kwa Malengo mbalimbali ikiwemo kuweza kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama na katia serikali kwa Ujumla Hapa tumekuwekea Hatua za Jinsi ya kupata adi ya chama cha mapinduzi (ccm).

Sifa za Kuwa Mwanachama wa CCM

Ili kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi, ni muhimu kufikia vigezo vifuatavyo:

  1. Kuwa Mtanzania mwenye umri wa angalau miaka 18.

  2. Kukubaliana na Itikadi, Katiba, Kanuni na Malengo ya CCM.

  3. Kuwa tayari kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za chama katika eneo lako.

  4. Kujaza fomu ya uanachama na kutoa taarifa sahihi kuhusu jina lako, makazi, namba ya simu, nk.

  5. Kulipia ada ya uanachama inayowekwa na chama husika (kawaida ni kati ya TZS 2,000 – 3,000).

  6. Kukubali kuwa mtiifu kwa viongozi wa chama na kuheshimu taratibu zake.

Sifa za Kugombea Uongozi Katika Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Kama unalenga kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya CCM, unatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:

  1. Uwe mwanachama halali wa CCM mwenye kadi ya chama.

  2. Uwe na uzoefu wa kushiriki katika shughuli za chama angalau kwa kipindi fulani (kawaida ni si chini ya miaka 5 kwa nafasi za juu).

  3. Uwe na tabia njema na mwenendo unaoendana na maadili ya CCM.

  4. Uwe na elimu inayohitajika kwa nafasi husika (kulingana na ngazi ya nafasi).

  5. Uwe hujawahi kushitakiwa au kuhukumiwa kwa kosa la jinai au ubadhirifu.

  6. Kujaza fomu ya kugombea na kulipia ada ya kugombea kama itakavyotangazwa na chama.

Jinsi ya Kupata Kadi ya CCM

Kupata kadi ya CCM ni mchakato rahisi unaohusisha hatua chache muhimu:

1. Tembelea Ofisi ya CCM ya Kata au Tawi

  • Nenda kwenye ofisi ya CCM iliyo karibu nawe.

  • Omba fomu ya kujiunga na chama.

SOMA HII :  Jina la mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Tanzania

2. Jaza Fomu ya Uanachama

  • Jaza taarifa zako binafsi kama:

    • Jina kamili

    • Tarehe ya kuzaliwa

    • Anuani

    • Namba ya simu

    • Elimu na kazi

  • Weka sahihi yako na picha (ikiwa inahitajika).

3. Lipia Ada ya Uanachama

  • Ada ya kupata kadi ni nafuu, kawaida ni kati ya TZS 2,000 – 3,000.

  • Malipo yanaweza kufanyika ofisini au kwa njia ya simu kwa kutumia control number ya serikali (malipo ya serikali mtandao).(Jinsi ya kulipia kadi ya ccm kwa simu)

4. Subiri Kadi Yako

  • Baada ya malipo na uchakataji wa maombi yako, utapewa kadi ya chama ikiwa ni ushahidi wa uanachama wako.

  • Baadhi ya maeneo huweza kutoa kadi ya muda hadi ile ya kudumu itakapopatikana.

5. Jiunge na Tawi lako

  • Mwanachama hutakiwa kujiunga na tawi la CCM katika eneo analoishi ili kushiriki kikamilifu kwenye vikao, shughuli na maamuzi ya chama.

About Burhoney 4806 Articles
Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati