Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni chama kikuu cha siasa nchini Tanzania ambacho kimeongoza taifa tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977, baada ya muungano wa TANU na ASP. Ikiwa na historia ndefu ya uongozi, CCM imeendelea kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za Tanzania. Watu wengi hujiuliza jinsi wanavyoweza kuwa wanachama wa chama hiki kikongwe.
SIFA ZA KUWA MWANACHAMA WA CCM
Kabla ya kujiunga na CCM, ni muhimu kuhakikisha unakidhi vigezo vya msingi vilivyowekwa na chama. Sifa hizo ni pamoja na:
Kuwa Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea.
Kuamini na kukubali Itikadi, Malengo, Sera na Katiba ya CCM.
Kuwa na tabia njema na kutohusika na vitendo vinavyokiuka maadili ya jamii.
Kuwa tayari kushiriki shughuli za chama na kutii maelekezo ya viongozi wa chama.
Kutokuwa mwanachama wa chama kingine cha siasa.
JINSI YA KUWA MWANACHAMA WA CCM
Ikiwa umetimiza sifa hizo, unaweza kujiunga na CCM kwa kufuata hatua hizi:
Tembelea Tawi la CCM lililo karibu nawe (kata au mtaa).
Jaza fomu ya maombi ya uanachama – fomu hii hupatikana ofisi ya chama au kwa njia ya mtandao (kwa baadhi ya maeneo).
Toa picha ndogo mbili za pasipoti kwa ajili ya kadi ya uanachama.
Lipa ada ya uanachama – kiasi cha ada kinaweza kutofautiana kidogo kulingana na eneo au uongozi husika.
Subiri uhakiki wa maombi yako – kamati ya tawi au kata itapitia maombi yako na kukupatia taarifa za uanachama mara baada ya kuidhinishwa.
Kukabidhiwa kadi ya uanachama – ukishathibitishwa, utapewa kadi rasmi ya CCM inayokutambulisha kama mwanachama halali.
Soma Hii :Jinsi ya Kupata kadi ya CCM (Kadi ya Uanachama chama cha Mapinduzi)
MAKOSA GANI YANAYOWEZA KUKUFUKUZISHA UANACHAMA WA CCM
Uanachama wa CCM ni wa heshima, hivyo kuna baadhi ya makosa ambayo yanaweza kusababisha mtu kupoteza haki hiyo, ikiwemo:
Kukiuka maadili ya chama au kutenda vitendo vinavyoharibu taswira ya CCM.
Kuhusika na rushwa au ufisadi ndani au nje ya shughuli za chama.
Kutoa siri za chama kwa vyama pinzani au watu wasiohusika.
Kushiriki katika propaganda au vitendo vinavyopinga chama.
Kutoruhusu ukaguzi wa mwenendo wa mwanachama unapohitajika.
Kuwa mwanachama wa chama kingine cha siasa kinyume na Katiba ya CCM.
MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA KUHUSU UANACHAMA WA CCM
1. Je, naweza kujiunga na CCM nikiwa mwanafunzi?
Ndiyo. Mradi una umri wa miaka 18 au zaidi, na unakidhi sifa nyingine, unaweza kujiunga hata kama bado unasoma.
2. Ni lazima kuwa na kadi ya mpiga kura ili kujiunga na CCM?
Hapana. Kadi ya mpiga kura si sharti la kuwa mwanachama, lakini utahitajika kutoa uthibitisho wa uraia na umri wako.
3. Je, ada ya uanachama ni kiasi gani?
Ada inaweza kutofautiana kidogo kulingana na eneo, lakini kwa kawaida ni kati ya shilingi elfu tano hadi elfu kumi kwa mwaka.
4. Naweza kujiunga na CCM kupitia mtandaoni?
Katika maeneo mengine, huduma hii inawezekana kupitia tovuti rasmi ya CCM, lakini bado ofisi za mtaa/kata ndizo zenye mamlaka ya mwisho.
5. Je, kuna faida gani kuwa mwanachama wa CCM?
Kuwa mwanachama hukupa nafasi ya kushiriki maamuzi ya chama, kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, na kushiriki katika maendeleo ya taifa kupitia chama.