Close Menu
swahiliforums.com
  • Home
  • Ajira Mpya
  • Elimu
  • Michezo
  • Makala
Facebook X (Twitter) Instagram
swahiliforums.com
BOFYA HAPA
  • Home
  • Ajira Mpya
  • Elimu
  • Michezo
  • Makala
Facebook X (Twitter) Instagram
swahiliforums.com
Home » Jinsi ya Kulipia Leseni za biashara Online katika (TAUSI PORTAL)
Biashara

Jinsi ya Kulipia Leseni za biashara Online katika (TAUSI PORTAL)

BurhoneyBy BurhoneyMarch 15, 2025Updated:March 15, 2025No Comments5 Mins Read
Share Facebook Twitter Telegram WhatsApp
Jinsi ya Kulipia Leseni za biashara Online katika (TAUSI PORTAL)
Jinsi ya Kulipia Leseni za biashara Online katika (TAUSI PORTAL)
Share
Facebook Twitter Telegram WhatsApp
JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

Leseni ya biashara ni kibali cha kisheria kinachotolewa na mamlaka husika ili biashara yako ifanye kazi kwa mujibu wa sheria za nchi au mkoa. Leseni hii inahakikisha kuwa biashara yako inafuata kanuni na sheria zinazohusiana na mazingira, usalama, afya, na kodi.

Leseni hizi zinatolewa na mamlaka za serikali, mamlaka za mitaa, na hata taasisi maalum kulingana na aina ya biashara unayoanzisha. Kwa mfano, biashara za chakula, dawa, na huduma za afya zinahitaji leseni maalum zinazohusiana na udhibiti wa afya na usalama.

Mahitaji Muhimu

Ili kuanza mchakato wa kulipia leseni ya biashara mtandaoni, unahitaji kuwa na vitu vifuatavyo:

  • Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIDA)
  • Barua pepe inayofanya kazi
  • Namba ya simu
  • Taarifa za biashara yako

kupata leseni y biashara hakikisha una TIN namba toka TRA

 UTARATIBU WA KUPATA LESENI ZA BIASHARA

 

 

Leseni zote za Biashara hutolewa chini ya sheria ya Biashara Na.25 ya Mwaka 1972 na Marekebisho yake yaliyofanyika june 2014 pamoja na marekebisho katika sheria ya Fedha Na.2 ya Mwaka 2014 na Na.16 ya Mwaka 2015. Mwombaji wa leseni ya biashara  anapaswa ajaze fomu ya maombi ya leseni TFN211 (Business application form).

Mtu yeyote raia wa Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya biashara ili mradi awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane(18) Mwenye akili timamu ambaye hajawahi kupatikana na kosa la jinai na awe na eneo la kufanyia biashara kisheria.

Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania anapaswa kuwa na kibali kinacho mruhusu kufanya biashara nchini kutoka idara ya uhamiaji.

LESENI ZA BIASHARA ZIMEGAWANYIKA KATIKA MAKUNDI MAWILI:

KUNDI A;Leseni hizi hotelewa na Wizara ya Viwanda ,Bishara na Uwekezaji.(Fomu ya maombi iwasilishwe na Halmashauri kabla ya kupelekwa Wizarani)

Mfano;

  • Uagizaji bidhaa toka nje(import licence)
  • Kusafirisha bidhaa nje (Export licence)
  • Hotel za kitalii (Tourist Hotel& Lodging)
  • Wakala wa kupokea na kusafirisha mizigo (Clearing and Fowarding/Freight Forwarders) n.k

KUNDI B:Hizi hutolewa na Halmashauri za Wilaya,Manispaa,Miji na Majiji husika.

Mfano:

  • Wakala wa Bima (Insurance Agent)
  • Vipuri (Spare parts,Mshine tools)
  • Maduka ya dawa za Binadamu/Mifugo
  • Viwanda Vidogo (Small Scale Manufacturely and Selling)
  • Uuzaji Bidhaa Jumla na Rejareja (Wholesale and Retail trade) n.k

UTARATIBU WA KUPATA LESENI ZA BIASHARA

Kila Mfanyabiashara anatakiwa afike ofisi ya Biashara katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kwa ajili ya kuchukua fomu na kujaza kama utakavyoelekezwa .Baadhi ya nyaraka zinazohitajika kama kiambatanisho na masharti katika fomu ya maombi (TFN221) ni ;

  • Mfanyabiashara anapaswa awe na hati ya usajili iwapo anatumia jina la biashara      ( Certificate of Registration or Incorporate).
  • Kama ni Kampuni mwombaji awe na memorandum and Article of Association ambazo zinaonyesha kuwa kampuni imeruhusiwa kufanya biashara anayoiomba.
  • Mwombaji awe na umri wa miaka 18 au zaidi
  • Awe na mahali/Eneo linalokubalika kwa aina ya biashara anayoiomba  na isiwe vidanda vilivyopo kando kando ya barabara.
  • Awe na TIN certificate.
  • Awe na hati ya kuthibitisha uraia wake kama,Nakala ya Hati ya Kusafirisha”passport”ya Tanzania,cheti cha kuzaliwa au Hati ya kiapo(Affidavit) au Kitambulisho cha Mpiga kura.Kama ni mgeni awe na hati ya kuishi nchini daraja la “A” (Resident Permit Class “A”.)
  • Masharti mengine ya kupata leseni hutegemea aina ya biashara mtu anayetaka kuanzisha  e.g. Mgahawa,Dawa za Binadamu na Mifugo,Vyakula,Nyama na Samaki inabidi afuate taratibu zote za afya na kupima wafanyakazi wake
  • Hati ya Utaalam (Professional Certificates) kwa biashara zote za kitaalam
  • Maombi mapya yatapitia ngazi za Serikali ya Mtaa/kijiji ,Afya na Kisha ofisi ya biashara kwa ajili ya utoaji wa leseni.

MALIPO:Kutokana na marekebisho ya sheria ya fedha Na 2 ya mwaka 2014 ada za leseni hulipwa kulingana na aina ya biashara kama ilivyoanishwa katika jedwali la viwango vya ada kwa mwaka

MUDA WA LESENI: Umri wa leseni ni miezi 12 toka siku ya kutolewa.

 

MASHARTI YA UTUMIAJI WA LESENI

1.Mwenye leseni hataweka masharti yeyote kwa mnunuzi

2. Mwenye leseni atatoa risiti kwa mauzo yote.

3.Mwenye leseni atafuata sheria ya leseni ya biashara No. 25 ya 1972

4.Mwenye leseni hatatoa huduma/bidhaa ambazo hazizingatii viwango vya ubora,uliowekwa na Vyombo vinavyotumika kisheria

5.Mwenye leseni anaweza kunyang’anywa wakati wowote ikiwa inaonekana aliipata kwa njia ya udanganyifu au amekiuka masharti ya leseni.

MAKOSA

1.Kuendesha biashara bila leseni

2.Kuendesha biashara eneo tofauti na linaloonyeshwa kwenye Leseni.

3.Kutumia leseni moja kufanya biashara zaidi ya moja au maeneo mawili au zaidi

4.Kushindwa kuonyesha leseni ya biashara inapotakiwa kufanya hivyo na Afisa aliyedhinishwa na Serikali.

5.Kutokuweka leseni ya biashara mahali ambapo inaonekana kwa urahisi (Kuficha leseni).

6.Kutoa maelezo ya uongo ili kupata leseni au kukwepa kulipa ada /kodi inayostahili

7.Kumzuia Afisa wa Serikali aliyepewa mamlaka ya kukagua kufanya kazi yake.

ADHABU;  (i). Mtu yeyote anayetenda mojawapo ya makosa hapo juu adhabu yake ni faini isiyopungua Tsh 50,000/= na isiyozidi Tsh 100,000/= au kifungo kisichozidi miaka miwili(2) au faini na kifungo kwa pamoja.

(ii). Mtu yeyote atakayechelewa kuhuisha leseni yake baada ya siku 21 baada ya     muda wa leseni kuisha atalipia asilimia 25 ya ada iliyotakiwa kulipia na itaongezeka asilimia 2 kila mwezi kadri mfanyabiashara anavyochelewa kuhuisha leseni ya biashara

NB.Wafanyabiashara wote wanaaswa kufuata na kutekeleza sheria bila shuruti,kwani kutofanya hivyo kunawaingiza gharama zisizo za lazima kama faini na kupoteza muda hasa pale wanapokutwa na makosa

Hatua za Kulipia Leseni ya Biashara Mtandaoni

  1. Tembelea TAUSI PORTAL: Anza kwa kufungua TAUSI PORTAL kwenye kivinjari chako.
  2. Jisajili: Kama hujawahi kutumia mfumo huu, utahitaji kujisajili kwa kutoa taarifa zako za msingi kama vile jina, barua pepe, na namba ya simu.
  3. Jaza Fomu ya Maombi: Baada ya kujisajili, jaza fomu ya maombi ya leseni ya biashara kwa kutoa taarifa zote muhimu za biashara yako.
  4. Pakia Viambatisho: Hakikisha unapakia viambatisho muhimu kama vile cheti cha usajili wa biashara na hati ya kutodaiwa kodi.
  5. Thibitisha Malipo: Malipo yanaweza kufanyika kupitia njia mbalimbali kama vile benki au huduma za kifedha za simu. Thibitisha malipo yako kupitia mfumo.
  6. Pokea Leseni Yako: Baada ya kuthibitisha malipo, utapokea leseni yako ya biashara kupitia barua pepe au unaweza kuipakua moja kwa moja kutoka kwenye portal.
JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA
Follow on Telegram Follow on WhatsApp
Share. Facebook Twitter Email Telegram WhatsApp
Burhoney
  • Website

Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati

Related Posts

Bei Ya Mafuta Ya Parachichi

April 15, 2025

Wauzaji wa ng’ombe wa maziwa Tanzania

April 15, 2025

Bei Ya Ng’ombe Wa Maziwa

April 15, 2025

Gharama za kusafirisha mizigo kwa treni

April 15, 2025

Gharama za kusafirisha mzigo au Bidhaa kutoka Zanzibar

April 15, 2025

Bei ya Simu za Oppo na Sifa zake (Specifications)

April 15, 2025
Leave A Reply Cancel Reply

Latest Posts

Nafasi 83 za Kazi Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) June 2025

June 12, 2025

Nafasi za Kazi – NARCO (Kampuni ya Ranchi za Taifa) – Juni 2025

June 12, 2025

Majina ya Walioitwa kazini Ajira Portal Utumishi PSRS 2025 PDF Download

June 12, 2025

Majina Ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI na Ajira Portal 2025

June 12, 2025

Matokeo ya Usaili Ajira Portal 2025 / 2026 Utumishi wa Umma PSRS

June 12, 2025
Load More

Subscribe to Updates

Usipitwe na Habari zetu za kila siku Kuwa wa kwanza kupata Habari zetu Kwa Kuandika Email yao Hapo chini

SwahiliForums Ni jukwaa la Habari na Makala mbalimbaali kwa Lugha kiswahili Habari za Michezo,Elimu, Biashara,Ajira Mpya na Dondoo za Afya Endelea kutufuatilia kwa kutembelea site yetu SwahiliForums.com

Karibu kwenye Swahiliforums, jukwaa lako la kipekee kwa habari, maarifa, na mijadala inayoangazia masuala ya kijamii, uchumi, na utamaduni kutoka kwa mtazamo wa Kiswahili. Hii ni blog ambayo inalenga kutoa taarifa za kina kuhusu matukio ya sasa, maisha ya kila siku, na masuala muhimu yanayoathiri jamii zetu katika eneo la Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla.

swahiliforums.com
Facebook X (Twitter) Instagram WhatsApp Telegram Pinterest
Copyrights reserved @2025 swahiliforum.com

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.