Kupanga uzazi ni uamuzi muhimu kwa wanawake na wanandoa wanaotaka kudhibiti uzazi na kupanga familia zao kwa utaratibu mzuri. Miongoni mwa njia nyingi za kupanga uzazi, kitanzi (au IUD – Intrauterine Device) ni mojawapo ya mbinu zinazotumika sana. Lakini, je, kitanzi ni njia salama ya kupanga uzazi?
Kitanzi ni Nini
Kitanzi ama intrauterine device ni kifaa chenye umbo la T kinachoingizwa kwenye kizazi cha mwanamke ili kuzuia mimba isitunge. Kinfanya kazi kwa kuzuia mbegu ya kiume isilifikie yai lililokomaa na kulirutubisha. Kitanzi kikitumika ipasavyo uwezo wake wa kuzuia mimba ni zaidi ya asilimia 99.
Aina za Kitanzi
Kuna aina kuu mbili za kitanzi cha Copper na kile cha homoni
Kitanzi cha homoni (Hormonal IUD)
Kitanzi cha homoni kinaitwa hivo kwasababu kinatoa kichocheo kiitwacho progestin. Kazi ya kichocheo hiki ni kufanya ute wa ukeni kuwa mzito kiasi ya kuzuia mbegu kulifikia yai. Progestin pia inafanya ukuta wa kizazi uwe mwembemba sana na hivo kuzuia upandikizaji.
Kitanzi cha copper (Copper IUD)
Kitanzi cha copper kinafanya kazi kwa kuua mbegu zinazoingia kwennye kizazi kabla hazijafikia kulirutubisha yai.
Faida za kitanzi cha Copper ni kwamba
- haivurugi mpangilio wa homoni
- kinaanza kufanya kazi mapema tu ukiweka
- Kinaweza kukaa mda mrefu mpaka miaka 10 na kikafanya kazi ya kuzuia mimba
Hasara zake ni pamoja na
Kupelekea upate hedhi nzito sana: Hii ni kwa baadhi ya wanawake na siyo wote. Aina hii ya kitanzi haifai kama unapataga hedhi nzito yenye maumivu makali.
Aleji ya copper: watu wenye aleji na madini ya copper njia hii haitawafaa
Ni zipi faida za Kutumia Kitanzi?
- kinaweza kutumika kwa muda mrefu bila kubadilisha
- huhitaji kukagua ama kufatilia mara kwa mara, ukishaweka mara moja tu kwa usahihi inatosha
- gharama yake ni nafuu na unalipia mara moja tu
- ni salama kutumia hata kama unanyonyesha
Ni watu gani wanapaswa kutumia kitanzi?
Wanawake wote wenye afya njema wanaweza kutumia kitanzi. Muhimu kumbuka kitanzi hakizuii kutoambukizwa magonjwa ya zinaa. Na usitumie kitanzi kama
- unaugua ugonjwa wa zinaa ama umeugua PID hivi karibuni
- ni mjamzito
- una saratani ya kizazi au ya shingo ya kizazi
- una tatizo la kutokwa damu kusiko kawaida
Je hedhi yangu itabadilika baada ya kuweka kitanzi?
Baadhi ya wanawake hupata maumivu kiasi kwenye hedhi baada ya kuweka kitanzi na hedhi kuwa nzito sana. Kwa miezi michache ya mwanzoni baadhi wanaweza kuona hedhi ikivurugika. Wanawake wengi hupata hedhi kidogo ama wengine hukosa kabisa hedhi.
Je Mwanaume Atakigusa Kitanzi Wakati wa Tendo la ndoa?
Kama kitanzi kimewekwa vizuri basi mwanaume ni ngumu kugusa kitanzi wakati wa tendo. Lakini hata kama ikitokea hivo basi haiwezi kupunguza ladha ya penzi kwasababu pia kamba fupi za kitanzi zinazobaki nje ya uke huendelea kuwa laini zaidi kadiri muda unavoenda.
Je kuna Madhara ya Kutumia kitanzi?
⚠️ Maumivu na kutokwa na damu zaidi – Baadhi ya wanawake hupata maumivu makali wakati wa kuwekewa kitanzi au huona hedhi nzito na yenye maumivu zaidi, hasa kwa kitanzi cha shaba.
⚠️ Mabadiliko ya hedhi – Kitanzi chenye homoni kinaweza kusababisha hedhi isiyo ya kawaida au hata kusimama kabisa kwa muda fulani.
⚠️ Hatari ya maambukizi – Ingawa ni nadra, kuna hatari ya maambukizi endapo kitanzi kitawekwa bila kufuata usafi wa hali ya juu au endapo kuna maambukizi ya zinaa.
⚠️ Kupitiliza au kutoka nje ya mfuko wa uzazi – Katika visa vichache, kitanzi kinaweza kuhamia sehemu isiyofaa au kutoka nje ya uterasi, hali inayohitaji matibabu.
PID
Kama utapata dalili za tumbo kujaa, kuvimba na maumivu makali chini ya kitovu muhimu uende hospitali haraka.
Kwa kiasi fuani matumizi ya kitanzi huongeza hatari ya kuugua PID, ambayo ni maambukizi kwenye kizazi, mirija na mifuko ya mayai.
Dalili za PID ikiwa ni pamoja na
- maumivu wakati wa tendo
- kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya ukeni
- hedhi nzito kupita kiasi na homa.
Muone daktari mapema kama unaanza kupata dalili hizi ili utibiwe na kuepusha madhara zaidi ikiwemo kuziba kwa mirija.
Je kitanzi kinaweza kutoka chenyewe ?
Daktari atakuchunguza kama kitanzi hakipo sawa kila mara unapotembelea hospitali. Kitanzi kinatakiwa kishikiliwe na shingo ya kizazi. Kwa baadhi ya wanawake kitanzi kinaweza kutoka nje ya kizazi.
Hali hii hutokea hasa kama
- hujawahi kuzaa
- una umri chini ya miaka 20
- umewekewa kitanzi mapema sana baada tu ya kuzaa au baada ya mimba kuharibika
- una vimbe(fibroids) kwenye kizazi
- kizazi chako kimeinama ama kina shape isiyo ya kawaida
Je vipi kama Nahitaji kuzaa kwa siku za baadae?
Kutumia kitanzi kwa watu wengi haitaathiri uwezo wako wa kushika mimba siku za baadae. Kama utafikia wakati unahitaji kubeba mimba ingine, tembelea hospitali onana na daktari muombe akutolee kitanzi. Baada ya hapo hedhi yako itarudi kuwa kawaida na utashika mimba mapema.
Je vipi kama sitashika mimba mapema?
Inatokea kwa wanawake wachache kupata madhara ya kitanzi, hasa kuvurugika kwa mazingira ya kizazi na hivo mimba kutoshika. Kwa grupu hili la wanawake tunawashauri kutumia hizi tiba asili ili kusafisha kizazi na kusaidia mayai kupevuka.
Je, Kitanzi ni Salama?
Kwa wanawake wengi, kitanzi ni njia salama na yenye ufanisi wa hali ya juu. Hata hivyo, si kila mwanamke anafaa kutumia kitanzi. Inashauriwa mwanamke amwone daktari au mtaalamu wa afya ili kupima kama kitanzi ni chaguo bora kwake.
Ikiwa unatafuta njia ya kudhibiti uzazi kwa muda mrefu, isiyo na usumbufu wa matumizi ya kila siku, na yenye ufanisi mkubwa, basi kitanzi kinaweza kuwa suluhisho sahihi. Walakini, kama una historia ya matatizo ya kiafya kama maambukizi ya mara kwa mara kwenye via vya uzazi au matatizo ya hedhi, ni vyema kujadiliana na mtaalamu wa afya kabla ya kuchagua njia hii.