Bei ya friji za Boss hutofautiana kulingana na ukubwa, aina ya friji (model), na muuzaji. Kwa wastani, unaweza kupata kwa bei kati ya Tsh 300,000 hadi Tsh 2,000,000 kwa friji mpya ya Boss kulingana na ukubwa. HIzi apa chini ndizo bei za friji za boss kwa ukubwa
Ukubwa | Bei | Muuzaji (Instagram Name) |
BS70 FRIDGE LITA 60 | 345,000 | kariakoo_mall |
Fridge Boss BS LITA 70 | 380,000 | kariakoo_mall |
BS70 FRIDGE LITA 90 | 410,000 | Friji_Beipoa |
BS70 FRIDGE LITA 100 | 450,000 | og_electronixtz |
BS70 FRIDGE LITA 145 | 620,000 | kariakoo_mall |
Fridge Boss BS 185 | 650,000 | og_electronixtz |
Ni wapi unaweza Kununua Friji za Boss
Friji za Boss zinapatikana katika maduka makubwa ya vifaa vya elektroniki kote Tanzania. Pia unaweza kuzinunua mtandaoni kupitia tovuti za maduka hayo au tovuti za biashara za mtandaoni.
Mambo ya Kuzingatia Unaponunua Friji ya Boss
Kabla ya kununua friji, zingatia mambo yafuatayo:
- Ukubwa na Uwezo – Hakikisha friji inakidhi mahitaji yako ya kuhifadhi vyakula.
- Matumizi ya Umeme – Chagua friji yenye teknolojia ya kuokoa umeme (Energy Saving).
- Aina ya Compressor – Friji zenye inverter compressors zinatumia umeme kidogo na ni tulivu.
- Dhamana na Huduma kwa Wateja – Angalia dhamana ya kifaa na upatikanaji wa vipuri.
- Bei na Bajeti – Chagua friji inayolingana na bajeti yako bila kuathiri ubora.