Mwanamke Kupendeza hakuishii kwenye Mavazi na kupaka make up mpaka aina ya Perume unayotumia inaweza kuwa sababu ya kukufanya uonekane mrembo zaidi au laa Hapa nimekuwekea Oodha ya Perume Bora za muda wote kwa Wanawake.
- Guerlain La Petite Robe Noir
Waswahili wenyewe wanasema mwamba huyu hapaaa. Nikizungumza hivyo nadhani naeleweka kabisa yaani. Huu ni unyunyu classic ambayo hutumiwa na kupendelewa sana na baadhi ya watu wazito. Perfume hii bwana iko na ladha ya matunda, berry na mimea.
- Milioni Lady, ya Paco Rabanne
Perfume nyingine ambayo hupendelewa na wanawake wengi kwakuwa na ladha ya harufu ya kumvuta mtu kwa jina linguine tusema ina harufu kali kidogo, ina ladha ya mchanganyiko wa asali na jimmy, kuna raspberry, hii ni jamii ya strawberry, pia iko ya machungwa nk.
- Afyuni, Yves Saint Laurent
Wale wapenzi wa udii udii mwamba huyu hapa, sio poa maana ina harufu nyingi kama vile karafuu, mdalasini ubani, oud, vanilla, peach nk. Wewe dada mrembo unayependa kunukia unyunyu wa oud basi hii itakufaa.
- Versace Bright Crystal
Walee wazee na ndoa zao wapenda kufusha manukato ya miski, hii hapa nyingine ni nzuri mno na ukipulizia ndani mpaka mtaa wa saba wanasikia, wale wapenzi wa miski wananielewa nini namaanisha yaani harufu yake haikeri.
Soma Hii :Biashara Ya Mtaji Wa Million 100 (100,000,000) Tanzania
- Nina Ricci
Haya ni manukato bwana ambayo yamekaa kidada zaidi maana hata muuondo wake nje uko kirembo zaidi licha ya kuwa na harufu nzuri na hata ladha ya harufu yake imetawaliwa na maua zaidi.
- D & G 3 L’Imperatrice
Unyunyu huu bwana unamfanya mwanamke kujiamini haswa anapokuwa mbele za watu maana hata ladha za harufu yake ni ya kipekee sana kama vile unyunyu wa tikiti maji, miski nk yaani ukijipulizia lazima harufu yako ionekane ya tofauti mbele za watu.
- Green, DKNY
Haya ni manukato ambayo muundo wake kwa nje ni kama apple na maji yake kwa ndani like green apple ndo maana ikaitwa jina hilo na harufu nzuri mno maana manufacture iliotumika kutengenezea ni lile tunda alilokula Eva apple yaani perfume hii ni balaa.
Mbali na kuwa na jina hilo la green likiwa na maana ya green apple pia katika kampuni hii kuna ladha za harufu mbalimbali kama vile tango, zaituni, rose nk.
- Armani Giorgio
Kuna baadhi wao hupendelea sana manukato ambayo yana harufu tofauti na mwingine, basi hili ndo suluhisho kwasababu Armani ina ladha ya harufu tofauti tofauti kama vile machungwa, limao, tangawizi nk, kama unahitaji harufu ya pekee yako basi nakushauri tumia hii kitu utakuja kunishukuru baadae.
- Givenchy Ange Ou Demon Le Secret
Wale wenzangu na mie wasiopenda harufu za karaha, tusiopenda mbambamba, unyunyu huu hapa wale wa lemon yenyewe wazee wa kupenda manukato ya maua basi hapa ndo kwisha kazi, uende kwengine ufuate nini. Hii nayo ni perfume ambayo hupendelewa sana kutumiwa na wanawake mbalimbali.
- Gucci Guilty
Uuuuwiiih! Wale wazee na vipenzi vya Gucci, sio unavaa nguo tu za kampuni hiyo halafu manukato yakushinde dada, nikuibie siri ya unyunyu huu bwana unakaa haswa kwenye nguo, kuna ladha za harufu tofauti tofauti kama vile chenza, limao, maua nk unakosaje kuitumia kwa mfano.
Perume nyingine Bora kwa Wanawake kwa Mujibu wa Tovuti ya Kaziforums
Jina la Manukato | Vidokezo Muhimu |
---|---|
Chanel No. 5 | Maua, Vanila |
Dior J’adore | Maua ya Mithili, Yasemini, Tuberose |
Gucci Bloom | Jasmine, Tuberose, Maua ya Mithili |
Yves Saint Laurent Black Opium | Kahawa, Yasemini, Vanila |
Marc Jacobs Daisy | Yasemini, Maua ya Mithili, Vanila |
Tom Ford Black Orchid | Maua ya Mithili, Vanila, Patchouli |
Chloe Chloe | Yasemini, Vanila, Maua ya Mithili |
Prada Candy | Vanila, Musk, Caramel |
Versace Bright Crystal | Yasemini, Maua ya Mithili, Vanila |
Lancome La Vie Est Belle | Vanila, Iris, Maua ya Mithili |
Guerlain Mon Guerlain | Lavender, Jasmine Sambac, Vanila, Sandalwood |
Carolina Herrera Good Girl | Almond, Tuberose, Kahawa, Vanila |
Maison Margiela Replica Beach Walk | Bergamot, Coconut Milk, Musk |
Jo Malone English Pear & Freesia | Pear, White Freesia, Patchouli |