Close Menu
swahiliforums.com
  • Home
  • Ajira Mpya
  • Elimu
  • Michezo
  • Makala
Facebook X (Twitter) Instagram
swahiliforums.com
BOFYA HAPA
  • Home
  • Ajira Mpya
  • Elimu
  • Michezo
  • Makala
Facebook X (Twitter) Instagram
swahiliforums.com
Home » Zijue Dawa Za Asili Za Fangasi Ukeni
Afya

Zijue Dawa Za Asili Za Fangasi Ukeni

BurhoneyBy BurhoneyMarch 10, 2025No Comments6 Mins Read
Share Facebook Twitter Telegram WhatsApp
Zijue Dawa Za Asili Za Fangasi Ukeni
Zijue Dawa Za Asili Za Fangasi Ukeni
Share
Facebook Twitter Telegram WhatsApp
WhatsApp Group Join Now
Telegram Group Join Now

Fangasi ukeni ni moja ya matatizo ya afya ya wanawake ambayo mara nyingi husababisha usumbufu mkubwa, ikiwa ni pamoja na muwasho, kutokwa na uchafu wenye harufu, na maumivu wakati wa kujamiiana. Ingawa kuna matibabu mengi ya kibiashara yanayotolewa kwa ajili ya fangasi ukeni, baadhi ya wanawake wanapendelea kutumia dawa za asili kutibu tatizo hili.

Fangasi Ukeni:

Fangasi ukeni ni muwasho sehemu ya ndani ya uke ambao unaweza kuambatana pia na kuvimba kwa uke. Maambukizi ya fangasi sehemu za siri imekuwa ni tatizo kubwa sana duniani, 75% ya wanawake wote duniani wanaosumbuliwa na tatizo hili wanatafuta dawa ya fangasi ukeni kila siku. Maambukizi haya ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa kwa kiasi kikubwa na fangasi aina ya candida albicans na maambukizi haya pia hujulikana kama vaginal yeast infection au vaginal thrush.

SOMA HII :Madhara ya kufanya mapenzi kipindi cha hedhi Kwa Wanaume Na Wanawake.

Chanzo Cha Fangasi Ukeni:

Chanzo cha fangasi ukeni ni fangasi wajulikanao kwa kitaalamu kama “candida albicans,” ambao kwa kawaida huishi kwenye sehemu za siri bila kusababisha madhara, lakini wanapoongezeka kupita kiasi, husababisha maambukizi hayo. Fangasi ukeni ni maambukizi ya kawaida sana kwa wanawake na yanaweza kumuathiri mwanamke wa umri wowote.

Mambo Yanayoongeza Hatari Ya Kupata Fangasi Ukeni:

Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayomuweka mwanamke katika hatari ya kupata fangasi ukeni;

  1. Ujauzito.
  2. Kushuka kwa kinga ya mwili kutokana na kuugua magonjwa mbalimbali kama vile kisukari, UKIMWI.
  3. Matumizi yaliyokithiri ya dawa hasa zile za kuua bakteria (antibiotics).
  4. Wanawake wenye umri wa miaka 20-30 wapo katika hatari ya kupata maambukizi haya wakati wale ambao wamekoma hedhi (menopause) na wale ambao hawajaanza kupata hedhi hawako katika hatari kutokana na mazingira au vitu wanavyotumia.
  5. Matumizi ya mara kwa mara ya vidonge vya majira (oral contraceptive pills).
  6. Msongo wa mawazo uliokithiri.
  7. Kujamiiana kwa njia ya kawaida mara tu baada ya kujamiiana kupitia haja kubwa (anal sex).
  8.  Matumizi ya vilainishi wakati wa kujamiiana husababisha maambukizi pia.
  9. Kuwa na historia ya kupata matibabu ya homoni (hormonal replacement therapy).
  10.  Kuwa na utapiamlo (malnutrition).
  11.  Kuvaa nguo za ndani zisizokauka vizuri na kuvaa mavazi yanayoleta sana joto sehemu za siri.
  12.  Matumizi makubwa ya mipira wakati wa ngono mfano condoms.
SOMA HII :  Dawa ya kutibu kilimi

Dalili Za Fangasi Ukeni:

Zifuatazo ni baadhi ya dalili za fangasi ukeni ambazo ni pamoja na;

  1. Kuwashwa sehemu za siri.
  2. Kuhisi maumivu makali  wakati wa kujamiiana.
  3. Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri mara baada ya kutoka kufanya tendo la ndoa au kutoka kukojoa (burning sensation).
  4. Kuvimba na kuwa  mwekundu katika mdomo wa nje ya uke (labia minora).
  5. Kupata vidonda ukeni (soreness).
  6. Kupata maumivu wakati wa kukojoa na kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au kijivu unaoweza kuwa mwepesi, mzito au majimaji.
  7. kutoa harufu mbaya ukeni.

Matibabu Ya Fangasi Ukeni:

1. JUISI YA MALIMAO (LEMONADE):
Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau, maji, asali na mdalasini ya unga kidogo. Kunywa robo lita (ml 250) kutwa mara 2 kwa siku 10 kwa mtu mzima na glasi ndogo moja kwa siku kwa mtoto wa miaka miwili mpaka kumi. Unaweza pia kuongeza majani kidogo ya mnanaa (mint) na mbegu za shamari (fennel seeds) ili kuongezea ladha na harufu nzuri. Kunywa juisi hii kila unapotoka kula chakula cha mchana au cha jioni.
2. MAZIWA MTINDI
Mtindi au bidhaa zitokanazo na maziwa ya mtindi ni tiba ya kuaminika ya fangasi wa ukeni. Pia inashauriwa kula tu huu mtindi kiasi cha kutosha kila siku.
3. KITUNGUU SWAUMU
Kitunguu swaumu kina sifa na uwezo wa kuua bakteria na hata virusi mwilini. Vikatekate (chop) vipande vidogo. Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine muhimu zilizomo kwenye mtindi.
4. MAFUTA YA NAZI
Kama fangasi hao wa ukeni wanajitokeza hadi sehemu kidogo ya nje ya uke na unapata muwasho pia, hakikisha unapakaa mafuta ya asili ya nazi yaliyotengenezwa nyumbani. Hii dawa tosha kwa fangasi wowote juu ya ngozi.
5. KUTUMIA FEMININE WASH
Hii huwa inafahamika kama mkombozi wa wanawake kwa maambukizi ya sehemu za siri.
Imeandaliwa maalum kwa ajili ya wanawake
Imetengenezwa kwa vyakula,mimea na madini na viua sumu mwilini.
Inamadini yanayohuisha uke na kuwa na ulinzi asilia,inaviua sumu vinavyozuia uke kuzeeka(mashavu),uke uliolegea, na kuondoa harufu mbaya ukeni.
Ina mafuta mazuri yanaitwa *essential oil* kwa ajili ya kufanya uke urudishe mnato wake wa asili.

Dawa Ya Fangasi Ukeni Ya Vidonge:

Klotrimazole (clotrimazole) ni dawa ya vidonge ya kuua fangasi ukeni (antifungal). Dawa hii ina majina mengi ya kibiashara ikiwemo Cruex, Desenex, Fungoid, Lotrimin, Mycelex, Clotrimazole,  Canesten, Clotrimaderm, Myclo, FungiCURE na Candistat. Hupatikana pia kama dawa ya vidonge vya kuweka ukeni (vaginal pessaries).

Jinsi Ya Kutumia Klotrimazole (Vaginal Pessaries) Kutibu Fangasi Ukeni;

Tumia dawa hii wakati unaenda kulala. Hakikisha mikono yako ipo safi, kisha lala chali, panua magoti ukiwa umeyainua. Ingiza dawa ukeni kwa kutumia kifaa chake maalum. Kama haina kifaa maalum, baada ya kuitoa kwenye gamba lake, ingiza kidonge hicho kwenye uke na kisha kisukumize kwa kidole cha kati mpaka kifike mwisho. Baada ya hapo nawa mikono yako. Tumia kwa muda uliolekezwa na daktari.

SOMA HII :  Magonjwa 40 yanayotibiwa na mwarobaini

Madhara Ya Fangasi Ukeni:

Madhara yafuatayo yanaweza kutokea ikiwa mgonjwa mwenye fangasi ukeni atashindwa kupata tiba mapema;

1. Mimba Kuharibika.

Hii hutokea kwa mama mjamzito ambaye hakupata tiba ya maambukizi ya fangasi ukeni mapema ambapo maambukizi hayo huenea sehemu mbalimbali za via vya uzazi na kuharibu mji wa mimba (uterus), sehemu ambapo mimba hujishikiza (fetal implantation) na kupelekea mimba kuharibika kabla ya wakati wake.

2. Kupata Homa Na Kizunguzungu.

Hali hii hutokea kwa sababu ya kubadilika kwa hali ya kawaida ya mwili na kuharibika kwa sehemu mbalimbali za mwili kutokana na maambukizi ya fangasi hali ambayo  husababisha kubadilika kwa joto la mwili pia.

3. Kuongezeka Kwa Miwasho Sehemu Za Siri.

Madhara ya fangasi ukeni husababisha kuwepo kwa miwasho kwenye sehemu za siri ambapo mwathirika hujikuna kila wakati, hali hii huongeza uwezekano mkubwa wa kuenea kwa ugonjwa wa fangasi ukeni kwa sababu mwenye maambukizi kama anajikuna na anawagusa wengine wanaomzunguka basi anaweza kusambaza maambukizi hayo kwa wanaomzunguka kwa urahisi.

4. Maumivu Makali Wakati Wa Kukojoa.

Hali hii hutokea kwa mgonjwa Mwenye tatizo la fangasi ukeni, pale ambapo maambukizi yameenea sehemu mbalimbali za via vya uzazi na kusababisha michubuko. Hivyo wakati wa haja ndogo, mgonjwa akikojoa na mkojo ukagusa sehemu ya michubuko maumivu makali hutokea na kusababisha  kukosa raha.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA:

Fangasi hii inaweza ikachelewa kupona au ikawa inajirudia hata baada ya kupona kwa sababu zifuatazo:
•Kutokunywa maji ya kutosha. (glasi nane kwa siku kwa mtu mzima).
•Matumizi ya vyakula vyenye wanga kwa sana.
•Matumizi ya sukari kwa sana/vitu vitamu.
•Matumizi ya vinywaji vya baridi, chai, kahawa.
•Matumizi ya pafyumu na kuweka vitu nani ya uke.
•Matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango. Ni vyema kutumia njia mbadala za kujikinga na mimba Kama njia ya kalenda.
•Kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

 

SOMA HII :  Dawa ya Kutokwa na Uchafu Sehemu za Siri: Sababu, Dalili na Matibabu

Follow on Telegram Follow on WhatsApp
Share. Facebook Twitter Email Telegram WhatsApp
Burhoney
  • Website

Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati

WhatsApp Group Join Now
Telegram Group Join Now

Related Posts

Jinsi ya kuacha kujichua kwa mwanamke

December 2, 2025

Kazi ya vipipi ukeni

December 2, 2025

Jinsi ya kutumia vipipi mahaba

December 2, 2025

Dalili za mimba ya mtoto wa kiume

December 2, 2025

Tabia ya mtoto wa kiume akiwa tumboni

December 2, 2025

Jinsi ya kutumia pipi kifua kwa mwanamke

December 2, 2025

Comments are closed.

Latest Posts

Zimamoto Recruitment Portal Login:Mfumo wa Maombi ya Ajira Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

December 13, 2025

Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Jeshi la Zima moto PDF Download December 2025

December 12, 2025

MAJINA Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs 2026

December 12, 2025

Orodha ya Majina walioitwa kwenye Usaili kada ya Afya na Ualimu Ajira portal December 2025

December 4, 2025

Mfumo wa Maombi ya Ajira kwa Kada za Afya na Elimu TAMISEMI

November 26, 2025
Load More

Subscribe to Updates

Usipitwe na Habari zetu za kila siku Kuwa wa kwanza kupata Habari zetu Kwa Kuandika Email yao Hapo chini

SwahiliForums Ni jukwaa la Habari na Makala mbalimbaali kwa Lugha kiswahili Habari za Michezo,Elimu, Biashara,Ajira Mpya na Dondoo za Afya Endelea kutufuatilia kwa kutembelea site yetu SwahiliForums.com

Karibu kwenye Swahiliforums, jukwaa lako la kipekee kwa habari, maarifa, na mijadala inayoangazia masuala ya kijamii, uchumi, na utamaduni kutoka kwa mtazamo wa Kiswahili. Hii ni blog ambayo inalenga kutoa taarifa za kina kuhusu matukio ya sasa, maisha ya kila siku, na masuala muhimu yanayoathiri jamii zetu katika eneo la Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla.

swahiliforums.com
Facebook X (Twitter) Instagram WhatsApp Telegram Pinterest
Copyrights reserved @2025 swahiliforum.com

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.