Hedhi ni kipindi cha asili katika mzunguko wa mwezi wa mwanamke ambapo damu hutoka kwenye mfuko wa uzazi kutokana na kutoshika mimba. Ingawa ni mchakato wa kimaumbile na wa kawaida kwa wanawake, bado kuna maswali mengi kuhusu athari za kufanya mapenzi wakati wa hedhi. Hapa, tutachunguza madhara yanayoweza kutokea kwa wanaume na wanawake wanapofanya mapenzi wakati wa hedhi,
Madhara Ya Kushiriki Tendo La ndoa Wakati Wa hedhi Kwa Wanaume Na Wanawake.
A) Madhara Kwa Wanawake:
Yafuatayo ni baadhi ya madhara yanayoweza kutokea kwa wanawake kutokana na kushiriki tendo la ndoa wakati wa hedhi ambayo ni pamoja na:
1) Maumivu Na Kutokwa Na Damu Nyingi Zaidi.
Wakati wa hedhi, baadhi ya wanawake wanaweza kuwa na maumivu zaidi ya tumbo (dysmenorrhea) na kutokwa na damu nyingi zaidi.
Kushiriki tendo la ndoa wakati huu kunaweza kuongeza maumivu na kusababisha kutokwa na damu nyingi zaidi.
2) Hatari Ya Kupata Maambukizi.
Kwa wanawake, kushiriki tendo la ndoa wakati wa hedhi kunaweza kuongeza hatari ya kupata maambukizi ya uke au njia ya mkojo kutokana na mlango wa uzazi (cervix) kuwa wazi zaidi kwa bakteria ikiwa wapenzi wao wana maambukizi. Mfano wa maambukizi hayo ni pamoja na Pelvic inflammatory Disease (PID), maambukizi ya zinaa (STIs) n.k
3) Saratani Ya Shingo Ya Kizazi.
Kushiriki tendo la ndoa wakati wa hedhi kunaweza kuongeza hatari ya kuambukizwa virusi vya HPV (Human Papilloma Virus), ambavyo vinasababisha saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.
4) Kuziba Kwa Mirija Ya Uzazi.
Kwa wanawake, kushiriki tendo la ndoa wakati wa hedhi kunaweza kuongeza hatari ya kuziba kwa mirija ya uzazi (fallopian tubes), hali ambayo inaweza kusababisha ugumba au matatizo ya uzazi.
5) Hatari Ya Kupata Ujauzito.
Ingawa ni nadra, kuna hatari ya kupata mimba wakati wa hedhi. Manii (sperms) inaweza kuishi kwa siku kadhaa (mpaka siku 5) ndani ya mwili wa mwanamke, na inawezekana kutokea ovulation (kutoa yai) mapema.
B) Madhara Kwa Wanaume:
Yafuatayo ni baadhi ya madhara yanayoweza kutokea kwa wanaume kutokana na kushiriki tendo la ndoa wakati wa hedhi ambayo ni pamoja na:
1) Hatari Ya Kupata Maambukizi.
Wanaume wanaweza kuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya zinaa wakati wa tendo la ndoa kipindi cha hedhi, ikiwa wapenzi wao wana hayo maambukizi.
2) Matatizo Ya Tezi Dume.
Kwa wanaume kushiriki tendo la ndoa wakati wa hedhi kunaongeza hatari ya damu ya hedhi kuingia kwenye tezi dume, hali ambayo inaweza kusababisha ugumba au matatizo ya tezi dume mfano prostatitis.
3) Athari Ya Kisaikolojia.
Baadhi ya wanaume wanaweza kuhisi wasiwasi au kutojisikia vizuri kushiriki tendo la ndoa wakati wa hedhi kutokana na kuvuja damu, harufu, au maumivu ambayo wapenzi wao wanaweza kuhisi.
4) Tatizo La Uume Kusimama Lege Lege.
Wakati wa tendo la ndoa kipindi cha hedhi, uchafu unaotoka ukeni ukiingia kwenye mishipa ya damu ya uume unaweza kupelekea tatizo la uume kusimama lege lege, hali ambayo hujulikana kwa kitaalamu kama erectile dysfunction.
Faida za Kufanya Tendo la Ndoa Kipindi cha Hedhi
- Kupungua kwa maumimu ya misuli ya tumbo na nyonga : Mwanamke anapofika kileleni kwa kutoshelezwa kimapenzi husaidia kupunguza maumivu kwenye nyonga na misuli. Kufika kileleni kunasaidia misuli kusinyaa na hivo kuondoa maumivu. Tendo la ndoa pia husaidia kutoa kichocheo na endorphims ambacho kinakufanya ujiskie vizuri.
- Kupunguza siku za hedhi Kufanya mapenzi kipindi cha hedhi kunaweza kusaidia kupunguza siku za kutokwa hedhi. Hii inawafaa zaidi wanaopata hedhi zaidi ya siku 4. Kutanuka kwa misuli ya kizazi kunasaidia kusukuma damu kwa wingi na haraka na hivo kufupisha siku za hedhi.
- Kuongezeka kwa hamu ya tendo Baadhi ya wanawake wanaokosa hamu ya tendo la ndoa wanaweza kutumia kipindi cha hedhi kufaidi tendo hili. Hii ni kutokana na kuongezeka kwa hamu ya kufanya mapenzi kwenye kipindi cha hedhi kutokana na mabadiliko ya homoni.
- Damu ya hedhi kama kilainishi Kipindi cha hedhi damu inayotoka inaweza kutumika kama kilainishi ili kupunguza maumivu.
- Kupunguza maumivu ya kichwa:Karibu nusu ya wanawake hupata maumivu ya kichwa kipindi cha hedhi. Kushiriki tendo kutakusaidia kupunguza maumivu haya.
Je Naweza Kupata Ujauzito Kufanya Mapenzi Kipindi cha Hedhi?
Inawezekana kabisa kushika ujauzito wakati wa hedhi. Kwahivo kama hujapanga kushika mimba kumbuka kutumia kondomu muda wote. Kila mwanamke ana mzunguko tofauti wa hedhi, na pia mpangilio unaweza kubadilika ushike mimba kwenye kipindi ambacho hukupangilia. Wanawake wenye mzunguko mfupi wa siku 22 wapo kwenye hatari zaidi ya kushika mimba kipindi cha hedhi. Kumbuka mbegu za mwanaume zinaweza kuishi ndani ya kizazi kwa siku 5 mpaka 7, kwaivo kama una mzunguko wa siku 22 na yai kutolewa baada ya hedhi, kuna uwezekano mimba ikatungwa.
Soma Hii :Jinsi ya kusafisha uke baada ya tendo la ndoa
Dondoo zingine Muhimu Unapofanya Mapenzi Kipindi cha Hedhi.
- Ongea na mpenzi wako jinsi unavojiskia unapofanya mapenzi kipindi hiki cha hedhi. Kuwa muwazi na mweleze kama hujiskii vizuri.
- Tumia taulo nyeusi au kitambaa cha pamba cheusi kutandika kwenye godoro ili kufyonza damu.
- Andaa kitambaa chenya maji au wipes pembeni ya kitanda ili kujisafisha baada ya kumaliza tendo
- Ongea na mpenzi wako kuvaa kondomu kabla ya tendo kupunguza hatari ya kupata maambukizi.
- Jaribu staili tofauti kufanya mapenzi ili kupata inayokufaa ambayo haisababishi maumivu.