JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

Uhamisho wa mtumishi wa umma ni mchakato muhimu unaohusisha mabadiliko ya mtumishi kutoka sehemu moja ya kazi kwenda sehemu nyingine ndani ya taasisi au idara ya serikali. Hii ni hatua inayoweza kuchukuliwa kwa sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuboresha utendaji, kuongeza ufanisi, au kujibu changamoto za kiutawala. Kupata kibali cha uhamisho ni mchakato unaohitaji kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa na serikali. Katika makala hii, tutajadili utaratibu na hatua za kufuata ili kupata kibali cha uhamisho kwa mtumishi wa umma.

Aina za Uhamisho kwa Watumishi Wa Umma

Kuna aina mbili za Uhamisho kwa Watumishi wa Umma nazo ni;

  1. Uhamisho wa Kuomba

Taratibu za Kuomba Nafasi:-

1. Mtumishi atapaswa kuomba nafasi ya uhamisho kwa kuwasilisha maombi yake ya uhamisho kwa Mkurugenzi wa Halmashauri au Mamlaka anayotaka kuhamia kupitia kwa Wasimamizi wake wa kazi katika kituo chake cha kazi alichopo na Mkurugenzi wake.

2. Wasimamizi wa mtumishi anayeomba uhamisho watapaswa kuhakikisha maombi ya mtumishi yanafika katika mamlaka husika yakiwa na maoni yao kuhusu maombi hayo na sio kuzuia maombi. Iwapo kutakuwa na sababu ya msingi ya kuzuia maombi mwajiri amjulishe mtumishi kwa kumrejesha katika miongozo iliyopo

3. Iwapo Mwombaji hataridhika na maoni /sababu za mwajiri /Msimamizi wa kazi kukataa maombi yake mwombaji atawasilisha maombi yake kwa Katibu Tawala wa Mkoa kwa ushauri na kama hataridhia maombi yatawasilishwa kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI yakiwa na vielelezo muhimu kuthibitisha maombi hayo kukataliwa na Mkurugenzi na kueleza sababu za yeye kuomba uhamisho huo.

4. Mkurugenzi/Msimamizi wa kazi atayeombwa nafasi ya kuhamia atapaswa kumjibu mtumishi kupitia kwa Mkurugenzi wake kwa barua akimweleza kupatikana kwa nafasi hiyo kumetokana na nini ikiwa ni pamoja na kutaja Check Namba za watumshi waliofariki au kuacha kazi.

5. Iwapo mtumishi wa umma ataomba uhamisho kwa sababu za kumfuata mume au mke, kujiandaa kustaafu baada ya kukaa miaka kumi nje ya mkoa anaotarajia kustaafia na kukaa katika kituo kimoja kwa zaidi ya miaka mitano anaweza kufikiriwa kugharamiwa gharama za uhamisho hata kama ataomba uhamisho mwenyewe.

6. Mtumishi anayeomba uhamisho atapaswa kuwasilisha maombi yake kwa Katibu Mkuu au Katibu Tawala Mkoa au Mkurugenzi akiambatanisha barua iliyomkubalia kuhamia katika kituo anachotaka kuhamia. Aidha ni muhimu amjulishe mwombaji iwapo atagharimiwa uhamisho au la kufuatia kupata nafasi hiyo

7. Angalizo: Hairuhusiwi Mtumishi yeyote kutumia mtu mwingine isipokuwa yeye mwenyewe au Mwajiri wake kwa njia ya posta au Mkono kuwasilisha maombi yake ya uhamisho. Inashauriwa kutumia njia ya EMS au regista kwa urahisi wa ufuatiliaji.Upatikanaji wa Majibu:-

8. Watumshi wote walioomba uhamisho watapata majibu yao kwa barua kupitia kwa waajiri wao na sio vinginevyo.

9. Aidha kwakuwa uhamisho huu ni wa wazi watumishi waliokubaliwa au kaukataliwa uhamisho watapata taarifa za awali kupitia Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI yaani www.pmoral.go.tz mapema mwezi Julai kwa maombi yatakayopokelewa kuanzia Januari hadi Juni na mapema mwezi Januari kwa maombi yatayopokelewa kuanzia mwezi Julai hadi Desemba kwa kuwa Ofisi yetu imejipanga kushughulikia masuala ya uhamisho mara mbili kwa mwaka ili kuepusha mwingiliano wa majukumu katika vituo vya kazi kwa mwaka.

10. Mtumishi atakayekuwa na malalamiko kuhusu maombi yake ya uhamisho anashauriwa kuelekeza maombi yake kwa Mamlaka iliyomwamisha kupitia kwa mwajiri wake na msimamizi wa kazi akiambatisha maombi yake ya awali na vilelezo vingine muhimu kama sababu za kuomba uhamisho na ushahidi wa kufikisha barua yake kwa Mamlaka ya uhamisho.

11. Malalamiko ya mtumishi aliyeomba uhamisho na hakupata majibu au hakuridhika na majibu aliyopatiwa malalamiko yake yatashughulikiwa ndani ya siku saba bila kujali muda wa uhamisho yaani June au Desemba.

12. Baada ya mtumshi kupata majibu /barua ya uhamisho atapaswa kuripoti ndani ya siku kumi na nne tangu amekabidhiwa barua yake ya uhamisho vinginevyo atachulikuliwa ni mtoro kazini.

2. Uhamisho wa Kawaida

Uhamisho huu ni wa kawaida ambapo Mwajiri au Msimaimizi wa kazi anafanya uhamisho kwa sababu za kuboresha utendaji.

Hata hivyo ili uhamisho huo ufanyike pia Mamlaka za uhamisho zinatakiwa kujiridhisha uwepo wa nafasi wazi katika Halmashauri anayohamishiwa mtumishi wa hakusababishi upungufu katika Sehemu mtumishi anakotoka au anakohamia.

Uhamisho huu kwa kawaida unagharamiwa na Halmashauri inayompokea mtumishi na ile inayomruhusu kwa kumlipa gharama za kufunga mizigo kama ilivyoelezwa kwenye Kanuni L (8 na 13) ya Utumishi wa Umma ya Kudumu toleo la 2009 na marekebisho yake ya mwaka 2010 kwa wakati. hivyo ni muhimu Mamlaka za Uhamisho kijiridhisha na uwezo wa Halmashauri kugharamia uhamisho huo ili kuepuka kuzalisha madeni kwa Serikali

Pamoja na utaratibu wa uhamisho kuwa ni uhamisho kufanyika mara mbili kwa mwaka, uhamisho huu wa kawaida unaweza kufanyika wakati wowote katika jitihada za kunusuru utendaji katika kituo alichopo mtumishi au anachohamishiwa mtumishi kwa manufaa ya umma.

Angalizo:

Mtumishi atakayebainika kughushi saini za viongozi, kuomba au kupokea rushwa katika ngazi yoyote atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kumfikishwa mbele ya vyombo vya dola kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Ni muhimu kwa Waajiri kujiridhisha na majibu ya barua za uhamisho kutoka katika Mamlaka za uhamisho ili kuona kama maombi yake yalifuata taratibu sahihi na watumishi waliopata majibu wanatayarishiwa mapema data sheet na kumbukumbu za utumishi na mshahara ili kuepusha usumbufu kwa watumishi na waajiri wanaowapokea watumshi.

Sababu zinazoweza kupelekea Uhamisho kwa Mtumishi wa Umma

  • Kumfuata Mwenza: Ikiwa mtumishi anaomba uhamisho ili kumfuata mwenza, anatakiwa kuwasilisha cheti cha ndoa kama uthibitisho.
  • Sababu za Kifamilia: Kama uhamisho unahitajika kwa sababu za kifamilia (kama vile kuwahudumia wazazi au ndugu wanaomtegemea), mtumishi anapaswa kuwa na barua kutoka kwa Mtendaji wa Kata, Kijiji, au Mtaa wa sehemu anakokwenda.
  • Sababu za Kiafya: Ikiwa mtumishi anahitaji kuhama kwa ajili ya matibabu, barua ya rufaa au ripoti kutoka kwa daktari wa hospitali ya serikali inapaswa kuambatanishwa. Barua hiyo inatakiwa kuonesha kuwa mtumishi anahitaji kupata matibabu katika hospitali iliyopo karibu na eneo analotaka kuhamia.
  • Kubadilishana Nafasi na Mtumishi Mwenzake: Kama mtumishi anabadilishana na mtumishi mwenzake, taarifa zote za mtumishi wanayebadilishana naye zinapaswa kuambatanishwa.

SOMA HII : Mfano na Muundo wa Barua ya Kazi ya Ualimu TAMISEMI

Jinsi ya Kupata Kibali cha Uhamisho kwa Mtumishi wa Umma

Mtumishi anapohitaji kibali cha Uhamisho kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa kwenda TAMISEMI anapaswa kuwa na vitu vifuatavyo:-

1. Barua ya kumuombea kibali iliyoandikwa na Mwajiri wake (Mkurugenzi)

2. Barua yake ya maombi ya uhamisho aliyotuma kule anakotaka kuhamia

3.Barua ya kukubaliwa maombi yake ya uhamisho kutoka kwa Mwajiri wa mahali anakotaka kuhamia

4. Barua yake ya ajira

5.Barua ya kuthibitishwa kazini

6.Nakala ya kitambulisho cha kazi

7. Nakala ya hati ya mshahara(Salary slip)

8. Kiambatisho cha sababu ya kuhama kwake ( kama ni kumfuata mwenza lazima awe na cheti cha ndoa, kama ni kwa sababu za kifamilia kwamfano kuwa karibu na wazazi au ndugu zake wanaomtegemea anapaswa kuwa na barua ya Mtendaji wa Kata/kijiji/Mtaa wa kule anakokwenda, kama ni ugonjwa barua ya Rufaa/au ya Daktari kutoka kwenye Hospitali ya Serikali inayoonesha kuwa mtumishi anahitaji kupata matibabu katika Hospitali ya mahali anakoomba kuhamia, ikiwa ni kubadilishana taarifa za mtumishi mwenzake wanayebadilishana naye ).

JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA
Share.

Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati

Leave A Reply