Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ni moja ya taasisi muhimu za kiusalama katika nchi yetu, likihusika na kulinda amani na utawala wa sheria. Kujiunga na JWTZ ni ndoto kwa vijana wengi wanaotamani kutumikia taifa lao kwa ufanisi na kujitolea. Hapa, tutazungumzia baadhi ya sifa muhimu zinazohitajika kwa mtu anayetaka kujiunga na Jeshi la Wananchi Tanzania.
Majukumu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilianzishwa tarehe 01 Septemba 1964 likiwa na lengo la kulinda uhuru wa nchi na mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Majukumu Mengine ya JWTZ
Kulinda Katiba na Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ulinzi wa Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kufanya Mafunzo na Mazoezi ili kujiweka tayari Kivita wakati wote.
Kufundisha umma shughuli za Ulinzi wa Taifa.
Kushirikiana na Mamlaka za Kiraia katika kutoa misaada ya kibinadamu na uokoaji wakati wa maafa.
Kukuza elimu ya kujitegemea na uzalishaji kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Kushiriki katika shughuli za Ulinzi wa Amani Kimataifa.
Vijana wengi wamekuwa wakitamani kujiunga na JWTZ lakini hawajua njia sahihi wanazotakiwa kupitia ili kuweza kutimiza ndoto zao ambapo hali hiyo inapelekea kuwapo kwa matapeli wengi. Matapeli hao hutumia kigezo cha watu kutokujua namna ya kujiunga na JWTZ kuweza kuwatapeli wakisema kuwa wanaweza kuwasaidia.
Sifa Unazotakiwa Kuwa Nazo Kuweza Kujiunga na Jeshi la Tanzania
Katika chapisho hili tunaenda kukueleza juu ya sifa na vigezo vinavyohitajika ili kujiunga na Jeshi la wananchi Tanznia JWTZ, pia utaenda kusoma juu ya mahitaji ya msingi unayotakiwa kua nayo katika mchakato wa kujiunga na jeshi la wananchi Tanzania JWTZ.
Tulio wengi tunapotaka kujiunga na jeshi tunatambua vigezo vya jumla kama vile
- Kuokua na michoro ya aina yoyote ile mwilini (Tatoo)
- Kuwa na tabia iliyo Njema
- Kutokua na historia ya kiharifu
Vigezo vya Kujiunga na Jeshi la JWTZ Tanzania
Kama unahitaji kujiunga na jeshi la JWTZ basi hivi hapa chini ni vigezo na sifa za wazi zitakazo kufanya uweze kuchaguliwa kujiunga na jeshi hilo la JWTZ bila kua na shaka yoyote ile
1. Usiwae na ulemavu wa aina yoyote
2. Uwe na afya iliyo bora yenye kukuwezesha kufanya kazi ya aina yoyote ile na yenye nguvu
3. Uwe na umri chini ya miaka 35
4. Elimu kuanzia darasa la saba
5. Uwezo wa kimwili kuhimili hali yoyote ya hewa na mazingira
6. Usiwe na Michoro ya aina yoyote mwilini
Inatakiwa mombaji wa nafasi ya kujiunga na jeshi la JWTZ afahamu kua ili kujiunga na tawi lolote lile la jeshi hilo basi ni lazima ale kiapo ambacho kitamfanya akili kulitumikia jeshi hilo wakati wote, mahali popote na katika mazingira yoyote hata kuiacha familia na vile vyote uvipendavyo na kuitii sheria.
Unaweza ukawa unavigezo na sifa zote zinazokufanya uweze kujiunga na jeshi la JWTZ bado itakuhitaji uwe na uaminifu na utii wa kutosha, kujitolea kwa moyo wote usahau maisha binafsi na uwe tayari kuitumikia sheria na kuacha mambo yoako yote binafsi.
SOMA HII: Mfano na Muundo wa Barua ya Maombi ya Kazi Kujiunga Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)
Zifuatazo ni sifa za kujiunga na Jeshi Tanzania JWTZ
Sifa hizi ndizo hutumika katika upokeaji wa maombi ya kazi za jeshi pale zinapotangazwa.
- Uwe Raia Wa Tanzania
- Awe na umri kati ya miaka 17-25.
- Uwe na elimu ya kuanzia KIdato cha 4 na kuendelea
- Usiwe na ndoa
- Usiwe na rekodi yoyote ya kiharifu
- Uwe na faya njema kimwili na kiakili