Airtel Wamewarahisishia maisha na kuwathamini Wateja wao kwa kuwaletea simu za mkopo ushirikiano na JUMO kwa Walokidhi Vigezo na Masharti na kuwaruhusu kulipa kidogo kidogo.
Simu Mpya ya Itel A80
Kampuni ya Airtel na Itel wamezindua simu ya Itel A80 kwa wateja wa Tanzania. Simu hii ina sifa za kisasa kama:
- Skrini ya 6.7 inch yenye punch-hole
- Betri ya 5000mAh inayodumu kwa muda mrefu
- Kamera ya 13MP (nyuma) na 8MP (mbele)
- Nafasi ya kuhifadhi data ya 128GB + 8GB RAM
- 4G kwa kasi ya mtandao.
Soma Hii :Makato ya NBC bank kwa mwezi
Bei na Mikopo:
Wateja wanaweza kununua simu hii kwa Tsh 265,000/= kwa fedha taslimu au kwa mkopo kwa kianzio cha Tsh 55,000/=. Kwa kila malipo ya siku (Tsh 1,200), wateja wanapokea MB 250 bure kwa miezi sita.
Jinsi ya Kupata Simu za Mkopo Airtel
Mchakato wa Maombi
- Piga *150*60# na fuata maelekezo kwenye menyu ya Airtel Timiza.
- Thibitisha taarifa zako (jina, nambari ya simu, akaunti ya Airtel Money).
- Chagua kiasi cha mkopo na muda wa malipo (siku, wiki, mwezi, au miezi sita).
Malipo na Marejesho
- Malipo ya kiotomatiki: Kiasi hukatwa moja kwa moja kutoka kwa akaunti ya Airtel Money kwenye tarehe ya mwisho.
- Ada ya kuchelewa: 10% ya kiasi kilichosalia ikiwa hulipwa kwa wakati.