Chuo cha Mipango Dodoma fahamu sifa za Kujiunga na kozi zinaotolewa katika chuo cha IRDP Dodoma ,Ni muhimu kufahamu sifa na kozi kabla ya kutuma maombi ya kujiunga na chuo Makala hii imekuorodheshea vigezo vyote unavyopaswa kuwa navyo ili kujiunga chuo cha mipango ya maendeleo vijijini
Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Mipango Dodoma
Sifa za Kujiunga Programu za Shahada za Kwanza (Bachelor’s Degree Programs)
Chuo cha Mipango Dodoma kinatoa programu kadhaa za shahada ya kwanza ambazo zinaangazia maeneo tofauti ya mipango na maendeleo. Ili kujiunga na mojawapo ya programu hizi, mwanafunzi anatakiwa kuwa na sifa maalum kulingana na kozi anayokusudia kusoma. Hapa chini ni baadhi ya programu zinazotolewa na sifa zinazohitajika:
- Shahada ya Mipango ya Fedha na Uwekezaji (Bachelor Degree in Development Finance and Investment Planning)
- Sifa: Ufaulu wa D mbili katika masomo ya Uchumi, Jiografia, Historia, Biashara, Uhasibu, Hisabati ya Juu, Lishe, Kilimo, Baiolojia, Kiingereza, Fasihi, Fizikia, au Kemia.
- Alama za chini za kujiunga: 4.0
- Muda wa masomo: Miaka 3
- Shahada ya Mipango na Usimamizi wa Mazingira (Bachelor Degree in Environmental Planning and Management)
- Sifa: Ufaulu wa D mbili katika masomo kama Uchumi, Jiografia, Historia, Biashara, Uhasibu, Hisabati ya Juu, Lishe, Kilimo, Baiolojia, Kiingereza, Fizikia, au Kemia.
- Alama za chini za kujiunga: 4.0
- Muda wa masomo: Miaka 3
- Shahada ya Mipango ya Idadi ya Watu na Maendeleo (Bachelor Degree in Population and Development Planning)
- Sifa: Ufaulu wa D mbili katika masomo ya Uchumi, Jiografia, Historia, Biashara, Uhasibu, Hisabati ya Juu, Kiswahili, Lishe, Kilimo, Baiolojia, Kiingereza, Fasihi, Fizikia, au Kemia.
- Alama za chini za kujiunga: 4.0
- Muda wa masomo: Miaka 3
- Shahada ya Mipango ya Maendeleo ya Mikoa (Bachelor Degree in Regional Development Planning)
- Sifa: Ufaulu wa D mbili katika masomo ya Uchumi, Jiografia, Historia, Biashara, Uhasibu, Hisabati ya Juu, Kiswahili, Lishe, Kifaransa, Kilimo, Baiolojia, Kiingereza, Fasihi, Fizikia, au Kemia.
- Alama za chini za kujiunga: 4.0
- Muda wa masomo: Miaka 3
- Shahada ya Mipango na Usimamizi wa Rasilimali Watu (Bachelor Degree in Human Resource Planning and Management)
- Sifa: Ufaulu wa D mbili katika masomo ya Uchumi, Jiografia, Historia, Biashara, Uhasibu, Hisabati ya Juu, Kiswahili, Lishe, Kilimo, Baiolojia, Kiingereza, Fasihi, Fizikia, au Kemia.
- Alama za chini za kujiunga: 4.0
- Muda wa masomo: Miaka 3