Tuzo za Tanzania Comedy Awards 2024/2025 zimefanyika kwa mafanikio makubwa, na kutambua michango ya wasanii na vichekesho bora vilivyowachaguliwa kwa mwaka huu. Hizi ni tuzo muhimu katika tasnia ya vichekesho nchini Tanzania, zinazolenga kutambua na kuenzi vipaji vya wasanii, waandishi wa vichekesho, na waandaaji wa vipindi vinavyowafanya watu wacheke na kufurahi.
Katika hafla hii, washindi kutoka katika makundi mbalimbali walitunukiwa kwa mafanikio yao, huku wakionesha umahiri na ubunifu mkubwa. Orodha kamili ya washindi wa tuzo hizi inatoa picha wazi ya ustawi wa tasnia ya vichekesho nchini na jinsi gani imetoa mchango mkubwa katika burudani na jamii.
Orodha Kamili ya Washindi wa tuzo za Tanzania Comedy Awards 2024/2025
- Champion Of Comedy – Rais Samia Suluhu Hassan.
- Hall Of Fame – King Majuto.
- Tuzo ya heshima – Coy Mzungu.
- Best Comedian Actor Of The Year – Joti.
- Best Comedy Special Award – Jol Master.
- Best Male Comedian Of The Year – Nanga.
- Best Comedian Of The Year People’s Choice – Leonardo.
- Best Female Comedian Of The Year – Asma.
- Best Male Stand Up Comedian Of The Year – Eliud samwel.
- Best Female Stand Up Comedia Of The Year – Neila.
- Best Funny Leader Of The Year – Makongoro Nyerere.
- Legend People’s Choice – Joti.
- Best Comedy Tv Show – Kitimtim.
- Best Kid Comedian – Dogo Sele.
- The award for Tanzania’s Comedian Leader – Makongoro Nyerere.
- Aliyemchekesha zaidi Rais Sami- Said Said.