Kwa mashabiki wa soka, kutazama mechi moja kwa moja ni jambo la msingi. Siku hizi, simu janja zimeleta urahisi mkubwa kwa kuwa unaweza kufuatilia mechi zako pendwa popote ulipo. Kuna apps mbalimbali zinazokuwezesha kuangalia mpira bure moja kwa moja (live streaming) bila malipo. Katika makala hii, tutakutambulisha apps bora ambazo unaweza kutumia kwa ajili ya kutazama mpira bure kwenye simu yako.
Mahitaji ya Kuweza Kutizama Mpira Live Kupitia Simu Yako
Ili uweze kutizama mpira live kupitia simu yako lazima uwe na vitu vifuatavyo;
- Simu janja (Smart Phone)
- Uwezo wa kuunganisha na Internet
- Internet yenye kasi nzuri
- App inayorusha matangazo ya Mpira live
1. Live Football TV
Sifa kuu:
- Hutoa mechi za moja kwa moja kutoka ligi mbalimbali kama EPL, La Liga, Serie A, Bundesliga, na Ligi ya Mabingwa.
- Ina ratiba za mechi na taarifa za hivi karibuni kuhusu mpira.
- Ubora mzuri wa picha na sauti.
Jinsi ya Kupakua:
- Inapatikana kwenye Google Play Store kwa watumiaji wa Android.
2. Mobdro (APK Download)
Sifa kuu:
- Inatoa chaneli za moja kwa moja zenye vipindi vya michezo kutoka kote duniani.
- Inahifadhi mechi ili uweze kuzitazama baadaye.
- Haipatikani kwenye Play Store, lakini unaweza kuipakua kutoka tovuti mbalimbali.
Jinsi ya Kupakua:
- Pakua kutoka kwa tovuti za APK zinazotegemewa kisha usakinishe (install manually).
3. Yacine TV
Sifa kuu:
- Maarufu kwa mechi za Ligi Kuu ya England, Ligi ya Mabingwa, na La Liga.
- Inatoa chaneli za michezo kwa ubora wa HD.
- Haina matangazo mengi ya kibiashara.
Jinsi ya Kupakua:
- Inapatikana kupitia tovuti rasmi ya Yacine TV.
4. Hesgoal (Website na App)
Sifa kuu:
- Inajulikana kwa matangazo ya mechi za moja kwa moja bure.
- Ina huduma ya live chat kwa mashabiki kujadili mechi.
- Hupatikana pia kama tovuti kwa wale wasiopenda kusakinisha app.
Jinsi ya Kupakua:
- Pakua kutoka kwa tovuti rasmi au utumie moja kwa moja kwenye browser.
Soma Hii : Jinsi Ya Kuangalia Channels Za Azam tv Bure
5. Football Live TV Streaming
Sifa kuu:
- Inatoa mechi za live streaming kutoka ligi tofauti.
- Inaruhusu kutazama highlights kwa wale waliokosa mechi moja kwa moja.
- Inatumika kwa Android na iOS.
Jinsi ya Kupakua:
- Pakua kutoka Google Play Store au App Store.
6. Live NetTV
Sifa kuu:
- Inatoa chaneli nyingi za michezo, ikiwa ni pamoja na Sky Sports, BT Sport, ESPN, na beIN Sports.
- Ina sehemu ya kutazama mechi zilizopita (replay feature).
- Inatumika kwa simu za Android.
Jinsi ya Kupakua:
- Pakua APK kutoka tovuti rasmi ya Live NetTV.
7. StarTimes ON
Sifa kuu:
- Inatoa mechi za moja kwa moja hasa kwa ligi za Afrika.
- Inaruhusu kutazama mechi bure kwa muda fulani.
- Ina toleo la kulipia kwa wale wanaotaka mechi zote.
Jinsi ya Kupakua:
- Inapatikana kwenye Google Play Store na App Store.