Kwa Wahitimu wa ngazi mbalimbali za Elimu ya yuo ambavyo vipo chini ya Nacte sasa wanaweza Kupata Hati zao za matokeo (Results Academic Transcript) kwa Njia ya Mtandao Tumekuwekea Utaratibu na Hatua za kfuata ili kujipatia Academic Transcrit yako kutoka NACTVET.
Nani Anaweza Kuomba Hati ya Matokeo ya NACTE?
- Sayansi ya Afya na Sayansi Shirikishi: Ikiwa ulisoma katika kozi zinazohusu afya au sayansi shirikishi, unastahili.
- Elimu ya Awali, Msingi, na Sekondari: Walimu wa ngazi hizi za elimu pia wanahusika.
- Mifugo: Wahitimu wa kozi kama Uzalishaji wa Afya ya Wanyama na Teknolojia ya Maabara ya Mifugo ni sehemu ya walengwa.
Muda gani Napaswa kuomba Hati ya Matokeo?
Ni muhimu kujua wakati sahihi wa kufanya “transcript request”. Baada ya matokeo yako ya mwisho kuthibitishwa na NACTE, unaweza kuendelea na maombi yako. Hakikisha umetimiza vigezo vyote vya kuhitimu na vikiidhinishwa kabla ya kutumia mfumo wa mtandaoni.
Jinsi ya Kuomba Hati ya Matokeo ya NACTE kwa Njia ya Mtandao
Ili kuomba hati yako ya matokeo mtandaoni, fuata hatua hizi:
- Tembelea Tovuti Rasmi ya NACTE: Anza kwa kufungua tovuti ya NACTE. Tafuta sehemu ya ” Key Links”
- Chagua Chaguo la Request Academic Transcript au “Request NACTE Transcript“: Ukishapata ukurasa wa maombi, bofya chaguo linalohusika.
- Tengeneza akaunti yako kwa Jaza Taarifa Binafsi na za Kitaaluma
- Chagua Mahali pa Kuchukua Hati ya Matokeo: Unaweza kuchagua kati ya Makao Makuu au ofisi za kanda.
- Tengeneza namba ya malipo na fuata taratibu za malipo zilizotolewa kupitia njia mbali mbali kama M-Pesa.
Malipo ya Maombi na Njia za Kulipa
- TSh 10,000: Kwa kuchukua hati Makao Makuu.
- TSh 15,000: Katika ofisi za kanda.
Malipo yanaweza kufanywa kupitia njia kama M-Pesa, Tigo Pesa, na Airtel Money. Hakikisha unafuata maelekezo kwa usahihi ili kuepuka matatizo ya malipo.
Nyaraka Muhimu na Mahitaji ya Maombi
Ili maombi yako yawe kamili, hakikisha una nyaraka zifuatazo:
- Picha ya Pasipoti: Inayokuwa na mandharinyuma ya rangi nyeupe au bluu ya anga.
- Kitambulisho Halali: Leseni ya udereva, kitambulisho cha taifa, au kadi ya mpiga kura.
Ufuatiliaji wa Maombi na Mawasiliano
Baada ya kufanya maombi yako, unaweza kufuatilia kupitia wasifu wako wa mtumiaji au kutumia barua pepe. Ikiwa unahitaji msaada zaidi, wasiliana na NACTE kupitia:
- Barua pepe: examinations@nacte.go.tz
- Simu: +255 677 004 202
Changamoto zilizopo katika utaratibu huu ni kama ifuatavvyo;
1. Gharama za kusafiri hadi kwenye ofisi za kanda kwa ajili ya kufatilia transcript
2 Changamoto ya mtandao endapo mtu akikosea wakati wa kutuma ombi la transcript inalazimika kufunga safari hadi ofisini kwao ili kufatilia na njoo kesho ni nyingi sana
3. Mfumo una changamoto ya kuleta taarifa za mtu aliesoma kozi zaidi ya moja, unaleta taarifa za kozi ya mwisho kuisoma au unayoisoma kwa wakati huo lakini ukihitaji transcript za kozi ulizosoma huko nyuma lazima usafiri adi ofisin kwao na mara nyingi tatizo hili hutatuliwa makao makuu tu.