Fahamu Jinsi ya Kuingia katika Account yako ya Heslb SIPA Kwa wanafunzi waliojisaili tayari kwa Ajili ya Kuomba Mikopo ya Elimu ya Juu kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa waiomaliza kidato cha sita (Form six) au kwa Waliotoka Diploma.
SIPA HESLB Ninini?
SIPA (Student’s Individual Permanent Account) ni sehemu muhimu ya mfumo wa OLAMS (Online Loan Application and Management System) wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB). Mfumo huu unawawezesha wanafunzi kusimamia mikopo yao kuanzia hatua za maombi hadi urejeshaji.
Akaunti ya HESLB inakupa uwezo wa:
- Kufanya ufuatiliaji wa Hali ya Maombi: Unaweza kuona kama maombi yako yamepokelewa, yanashughulikiwa, au yameidhinishwa.
- Kuangalia Mgao wa Mkopo: Baada ya maombi kuidhinishwa, unaweza kuona kiasi cha mkopo kilichotengwa kwako na ratiba ya malipo.
- Kusimamia Marejesho ya Mkopo: Kwa wanafunzi waliomaliza masomo na kuanza kurejesha mikopo yao, akaunti hii inawawezesha kuona salio la deni, ratiba ya malipo, na historia ya malipo yaliyofanyika.
- Kusasisha Taarifa Binafsi: Unaweza kubadilisha au kusasisha taarifa zako binafsi kama vile anwani, namba ya simu, na barua pepe ili kuhakikisha mawasiliano sahihi kati yako na HESLB.
Hatua Jinsi ya Kuingia kwenye Akaunti ya HESLB Akaunti baada ya kusajiliwa (HESLB Login as Registered User)
elea na masomo (HESLB Login as continuous)
Continuous Student
Maandalizi:
- Hakikisha una nenosiri lililosasishwa na namba yako ya udahili (admission number).
Hatua za Kuingia:
- Nenda kwenye Tovuti ya HESLB:
- Fungua kivinjari chako na tembelea http://olas.heslb.go.tz/olams/pre-applicant.
- Chagua Sehemu ya Wanafunzi Wanaoendelea au Loan Beneficiaries:
- Katika menyu ya tovuti, tafuta na ubofye sehemu inayohusiana na wanafunzi wanaoendelea (“Loan Beneficiaries “).
- Weka Taarifa za Kuingia:
- Ingiza namba yako ya udahili na nenosiri kwenye sehemu zinazohitajika.
- Bonyeza “Login”:
- Baada ya kuhakikisha taarifa zako ni sahihi, bonyeza kitufe cha “Login” ili kufikia akaunti yako na kupata huduma zinazotolewa.
Soma Hii :Jinsi ya kujiunga mfumo wa ESS PEPMIS – UTUMISHI
Jinsi ya Kuingia kwenye Akaunti ya HESLB kwa mwanafunzi anayesubiria kupata mkopo (SIPA HESLB Login Account)
Maandalizi:
- Hakikisha una taarifa za usajili za kudumu kama namba ya mtihani wa kidato cha nne na nenosiri.
Hatua za Kuingia:
- Tembelea Sehemu ya SIPA kwenye Tovuti ya HESLB:
- Fungua tovuti ya HESLB na ubofye sehemu ya Login For Registered Applicants au tembelea moja kwa moja http://olas.heslb.go.tz/olams/account/login
- Ingiza Maelezo Yanayohitajika:
- Weka namba yako ya mtihani wa kidato cha nne (mfano: S0143.0078.1990) na nenosiri ulilounda wakati wa usajili.
- Thibitisha Maelezo Yako na Uingie kwenye Akaunti:
- Baada ya kuhakikisha taarifa zako ni sahihi, bonyeza kitufe cha “Login” ili kufikia akaunti yako ya SIPA.
MASWALI NA MAJIBU YA UTOAJI MIKOPO
- Swali: Zipi ni sifa kuu za kupata mkopo wa elimu ya juu?
Jibu:
- Awe mtanzania
- Awe ameomba mkopo kwa utaratibu ulioelekezwa (online)
- Awe amepata udahili (admission) kwenye chuo kinachotambuliwa na jina lake kuwasilishwa Bodi ya Mikopo
- Asiwe na chanzo kingine cha kugharamia masomo yake ya chuo kikuu (mfadhili, ZHELB n.k)
- Maelezo ya kina kuhusu sifa na vigezo hutolewa na Mwongozo
- Swali:Ninapaswa kufanya nini ili niweze kuanza kuomba mkopo kwa njia ya mtandao (OLAMS)?
Jibu: Soma mwongozo unaotolewa na Bodi ambao unapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz), kisha, fungua mtandao wa maombi (www.olas.heslb.go.tz) ili ujisajili kwa kutumia namba yako ya mtihani wa kidato cha nne na mwaka uliofanya mtihani huo.
- Swali: Baada ya kujisajili, napaswa kufanya nini?
Jibu: Baada ya kujisajili, utapata namba ya kumbukumbu (Control Number) kwenye ‘screen’ ambayo itakuwezesha kufanya malipo ya ada ya maombi ya TZS 30,000/= kwa njia ya benki au simu. Lipa mara moja tu! Kiasi kamili cha TZS 30,000/=
Baada ya kulipa, utapokea ujumbe (sms) wa uthibitisho wa muamala wako utakaokuwezesha kuendelea na hatua inayofuata ya maombi. Jaza hatua kwa hatua.
- Swali: Ni nyaraka gani muhimu zinatakiwa wakati wa kuomba mkopo?
- Nakala za:
- Cheti cha kuzaliwa cha mwombaji kilichothibitishwa na RITA
- Vyeti vya kidato cha IV & VI au Stashahada (Diploma)
- Cheti cha kifo ikiwa umepoteza mzazi kilichothibitishwa na RITA;
- Kitambulisho cha mdhamini (NIDA, Mpiga Kura; Leseni ya Udereva au Pasi ya Kusafiria). Mdhamini anaweza kutumia kimoja kati ya vitambulisho hivi.
- Barua ya taasisi mfadhili (Sponsor) ikiwa ulifadhiliwa katika masomo ya sekondari
- Barua ya Mganga Mkuu wa Wilaya au Mkoa ikiwa mwombaji au mzazi wake ana ulemavu
- Picha (passport size) za mwombaji wa mkopo na mdhamini wake
(mdhamini anaweza kuwa mzazi au mlezi)
- Swali: Je, iwapo nimehitimu kidato cha sita au diploma wa mwaka huu
wa masomo na sijapata cheti, nitaambatanisha nini?
Jibu: Unatakiwa kujaza namba ya mtihani wa kidato cha sita ambayo itaweza kuhakikiwa na mamlaka husika. Kwa mhitimu wa diploma (Stashahada), unaweza kuambatanisha waraka wa matokeo (transcript).
- Swali: Je, mwanafunzi anaweza kupata usaidizi wa kuomba mkopo
kwenye ‘Internet Café’?
jibu:
- Swali: Je, nikijaza namba yangu ya mtihani isiyokuwa ya NECTA, kwa
mfano ya nje ya nchi, nitawezaje kuendelea kuomba mkopo?
Jibu: Wakati wa kujisajili, unatakiwa kuchagua kipengele cha ‘Non-NECTA students’ na kujaza kama inavyoelekezwa. Mfumo utakupatia namba ya kidato cha nne tofauti na ile uliyojaza ambayo itatambuliwa na mfumo wa Bodi. Namba hii mpya itatokana na taarifa yako ya namba uliyojazwa awali (isiyokuwa ya NECTA).
- Inachukua muda gani fomu kufunguka baada ya kulipa?
Jibu: Fomu inafunguka mara tu malipo yanapokamilika. Fomu inapochelewa kidogo kufunguka, mwombaji unashauriwa kutoka (Sign out) na kujaribu kuingia tena (Sign in) katika mtandao ili aweze kuendelea na hatua zinazofuata.
- Swali: Ikiwa nimelipa lakini sijapokea ujumbe wa kuendelea na maombi nifanyeje?
Jibu: Unatarajiwa kupokea ujumbe mara tu muamala unapokamilika. Ikiwa hautapata ujumbe ndani ya saa moja (dakika 60) baada ya kufanya malipo, unashauriwa kuwasiliana nasi kwa namba ya simu +255 22 550 7910 au 0736 665 533 au barua pepe info@heslb.go.tz
- Swali: Nitafanyaje ikiwa njia mojawapo ya kulipia mfano, CRDB,
NMB,TPB, M-pesa, Airtel Money, Tigo-Pesa, T-Pesa itanigomea kulipa na kuendelea?
Jibu: Kwa kuwa kuna njia zaidi ya moja ya kulipia, unashauriwa kutumia njia ya malipo ambayo ni rahisi kwako au inapatikana sehemu uliyopo wakati ukifanya malipo.
- Swali:Nifanyeje iwapo nimesahau neno langu la siri (Password)?
Jibu: Utapaswa kubofya kiunganishi cha “Forgotten the Password?” na kisha utapata neno jipya la siri hapo hapo (kwenye screen) mtandaoni.
- Swali: Je, ni wapi nitahakiki cheti za kuzaliwa au kifo cha mzazi?
Jibu: Vyeti vya kuzaliwa na vya vifo vya wazazi lazima vihakikiwe na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kabla havijapakiwa (uploaded) kwenye mtandao (olams)
- Swali: Je kuna athari zozote ikiwa nimeambatanisha na kuwasilisha cheti ambacho hakijahakikiwa na RITA?
Jibu: Ndiyo. Maombi yako yatakuwa hayajakamilika na hivyo kutofikiriwa katika hatua ya upangaji mikopo.
Unapaswa kuhakikisha nyaraka zote (siyo vyeti vya vifo au kuzaliwa tu) zinathibitishwa na mamlaka, taasisi au maafisa waliotajwa katika mwongozo.
- Swali: Kama simfahamu mzazi wangu, nitajaza nini?
Jibu: Unatakiwa kujaza taarifa za mlezi au mtu mwingine anayekulea au kusimamia masuala yako ya Elimu. Ni lazima taarifa za mlezi au msimamizi zithibitishwe na Serikali ya Mtaa unakoishi. Kama mlezi anazo nyaraka rasmi za kukuasili (adoption document) nazo ziambatanishwe.
- Swali: Iwapo niliwahi kupata mkopo zamani na nikaacha, kushindwa au kufukuzwa chuo, nitaweza kupata mkopo mwingine?
Jibu: Iwapo uliwahi kuwa mnufaika wa mkopo wa fedha za Serikali, utapaswa kwanza kurejesha mkopo wote au angalau asilimia 25 ya deni lako kabla ya kufikiriwa kupata mkopo mwingine. Deni unalopaswa kulipa utalipata kwenye mtandao (screen) na utatakiwa kulipa kwanza kabla ya kuendelea na maombi ya mkopo mpya.
- Swali: Kama nina wazazi wasio na uwezo, je niwasilishe
uthibitisho w aina gani ili kupata mkopo?
Jibu: Mwombaji ambaye ana mahitaji maalum, ni lazima mahitaji na hali yake ithibitishwe na mamlaka husika kama Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) au taasisi za aina hiyo. Taarifa za aina hii zitapekuliwa kuthibitishwa uhalisia na ukweli wake.
- Swali: Kama nilikosa mkopo mwaka jana, nikalazimka kuahirisha
masomo, natakiwa kuomba tena mkopo mwaka huu?
Jibu: Unaruhusiwa kuomba upya mkopo mwaka huu. Maombi yako yatapimwa kwa mwongozo na vigezo vya mwaka huu wa masomo. Unashauriwa usome mwongozo kwa makini na kuuzingatia.
Aidha, kama unasoma mwaka wa pili au wa tatu na kuendelea na una uhitaji wa mkopo, unaruhusiwa kuomba kwa kuzingatia vigezo vya mwaka huu.
- Swali: Nitafanyaje nisipoweza kumfikia mtoa huduma kwa njia ya
Simu zinazoonyeshwa kwenye mtandao?
Jibu: Kuna njia mbili za kuwafikia watoa huduma wa kitengo cha usaidizi (Helpdesk) Njia ya kwanza ni kwa simu +255 22 550 7910 au 0736 665 533 na nyingine ni kwa barua pepe info@heslb.go.tz.
Unashauriwa kuwasilisha taarifa au changamoto husika kwa njia ya barua pepe ili wataalamu waifanyie kazi na kukupigia simu kama itahitajika. Kumbuka kuandika mawasiliano yako ya simu itakayotumika kukupig
- Swali: Je, nitajuaje kama nimejaza fomu ya maombi kwa ukamilifu?
- Picha ya mwombaji na picha ya mdhamini wako;
- Vivuli vya nakala za vyeti vya kitaaluma zilizothibitishwa na Wakili au Mahakama;
- Vivuli vya nakala za vyeti vya kuzaliwa au kifo zilizothibitishwa na RITA;
- Nakala za barua za ufadhili kutoka katika taasisi zinazotambulika;
- Nakala ya kitambulisho cha mdhamini kilichothibitishwa na Wakili au Mahakama;
- Nakala ya fomu ya maombi iliyosainiwa na kugongwa muhuri na Serikali ya Mtaa, Mahakama au Wakili kama inavyoelekezwa;
- Aidha, nakala halisi ya fomu ya maombi inapaswa kusainiwa na mwombaji na mdhamini wake
- Maelezo ya kina yanapatikana katika mwongozo uliopo kwenye tovuti ya Bodi ya Mikopo (www.heslb.go.tz)
- Swali: Fomu za maombi ya Mikopo zinawasilishwaje Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu?
Jibu: Baada ya kuzi-upload na kukamilisha kujaza fomu ya maombi, mwombaji a-print fomu iliyokamilika na kuituma kwa EMS kwenda kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
Barabara ya Sam Nujoma – Mwenge
S.L.P. 76068
14113 DAR ES SALAAM
- Swali: Mwombaji atajuaje iwapo amepata mkopo?
Jibu: Baada ya Bodi kupokea, kuhakiki na kuchambua maombi ya mikopo, majina ya Wanafunzi watakaofanikiwa kupangiwa mikopo yatatangazwa kupitia tovuti ya Bodi ya Mikopo (www.heslb.go.tz) kabla ya kufunguliwa kwa vyuo vya elimu ya juu walikodahiliwa Wanafunzi husika.
- Swali: Mkopo unatolewa kwenye vipengele (Loanable Items) vipi?
Jibu:
- Chakula na malazi
- Ada ya mafunzo
- Vitabu na viandikwa
- Mahitaji maalumu ya kitivo
- Utafiti
Mafunzo kwa vitendo