Mwanamke ni kiumbe wa hisia nyingi na moyo wa huruma, lakini pia ana moyo unaoumizwa kwa urahisi na maneno. Tofauti na maumivu ya kimwili yanayoonekana, maumivu ya moyo yanayochochewa na maneno huweza kubaki moyoni kwa muda mrefu sana. Kila neno lina uzito, na linaweza kuwa upanga unaochoma hisia zake bila hata kugusa mwili wake.
SEHEMU YA 1: AINA YA MANENO YANAYOMUUMIZA MWANAMKE
1. Kubeza Muonekano au Mwili Wake
“Mbona umekuwa na makunyanzi hivi?”
“Huna mvuto hata kidogo.”
“Wengine wana shepu kuliko wewe.”
Mwanamke anataka kujisikia mrembo machoni pa yule anayempenda. Kubeza mwonekano wake humvunja kabisa.
2. Kulinganisha na Mwanamke Mwingine
“Mama fulani anajua kupika zaidi yako.”
“Ex wangu alikuwa na akili kuliko wewe.”
Hakuna mwanamke anayependa kulinganishwa. Kulinganisha hujenga hofu, chuki na kujiuliza “Je, simtoshi?”
3. Kutishia Kuondoka au Kuachana
“Ninaweza kupata mwanamke bora kuliko wewe.”
“Nikiwa serious, nakuacha tu sasa hivi.”
Hii ni njia ya kuvunja moyo na kuharibu msingi wa uaminifu. Maneno haya huacha makovu ya kihisia.
4. Kudharau Mchango Wake katika Maisha Yako
“Wewe hunisaidii chochote.”
“Ningeendelea vizuri hata bila wewe.”
Mwanamke hujitahidi kila siku kuhakikisha mpenzi wake anajisikia vizuri. Maneno kama haya huumiza sana.
5. Kumfokea Hadharani au Kumpa Aibu
“We ni mpumbavu!”
“Nyamaza bibi, huelewi kitu!”
Hakuna mwanamke anayependa kudhalilishwa mbele ya watu. Hii huondoa heshima kabisa na kupunguza thamani yake.
6. Kubeza Hisia Zake
“Hayo ni mambo madogo tu, si ya kulia.”
“Unaleta drama tu.”
Mwanamke anapojaribu kuzungumza, ni kwa sababu anajali. Ukimpuuza, unamfanya ahisi hajaliwi.
SEHEMU YA 2: KWANINI WANAUME HUSEMA MANENO YA KUUMIZA?
Kukosa uvumilivu wa kihisia
Kutojua thamani ya mawasiliano mazuri
Kureact kwa hasira bila kufikiria
Kujaribu kuwa na mamlaka katika uhusiano
Kutokuwa tayari katika mahusiano ya kihisia
Sababu yoyote ile, haistahili kuwa sababu ya kuumiza moyo wa mwanamke.
SEHEMU YA 3: ATHARI ZA MANENO HAYA KWA MWANAMKE
Hupoteza kujiamini
Huhisi hafai wala kupendwa
Huacha kupenda kwa moyo wote
Hujifunga kihisia na kujilinda
Huathirika hata katika mahusiano yajayo
Ukweli mchungu: Mwanamke anaweza kupenda kwa moyo wote, lakini akiumizwa sana, huwa mgumu kurudi kama mwanzo.
SEHEMU YA 4: NIFANYEJE KAMA NILISHAWAHI KUMUUMIZA?
Kubali kosa kwa uwazi:
“Najua nilisema maneno ya kuumiza. Nimeyatambua na najutia.”
Omba msamaha wa kweli, si wa kulazimisha:
“Samahani mpenzi, nakuomba unisamehe. Si kwa sababu nataka turudi tu vizuri, bali kwa sababu najua nilikukosea.”
Onyesha kwa vitendo kwamba umejifunza:
Badili namna unavyoongea, jifunze kusikiliza na heshimu hisia zake kila wakati.