Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) ni taasisi ya elimu ya juu inayoongoza Zanzibar, ikitoa programu mbalimbali za shahada ya awali na za juu katika nyanja tofauti kama sayansi, elimu, afya, sanaa, na biashara. Baada ya mchakato wa udahili kukamilika, wanafunzi wengi hutaka kujua kama wamechaguliwa kujiunga na SUZA kwa mwaka wa masomo husika.
Majina ya Waliochaguliwa Chuo Kikuu Cha Zanzibar SUZA
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimechapisha rasmi orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo kwa mwaka wa masomo 2025. Wanafunzi waliopata nafasi za masomo wanapaswa kuchukua hatua kadhaa ili kuhakikisha wanakamilisha taratibu zote zinazohitajika ili waweze kujiunga rasmi na chuo cha SUZA 2025:
Soma Hii :Majina Waliochaguliwa Kujiunga Chuo Cha Maji Water Institute – WI 2025 /2026
Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Chuo Kikuu Zanzibar SUZA
Kwa mwaka wa masomo wa 2025, wanafunzi waliomba kujiunga na programu mbalimbali zinazotolewa na chuo kikuu ucha Zanzibar (SUZA). Majina ya waliochaguliwa tayari yamewekwa wazi, na wanafunzi wanaweza kuyapata kupitia njia mbalimbali:
Jinsi ya Kuangalia Walochaguliwa Online
1. Tembelea Tovuti Rasmi ya SUZA
Tovuti rasmi ya Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) ni chanzo cha kwanza cha kupata orodha ya wanafunzi waliochaguliwa. Unaweza kutembelea tovuti kwa kufuata kiungo hiki: www.suza.ac.tz.
2. Nenda Sehemu ya ‘Announcements’ au ‘Latest News’
Katika ukurasa wa mwanzo wa tovuti ya SUZA, tafuta sehemu ya Matangazo, Habari Mpya, au Announcements. Hii ni sehemu ambapo SUZA huchapisha taarifa zote muhimu, ikiwa ni pamoja na majina ya wanafunzi waliopata udahili.
3. Tafuta Tangazo la Majina ya Waliochaguliwa
Baada ya kufungua sehemu ya matangazo, tafuta tangazo linalosema “Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na SUZA kwa Mwaka wa Masomo 202X/202X.” Mara nyingi, tangazo hili linakuwa na faili ya PDF yenye majina ya wanafunzi waliochaguliwa.
4. Pakua na Fungua Orodha ya Majina
Baada ya kupata tangazo, bonyeza kiungo cha faili ya PDF ili kuipakua kwenye simu au kompyuta yako. Fungua faili na utafute jina lako kwa kutumia kipengele cha search (Ctrl + F kwa kompyuta au kipengele cha kutafuta kwa simu).
Kuangalia Majina Kupitia Ujumbe Mfupi wa Simu (SMS)
SUZA inatumia mfumo wa ujumbe mfupi (SMS) kuarifu wanafunzi waliochaguliwa. Ujumbe huu utatuma kwenye namba ya simu iliyotumika wakati wa kuomba kujiunga na chuo.
Kuthibitisha Udahili Chuo Kikuu Cha Zanzibar SUZA
Wanafunzi waliochaguliwa na ambao wamepata udahili kwenye vyuo zaidi ya kimoja wanapaswa kuthibitisha udahili wao kwa kuchagua chuo kimojawapo. Kuthibitisha huku kunafanywa kwa kutumia namba ya siri (confirmation code) iliyotumwa kwa njia ya ujumbe mfupi kupitia namba za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili.
Wale ambao hawajapokea ujumbe huo wanaweza kuingia kwenye akaunti zao walizotumia wakati wa kuomba udahili na kuomba namba ya siri upya kupitia sehemu iliyoandikwa “request confirmation code”. Ni muhimu kuhakikisha kwamba uthibitisho huu unafanyika kabla ya tarehe 21 Septemba 2025.
Kupakua Barua ya Udahili Ya Chuo Kikuu Cha Zanzibar SUZA
Baada ya kuthibitisha udahili, wanafunzi wanapaswa kupakua barua za udahili (admission letters) kutoka kwenye akaunti zao. Barua hizi zina maelezo muhimu kuhusu ratiba ya kujiunga na chuo, michango ya ada, na maelekezo mengine ya kujiandaa kwa masomo.
Nafasi za Udahili Awamu ya Pili Katika Chuo Kikuu Cha Zanzibar SUZA
Kwa wale ambao hawakupata nafasi katika awamu ya kwanza ya udahili, SUZA inatoa fursa ya pili ya kuomba udahili katika programu mbalimbali ambazo bado zina nafasi. Awamu ya pili ya udahili imeanza rasmi tarehe 3 Septemba 2024 na itafungwa tarehe 21 Septemba 2024. Wanafunzi wanashauriwa kuchukua fursa hii kwa kutuma maombi yao haraka ili kujiunga na kozi ambazo zinaendana na sifa zao.