Je ni Kozi gani nikisoma nitapata mkopo wa Heslb ni swali ambalo wanafunzi wengi hujiuliza ,Makala hii imeorodhesha programu ambazo zinazopewa kipaumbele kwenye kupata mkopo kwa mujibu wa Heslb.
Kozi Zenye Kipaumbele Kupata Mkopo HESLB kwa Ngazi ya Degree
1. Sayansi ya Afya
Hii inajumuisha kozi kama Udaktari, Uuguzi, Ufamasia, na Maabara ya Kitabibu. Kozi hizi ni muhimu katika kuboresha sekta ya afya nchini.
2. Uhandisi
Kozi za uhandisi kama vile Uhandisi wa Umeme, Uhandisi wa Ujenzi, na Uhandisi wa Kompyuta zina umuhimu mkubwa katika kukuza miundombinu na teknolojia nchini.
3. Kilimo
Tanzania ikiwa nchi ya kilimo, kozi za Sayansi ya Kilimo, Ufugaji, na Usindikaji wa Vyakula zimepewa kipaumbele.
4. Sayansi ya Kompyuta na TEHAMA
Kozi zinazohusiana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ni muhimu katika zama hizi za dijitali.
5. Ualimu wa Sayansi na Hisabati
Kuna uhitaji mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi na hisabati katika shule za sekondari.
6. Utalii na Ukarimu
Kwa kuwa sekta ya utalii ni muhimu kwa uchumi wa Tanzania, kozi zinazohusiana na usimamizi wa hoteli na utalii zimepewa kipaumbele.
7. Usimamizi wa Rasilimali za Maji
Kozi zinazohusiana na usimamizi wa rasilimali za maji ni muhimu kwa maendeleo endelevu ya nchi.
8. Sayansi ya Mazingira
Kozi zinazoshughulikia masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi zimepewa umuhimu mkubwa.
Kozi Zenye Kipaumbele Kupata Mkopo HESLB kwa Ngazi ya Shahada (Diploma)
Katika mwaka wa masomo 2025 mikopo itatolewa kwa wanafunzi
waliodahiliwa katika Program/Stashahada zinazoangukia/zilizomo katika maeneo
sita ya kipaumbele yaliyoidhinishwa.
Afya na Sayansi Shirikishi (Health & Allied Sciences)
Programu katika kundi hili ni kama zifuatazo:-
(i) ‘Clinical Dentistry’;
(ii) ‘Diagnostic Radiotherapy’;
(iii) ‘Occupational Therapy’;
(iv) ‘Physiotherapy’;
(v) ‘Clinical optometry’;
(vi) ‘Dental Laboratory technology’;
(vii) ‘Orthotics & Prosthetics’;
(viii) ‘Health record & information’;na
(ix) ‘Electrical and Biomedical Engineering’.
Elimu ya Ualimu (Education and Teaching)
Programu katika kundi hili ni kama zifutazo:-
(i) Stashahada za msingi za Ualimu: Stashahada ya Ualimu wa Sayansi
katika masomo ya Fizikia, Kemia na Hisabati; na
(ii) Stashahada za Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TE&VET).
SOMA HII :Hatua kwa Hatua Jinsi Ya Kuomba Mkopo Wa Elimu Ya Juu HESLB
Usafiri na usafirishaji (‘Transport and Logistics’)
Programu katika kundi hili ni kama zifuatazo:-
(i) ‘Aircraft Mechanics’;
(ii) ‘Ship building and repair’;
(iii) ‘Railway construction and maintenance’; na
(iv) ‘Global Logistics and Supply Chain Management.
Uhandisi wa nishati (‘Energy Engineering’)
Programu katika kundi hili ni kama zifuatazo:-
(i) ‘Renewable Energy Engineering (Hydro, Wind, Solar)’; na
(ii) ‘Pipeline, Oil and Gas Engineering’.
Madini na sayansi ya sayari (‘Mining and Earth Science’)
Programu katika kundi hili ni kama zifuatazo:-
(i) ‘Lapidary and Jewelry’; na
(ii) ‘Mineral Processing’.
Kilimo na Ufugaji (‘Agriculture and Livestock’)
Programu katika kundi hili ni kama zifuatazo:-
(i) ‘Leather Technology’;
(ii) ‘Food Technology and Human Nutrition’;
(iii) ‘Sugar Production Technology’;
(iv) ‘Veterinary Laboratory Technology’;
(v) ‘Horticulture’;
(vi) ‘Irrigation Engineering’; na
(vii) ‘Agro Mechanization’.