Close Menu
swahiliforums.com
  • Home
  • Ajira Mpya
  • Elimu
  • Michezo
  • Makala
Facebook X (Twitter) Instagram
swahiliforums.com
BOFYA HAPA
  • Home
  • Ajira Mpya
  • Elimu
  • Michezo
  • Makala
Facebook X (Twitter) Instagram
swahiliforums.com
Home » Vigezo vya Kupata Mkopo Ngazi ya Diploma /Stashahada 2025/2026
Elimu

Vigezo vya Kupata Mkopo Ngazi ya Diploma /Stashahada 2025/2026

MWONGOZO WA UTOAJI MIKOPO KWA WANAFUNZI WA STASHAHADA
BurhoneyBy BurhoneyMarch 3, 2025No Comments4 Mins Read
Share Facebook Twitter Telegram WhatsApp
Vigezo vya Kupata Mkopo Ngazi ya Diploma /Stashahada 2025/2026
Vigezo vya Kupata Mkopo Ngazi ya Diploma /Stashahada 2025/2026
Share
Facebook Twitter Telegram WhatsApp
WhatsApp Group Join Now
Telegram Group Join Now

Serikali ya Tanzania kupitia bodi ya mikopo Heslb Walitangaza kuanza kutoa mikopo ya Elimu kwa wanafunzi wa ngazi ya Stashahada au Diploma Waliokidhi vigezo vya kupokea Mkopo huo ,Tumekuandalia makala hii kuorodhesha vigezo na Masharti ya kupata mkopo kwa ngazi ya stashahada.

Vigezo vya Kupata Mkopo Ngazi ya Diploma

Sheria na Kanuni za Bodi ya Mikopo zinaainisha sifa na vigezo vya jumla kwa
wanafunzi wanaohitaji mkopo baada ya kudahiliwa na vyuo vyenye ithibati. Mwombaji
atatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

  1. Awe Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 27 wakati wa kuomba mkopo;
  2. Awe amedahiliwa katika taasisi ya elimu inayotoa elimu ya ngazi ya kati nchini;
  3. Awe amekamilisha na kuwasilisha maombi ya mkopo kupitia mfumo wa maombi ya mkopo (OLAMS);
  4. Asiwe na ajira au mkataba wa kazi serikalini au sekta binafsi unaompatia mshahara au kipato;
  5. Awe amehitimu elimu ya Kidato cha Nne (CSEE), Cheti (astashahada) au Kidato cha Sita (ACSEE) ndani ya miaka mitano; yaani kati ya mwaka 2020 hadi 2024.
  6. Kwa mwanafunzi anayeendelea na masomo ahakikishe matokeo yake yanayomwezesha kuendelea na masomo yametumwa Bodi, kupitia Afisa Mikopo/uongozi wa Chuo.

Hali ya Kijamii na Kiuchumi

  1. Uyatima; aliyefiwa na mzazi au wazazi
  2. Familia au kaya ya kipato duni inayofadhiliwa na Mifuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) au taasisi nyingine za kitaifa zinazotoa ufadhili kwa kaya zenye vipato duni;
  3. Ulemavu wa mwombaji au wazazi wake

Nyaraka Za Kuambatisha Wakati Wa Maombi Ya Mkopo

Zifuatazo ni nyaraka muhimu za kuambatisha kwenye maombi ya mkopo: –

  1. Cheti cha kuzaliwa kutoka mamlaka husika, ZCSRA kwa waombaji kutoka Zanzibar au Namba ya Uhakiki (verification number) kutoka RITA kwa waombaji kutoka Tanzania Bara;
  2. Vyeti vya vifo vya wazazi kuthibitisha uyatima kutoka mamlaka husika, ZCSRA kwa waombaji waliozaliwa Zanzibar au Namba ya Uhakiki (verification number) kutoka RITA kwa waombaji waliozaliwa Tanzania Bara;
  3. Barua kutoka RITA au ZCSRA kuthibitisha taarifa za kuzaliwa kwa waombaji waliozaliwa nje ya nchi. Kwa mwombaji ambaye mzazi wake amefariki nje ya nchi anapaswa kuwasilisha barua kutoka RITA au ZCSRA kuthibitisha taarifa za kifo.
  4. Fomu ya Kuthibitisha Ulemavu wa mwombaji au mzazi wake iliyoidhinishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) au Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO);
  5. Namba ya kaya ya Mnufaika kutoka kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuthibitisha ufadhili wa kiuchumi alioupata mwombaji wakati wa elimu yake ya sekondari.
SOMA HII :  Chuo cha Ualimu Sumbawanga Teachers College courses offered na Sifa za Kujiunga

SOMA HII :Hatua kwa Hatua Jinsi Ya Kuomba Mkopo Wa Elimu Ya Juu HESLB

Jinsi Ya Kutuma Maombi Ya Mkopo Ngazi Ya Diploma

Mchakato wa kuomba mkopo wa HESLB kwa ngazi ya diploma ni rahisi na unafanyika mtandaoni. Hapa kuna hatua za kufuata:

  1. Maombi Mtandaoni: Maombi yote ya mkopo yatafanyika kupitia Mfumo wa Maombi na Usimamizi wa Mikopo (OLAMS). Waombaji wote wa mikopo wanakumbushwa kutumia namba ile ile ya Mtihani wa Kidato cha Nne iliyotumika wakati wa udahili.
  2. Ujazaji wa Fomu: Baada ya kuingia kwenye mfumo, jaza fomu ya maombi kwa usahihi na ukamilifu. Hakikisha unaambatanisha nyaraka zote zinazohitajika kama zilivyoainishwa katika mwongozo huu.
  3. Upakuaji na Saini: Baada ya kukamilisha maombi mtandaoni, pakua fomu za maombi na mikataba ya mkopo. Gonga mihuri sehemu husika, saini fomu, na ambatanisha nyaraka zinazohitajika.
  4. Uwasilishaji wa Fomu: Wasilisha kurasa zilizosainiwa (nambari 2 na 5) kwenye fomu ya maombi katika OLAMS.
  5. Malipo ya Ada ya Maombi: Lipia ada ya maombi ya mkopo ya shilingi elfu thelathini (TZS. 30,000.00) kwa namba ya kumbukumbu ya malipo utakayoipata katika mfumo. Unaweza kulipia kupitia benki au kwa mitandao ya simu.

UPANGAJI WA MIKOPO

Upangaji wa mikopo utazingatia vipaumbele vifuatavyo:-
(i) Mwanafunzi mwenye udahili kwenye programu za vipaumbele vya Taifa kama
zilivyofafanuliwa katika Kipengele cha 6 cha Mwongozo huu zitazingatiwa;
(ii) Ufaulu wa kitaaluma uliomuwezesha kudahiliwa kwa ajili ya elimu ya ngazi ya kati;
na
(iii) Hali ya kijamii kama ilivyofafanuliwa katika kipengele cha 3.2 cha mwongozo huu.

Follow on Telegram Follow on WhatsApp
Share. Facebook Twitter Email Telegram WhatsApp
Burhoney
  • Website

Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati

WhatsApp Group Join Now
Telegram Group Join Now

Related Posts

Majina ya waliochaguliwa kujiunga na veta 2026 pdf download

November 14, 2025

Orodha ya Vyuo ya Ualimu Vilivyopo Visiwani Zanzibar (Unguja na Pemba) — Ngazi ya Cheti na Diploma

November 14, 2025

Orodha ya Vyuo ya Ualimu Vilivyopo Mkoa wa Tanga (Ngazi ya Cheti na Diploma)

November 14, 2025

Orodha ya Vyuo ya Ualimu Vilivyopo Mkoa wa Tabora (Ngazi ya Cheti na Diploma)

November 14, 2025

Orodha ya Vyuo ya Ualimu Vilivyopo Mkoa wa Songwe (Ngazi ya Cheti na Diploma)

November 14, 2025

Orodha ya Vyuo ya Ualimu Vilivyopo Mkoa wa Singida (Ngazi ya Cheti na Diploma)

November 14, 2025

Comments are closed.

Latest Posts

Majina ya Walioitwa Kwenye Mafunzo Kusimamia Uchaguzi October 2025 :INEC Tume ya Taifa ya Uchaguzi

October 19, 2025

Majina ya Walioitwa kwenye Usaili kusimamia uchaguzi 2025 – INEC Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

October 12, 2025

Nafasi 70 Za Kazi Unitrans Tanzania Limited Madereva wa Malori 2025

September 17, 2025

Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wilaya ya Karatu 2025

September 13, 2025

Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo 2025

September 13, 2025
Load More

Subscribe to Updates

Usipitwe na Habari zetu za kila siku Kuwa wa kwanza kupata Habari zetu Kwa Kuandika Email yao Hapo chini

SwahiliForums Ni jukwaa la Habari na Makala mbalimbaali kwa Lugha kiswahili Habari za Michezo,Elimu, Biashara,Ajira Mpya na Dondoo za Afya Endelea kutufuatilia kwa kutembelea site yetu SwahiliForums.com

Karibu kwenye Swahiliforums, jukwaa lako la kipekee kwa habari, maarifa, na mijadala inayoangazia masuala ya kijamii, uchumi, na utamaduni kutoka kwa mtazamo wa Kiswahili. Hii ni blog ambayo inalenga kutoa taarifa za kina kuhusu matukio ya sasa, maisha ya kila siku, na masuala muhimu yanayoathiri jamii zetu katika eneo la Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla.

swahiliforums.com
Facebook X (Twitter) Instagram WhatsApp Telegram Pinterest
Copyrights reserved @2025 swahiliforum.com

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.