Watu wengi Vijana kwa wazee wanautiwa kujiunga na Chama cha mapinduzi kwa Malengo mbalimbali ikiwemo kuweza kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama na katia serikali kwa Ujumla Hapa tumekuwekea Hatua za Jinsi ya kupata adi ya chama cha mapinduzi (ccm).
Sifa za Kuwa Mwanachama wa CCM
Ili kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi, ni muhimu kufikia vigezo vifuatavyo:
Kuwa Mtanzania mwenye umri wa angalau miaka 18.
Kukubaliana na Itikadi, Katiba, Kanuni na Malengo ya CCM.
Kuwa tayari kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za chama katika eneo lako.
Kujaza fomu ya uanachama na kutoa taarifa sahihi kuhusu jina lako, makazi, namba ya simu, nk.
Kulipia ada ya uanachama inayowekwa na chama husika (kawaida ni kati ya TZS 2,000 – 3,000).
Kukubali kuwa mtiifu kwa viongozi wa chama na kuheshimu taratibu zake.
Sifa za Kugombea Uongozi Katika Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Kama unalenga kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya CCM, unatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
Uwe mwanachama halali wa CCM mwenye kadi ya chama.
Uwe na uzoefu wa kushiriki katika shughuli za chama angalau kwa kipindi fulani (kawaida ni si chini ya miaka 5 kwa nafasi za juu).
Uwe na tabia njema na mwenendo unaoendana na maadili ya CCM.
Uwe na elimu inayohitajika kwa nafasi husika (kulingana na ngazi ya nafasi).
Uwe hujawahi kushitakiwa au kuhukumiwa kwa kosa la jinai au ubadhirifu.
Kujaza fomu ya kugombea na kulipia ada ya kugombea kama itakavyotangazwa na chama.
Jinsi ya Kupata Kadi ya CCM
Kupata kadi ya CCM ni mchakato rahisi unaohusisha hatua chache muhimu:
1. Tembelea Ofisi ya CCM ya Kata au Tawi
Nenda kwenye ofisi ya CCM iliyo karibu nawe.
Omba fomu ya kujiunga na chama.
2. Jaza Fomu ya Uanachama
Jaza taarifa zako binafsi kama:
Jina kamili
Tarehe ya kuzaliwa
Anuani
Namba ya simu
Elimu na kazi
Weka sahihi yako na picha (ikiwa inahitajika).
3. Lipia Ada ya Uanachama
Ada ya kupata kadi ni nafuu, kawaida ni kati ya TZS 2,000 – 3,000.
Malipo yanaweza kufanyika ofisini au kwa njia ya simu kwa kutumia control number ya serikali (malipo ya serikali mtandao).(Jinsi ya kulipia kadi ya ccm kwa simu)
4. Subiri Kadi Yako
Baada ya malipo na uchakataji wa maombi yako, utapewa kadi ya chama ikiwa ni ushahidi wa uanachama wako.
Baadhi ya maeneo huweza kutoa kadi ya muda hadi ile ya kudumu itakapopatikana.
5. Jiunge na Tawi lako
Mwanachama hutakiwa kujiunga na tawi la CCM katika eneo analoishi ili kushiriki kikamilifu kwenye vikao, shughuli na maamuzi ya chama.