*LITANIA KWA MTAKATIFU RITHA WA KASHIA*
———————————–
Bwana Utuhurumie,
Kristo Utuhurumie,
Bwana Utuhurumie,
———————————–
*Kiitikio *”Utuhurumie”*
Baba wa Mbinguni, Mungu,
Mwana Mkombozi wa Dunia,Mungu,
Roho Mtakatifu, Mungu,
Utatu Mtakatifu, Mungu Mmoja,
———————————–
*Kiitikio* “Utuombee”*
Maria Imakulata Mama wa Mungu
Maria, Mama mfariji wa wanaoteseka
Maria, Malkia wa Watakatifu wote
Maria, Mwombezi mpenzi wa Mt Rita
———————————–
*Kiitikio* “Utuombee”*
Mt Rita, Zawadi toka Mbinguni:
Mt Rita, Mwombezi wetu mwenye nguvu:
Mt Rita, uliyejaliwa Utukufu:
Mt Rita, mstaajabiwa tangu utoto wako:
Mt Rita, mpenda upweke:
Mt Rita, Kielelezo cha usafi wa moyo:
Mt Rita, kielelezo cha upole wote:
Mt Rita, kielelezo cha mke mwema:
Mt Rita, kielelezo bora cha mama mtaratibu:
Mt Rita, kielelezo cha msamaha wa kweli:
Mt Rita, kielelezo hai cha kujikatalia:
Mt Rita, kioo cha maisha ya kitawa:
Mt Rita, kioo cha utii;
Mt Rita, mvumilivu wa kustajabiwa;
Mt Rita, shujaa wa kujitoa sadaka;
Mt Rita, shahidi katika kufanya toba
Mt Rita, mjane mtakatifu;
Mt Rita, mkarimu kwa masikini;
Mt Rita, mkarimu kwa masikini;
Mt Rita, mkereketwa wa kuitikia wito mtakatifu;
Mt Rita, aliyeingizwa utawani kimuujiza;
Mt Rita, harufu nzuri ya manemane;
Mt Rita, bustani ya kila fadhila;
Mt Rita, mpendezwa na Yesu Msulubiwa;
Mt Rita, uliyechomwa na mwiba kwenye paji la uso;
Mt Rita, binti mpendevu wa Bikira Maria;
Mt Rita, mwenye kiu ya upendo wa Kimungu;
Mt Rita, uliyevikwa utukufu;
Mt Rita, lulu ya mbinguni;
Mt Rita, utukufu wa shirika la Mt Augustino;
Mt Rita, tunu ya thamani ya Umbria;
Mt Rita, mwenye nguvu za utakatifu;
Mt Rita, msamaha wa wanaopata mahangaiko;
Mt Rita, mfariji wa wanaoteseka;
Mt Rita, nanga ya wokovu;
Mt Rita, mwombezi wa wagonjwa;
Mt Rita, mwombezi wa mambo yaliyoshindikana;
Mt Rita, kimbilio la walio hatarini;
Mt Rita, msaada wenye nguvu kwa wote;
Mt Rita, mastaajabio ya ulimwengu;
Mt Rita, uliyepokewa mbinguni kwa furaha;
———————————–
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia, *”Utusamehe Bwana”*
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia, *”Utusikilize Bwana”*
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia *”Utuhurumie”*
———————————-
*K:* Umemtia alama Ee Bwana mtumishi wako Rita
*W:* Kwa mhuli wa upendo na mateso
*TUOMBE*:
Ee Mungu , ambaye katika wema wako wa daima, umependa kusikiliza maombezi ya mtumishi wako Rita. Utujalie kupitia maombezi yake, yale ambayo yameshindikana kwa nguvu za kibinadamu. Utuhurumie sisi tunaoteseka, uwasaidie wote wasiokuamini wajue kuwa wewe ni tuzo la wanyenyekevu, mfariji wa wote wenye hofu, na nguvu ya wanyonge. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina
Mambo ya Kuzingatia
✔ Sali kwa imani na uvumilivu
✔ Fanya tafakari ya maisha yako na ongeza matendo ya huruma
✔ Kama inawezekana, shiriki Misa Takatifu wakati wa Novena
✔ Omba kwa moyo mnyenyekevu ukimkabidhi Mungu hitaji lako