Jinsi ya kusajili kikundi cha Ujasiriamali online BOT au TAMISEMI

Jinsi ya kusajili kikundi cha Ujasiriamali online BOT au TAMISEMI
Jinsi ya kusajili kikundi cha Ujasiriamali online BOT au TAMISEMI

Je mnakikundi chenu cha Ujasiria mali mnatamani kukisajili TAMISEMI au BOT Makala hii itakupa muongozo hatua za Kufuata ili kusajili kikundi ,Vigezo pia utaweza Kupakua fomu katika PDF.

Hatua za Kusajili Kikundi cha Ujasiriamali Mtandaoni

Afisa Maendeleo ya Jamii ndiye Muhusika Mkuu katika kuhakikisha vikundi vinajengewa uwezo.

Afisa Maendeleo ya Jamii atawapatia Mafunzo na mwongozo wa uandaaji wa Katiba.

Afisa Maendeleo ya Jamii atawapatia fomu ya maombi ya usajili ambayo itajazwa na viongozi.

Fomu hiyo itapitishwa na Afisa Mtendaji wa Mtaa kikundi kilipo.Baada ya hapo itatakiwa kupata uthibitisho wa Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata Husika.

5. Baada ya Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata kupitia Fomu na kuridhika, ataiwasilisha fomu ya maombi Ofisi ya Mendeleo ya Jamii Manispaa ambako vyeti vya Usajili vitaandaliwa na kisha Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata husika atapatiwa na kuvipatia vikundi vyake.

Kuandaa Nyaraka Muhimu: Kabla ya kuanza mchakato wa usajili, hakikisha una nyaraka zote muhimu kama vile katiba ya kikundi, orodha ya wanachama, na muhtasari wa vikao vya kikundi.

Kuingia kwenye Mfumo wa Kielektroniki: Tembelea mfumo wa usajili wa vikundi vya kifedha unaosimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania kupitia tovuti ya cmg.bot.go.tz. Mfumo huu unaruhusu vikundi kuwasilisha maombi ya usajili kwa njia ya mtandao.

Kuwasilisha Maombi: Jaza fomu za maombi ya usajili na uwasilishe nyaraka zinazohitajika kupitia mfumo wa mtandaoni. Hakikisha umejaza taarifa zote kwa usahihi na umeambatanisha nyaraka zote zinazohitajika.

Kulipia Ada ya Usajili: Lipa ada ya usajili kama inavyotakiwa na mamlaka husika. Ada hii inaweza kulipwa kupitia benki au njia nyingine za malipo zilizowekwa na halmashauri husika.

SOMA HII :  Jinsi ya kulipia simu za Mkopo Tigo

Soma Hii : Jinsi ya kulipa kwa Control Number

Kupokea Cheti cha Usajili: Baada ya maombi yako kukubaliwa, utapokea cheti cha usajili kinachothibitisha kuwa kikundi chako kimesajiliwa rasmi. Cheti hiki kitakuruhusu kufanya shughuli zako kisheria na kufaidika na fursa mbalimbali za kifedha.

Fomu za Kusajili kikundi Online Tamisemi au BOT

FOMU YA USAJILI-Maendeleo ya jamii.pdf

MUUNDO WA KATIBA-maendeleo ya jamii.pdf

About Burhoney 4806 Articles
Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati