Kama mmiliki wa gari nchini Tanzania, mojawapo ya wajibu wako ni kulipa ada ya maegesho yanayosimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA). Ada hizi hulipwa pale gari linapopaki kwenye maeneo rasmi ya maegesho katika miji mbalimbali kama Dar es Salaam, Dodoma, Arusha na mingineyo. Kukosa kulipia parking kunaweza kusababisha kuwekewa deni, kutozwa faini, au gari kufungwa (clamping).
TARURA ni Nani na Wanafanya Kazi Gani?
TARURA ni taasisi ya serikali chini ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI. Miongoni mwa majukumu yake ni:
Kusimamia na kutunza barabara za vijijini na mijini
Kuratibu huduma za maegesho ya magari mijini
Kukusanya ada za maegesho kwa kutumia mfumo wa kielektroniki
Namna ya Kulipia Parking kwa Njia ya Mtandao
1. Kupokea Taarifa ya Maegesho
Baada ya gari lako kupaki, afisa wa TARURA hukagua na kuingiza namba ya gari kwenye mfumo. Kisha unapaswa kupokea ujumbe mfupi (SMS) unaokuambia:
Gari lako limepakiwa wapi
Muda wa maegesho
Kiasi cha kulipia
Jinsi ya kulipa (kwa kutumia control number)
Mfano wa SMS:
“Gari T123ABC limeegeshwa Mtaa wa Samora. Control Number: 99123XXXX. Kiasi: TZS 500. Lipa kupitia Mpesa/Tigo Pesa/Airtel Money.”
2. Jinsi ya Kulipia kwa M-Pesa / Tigo Pesa / Airtel Money
Kwa M-Pesa
Piga 15000#
Chagua 4: Lipia kwa Mpesa
Chagua 5: Malipo ya Serikali
Ingiza control number
Weka kiasi kilichoelekezwa
Weka namba ya siri kuthibitisha
Kwa Tigo Pesa
Piga 15001#
Chagua 4: Lipia Bili
Chagua 3: Malipo ya Serikali
Weka control number
Weka kiasi
Thibitisha malipo
Kwa Airtel Money
Piga 15060#
Chagua 5: Lipa Bili
Chagua 6: Malipo ya Serikali
Ingiza control number
Weka kiasi
Thibitisha kwa kuweka PIN yako
Namna ya Kuangalia Kama Una Deni la Parking
Ikiwa hukuweza kulipia parking kwa wakati au hukujulishwa kwa SMS, unaweza kufuatilia mwenyewe kwa njia hizi:
Njia 1: Kupitia Simu (USSD)
Piga 15200#
Chagua namba 8 – Malipo ya Serikali
Chagua namba 1 – Lipa Serikali
Chagua TARURA – Maegesho
Ingiza namba ya gari (mfano: T123ABC)
Utapewa taarifa kama unadaiwa au la
Njia 2: Kupitia Tovuti ya TARURA
Tembelea: https://parking.tarura.go.tz
Ingiza namba ya gari lako
Taarifa zote za malipo na deni zitaonekana
Unaweza kupata control number ya kulipa papo hapo
Nini Kitatokea Ukishindwa Kulipa kwa Wakati?
Gari lako linaweza kufungwa na kitoaji clamping device
Unaweza kutozwa faini ya ziada
TARURA wanaweza kuchukua hatua za kisheria iwapo madeni yataendelea
MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA (FAQ)
Naweza lipia maegesho kabla sijapaki?
Ndiyo, kwa kutumia mfumo wa pre-payment kwenye app au tovuti ya TARURA.
Nikilipia kwenye kampuni ya simu, inachukua muda gani kuthibitishwa?
Malipo huthibitishwa mara moja au ndani ya dakika 1 hadi 3.
Nifanyeje gari langu likifungwa na TARURA?
Mpigie namba ya huduma kwa wateja (iliyopo kwenye gari lililofungwa), lipia deni lako, na utapewa maelekezo ya kuondoa kifaa.
Naweza kupata risiti?
Ndiyo, risiti ya kidigitali hutumwa kwa SMS baada ya malipo.