TANESCO (Shirika la Umeme Tanzania) linatumia mfumo wa control number kwa ajili ya malipo ya huduma zake kama vile:
Malipo ya bili ya umeme
Malipo ya kuunganishiwa umeme mpya
Malipo ya faini au huduma nyingine
Mfumo huu unarahisisha ufuatiliaji wa malipo na kuongeza usalama. Katika makala hii, tutaeleza kwa undani jinsi ya kulipa kwa kutumia control number ya TANESCO, iwe kupitia simu au benki.
Control Number ni Nini?
Control Number ni nambari maalum ya malipo inayotolewa na TANESCO kwa mteja kwa ajili ya kulipia huduma fulani. Kila control number inahusiana na mteja mmoja na malipo maalum.
Kwa mfano, ukihitaji kuunganishiwa umeme mpya au unadaiwa bili ya umeme, utapewa control number kwa malipo hayo tu.
Njia za Kupata Control Number ya TANESCO
Kupitia Ofisi ya TANESCO – Tembelea ofisi ya karibu na uombe control number kwa huduma unayotaka.
Kwa Simu au Mtandaoni – Kwa baadhi ya huduma, unaweza kuomba control number kupitia huduma za simu au tovuti ya TANESCO.
Kwa Kupitia SMS au Email – Baada ya maombi, control number huweza kutumwa moja kwa moja kwenye namba yako ya simu au barua pepe.
JINSI YA KULIPA KWA CONTROL NUMBER – NJIA MBALIMBALI
Hatua za Kulipa Kupitia M-Pesa
- Piga Namba ya Huduma ya M-Pesa: Piga *150*00# kwenye simu yako.
- Chagua ‘Lipa kwa M-Pesa’: Kutoka kwenye menyu, chagua “Lipa kwa M-Pesa”.
- Chagua ‘Malipo ya Serikali’: Katika orodha inayofuata, chagua “Malipo ya Serikali”.
- Ingiza Namba ya Malipo (Control Number): Weka namba ya malipo ambayo umepewa na TANESCO.
- Ingiza Kiasi cha Fedha: Weka kiasi cha fedha unachotaka kulipa.
- Thibitisha Muamala: Ingiza neno au namba yako ya siri ili kuthibitisha malipo.
- Hifadhi Ujumbe wa Simu: Baada ya muamala kukamilika, utapokea ujumbe wa kuthibitisha malipo. Ni muhimu kuhifadhi ujumbe huu kama ushahidi wa malipo yako.
Hatua za Kulipa Kupitia Tigo Pesa
- Piga Namba ya Huduma ya Tigo Pesa: Piga *150*01# kwenye simu yako.
- Chagua ‘Lipa Bili’: Kutoka kwenye menyu, chagua “Lipa Bili”.
- Chagua ‘Malipo ya Serikali’: Katika orodha inayofuata, chagua “Malipo ya Serikali”.
- Ingiza Namba ya Malipo (Control Number): Weka namba ya malipo ambayo umepewa na TANESCO.
- Ingiza Kiasi cha Fedha: Weka kiasi cha fedha unachotaka kulipa.
- Thibitisha Muamala: Ingiza neno au namba yako ya siri ili kuthibitisha malipo.
- Hifadhi Ujumbe wa Simu: Baada ya muamala kukamilika, utapokea ujumbe wa kuthibitisha malipo.
Hatua za Kulipa Kupitia Airtel Money
- Piga Namba ya Huduma ya Airtel Money: Piga *150*60# kwenye simu yako.
- Chagua ‘Lipa Bili’: Kutoka kwenye menyu, chagua “Lipa Bili”.
- Chagua ‘Malipo ya Serikali’: Katika orodha inayofuata, chagua “Malipo ya Serikali”.
- Ingiza Namba ya Malipo (Control Number): Weka namba ya malipo ambayo umepewa na TANESCO.
- Ingiza Kiasi cha Fedha: Weka kiasi cha fedha unachotaka kulipa.
- Thibitisha Muamala: Ingiza neno au namba yako ya siri ili kuthibitisha malipo.
- Hifadhi Ujumbe wa Simu: Baada ya muamala kukamilika, utapokea ujumbe wa kuthibitisha malipo.
4. Kupitia Benki
Unaweza pia kulipa control number ya TANESCO kupitia:
NMB
CRDB
NBC
TPB
Benki nyingine zilizounganishwa na mfumo wa GePG (Government e-Payment Gateway)
Njia za malipo ni kupitia teller, ATM, au mobile banking. Unachohitaji ni kuwasilisha control number na kiasi unachotakiwa kulipa.
Baada ya Malipo, Nini Kinafuata?
Uthibitisho wa malipo hutumwa kwa SMS au risiti.
Malipo huonekana moja kwa moja kwenye mfumo wa TANESCO ndani ya muda mfupi.
Unaweza kufuatilia kwa kupiga simu TANESCO au kutembelea ofisi zao ikiwa hufanyiwi huduma ndani ya saa 24.
MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA (FAQ)
Je, control number ya TANESCO inaisha muda wake?
Ndio, nyingi huwa na muda maalum wa matumizi (siku 7 hadi 14). Ikiisha, unatakiwa kuomba mpya.
Nifanyeje nikikosea control number?
Malipo hayatafanyika. Mfumo hukataa control number batili. Hakikisha unaingiza namba sahihi.
Ninawezaje kujua kiasi sahihi cha kulipa?
TANESCO watakupa control number pamoja na kiasi unachotakiwa kulipa, aidha kwa SMS, barua pepe au karatasi.
Je, naweza lipa kiasi pungufu ya kinachotakiwa?
Hapana. Mfumo utakataa malipo ikiwa kiasi hakilingani na kilicho kwenye control number.