Vijana wengi siku za hivi karibuni wamekuwa wakichangamkia fursa ya kuwekeza Pesa zao katika mfuo wa UTT Asset Management and Investor Services Plc (UTT AMIS) ndio mana nimepata msukumo kuwaandalia hii makala ya muongozo jinsi ya kujiunga UTT.
Chagua Mfuko wa Uwekezaji Unaotaka
UTT AMIS ina mifuko kadhaa ya uwekezaji, kila mmoja ukiwa na sifa tofauti. Kabla ya kujiunga, chagua mfuko unaolingana na malengo yako ya kifedha:
- Umoja Fund – Mfuko wa muda mrefu kwa wanaotaka ukuaji wa mtaji.
- Liquid Fund – Mfuko wa muda mfupi wenye ukwasi wa haraka.
- Bond Fund – Mfuko wa uwekezaji kwenye hati fungani za serikali.
- Wekeza Maisha Fund – Mfuko wa malengo ya muda mrefu kama elimu na ustaafu.
- Jikimu Fund – Mfuko unaolenga kutoa mapato ya mara kwa mara.
Soma Hii :Jinsi ya Kununua Vipande Vya Uwekezaji Vya UTT AMIS
Pata na Jaza Fomu ya Maombi
Fomu ya kujiunga na UTT AMIS inapatikana kwa njia zifuatazo:
✅ Kupakua kutoka kwenye tovuti rasmi: www.uttamis.co.tz
✅ Kupata moja kwa moja katika ofisi za UTT AMIS.
✅ Kupitia matawi ya benki washirika kama CRDB, NMB, na Stanbic.
Baada ya kupata fomu, jaza taarifa zako binafsi, ikiwa ni pamoja na:
- Jina kamili
- Namba ya simu
- Barua pepe
- Nakala ya kitambulisho (NIDA, Leseni ya Udereva, au Pasipoti)
- Anuani kamili
- Akaunti ya benki kwa malipo ya faida
Lipa Kiasi cha Awali cha Uwekezaji
Baada ya kujaza fomu, utahitajika kufanya malipo ya awali ili kuanza uwekezaji wako.
A. Malipo Kupitia Benki
Unaweza kulipia kupitia akaunti za UTT AMIS zilizopo kwenye benki zifuatazo:
- CRDB Bank
- NMB Bank
- Stanbic Bank
B. Malipo Kupitia Simu za Mkononi
Kwa wale wanaopendelea kutumia simu, unaweza kulipa kupitia huduma za kifedha za simu kama:
- M-Pesa
- Tigo Pesa
- Airtel Money
- HaloPesa
- T-Pesa
Mfano wa Jinsi ya Kulipa kwa M-Pesa:
- Piga 15000#
- Chagua 4 (Lipa kwa M-Pesa)
- Chagua 4 (Weka namba ya kampuni)
- Ingiza Namba ya Kampuni ya UTT AMIS
- Weka Namba ya Akaunti (Namba yako ya usajili UTT AMIS)
- Weka kiasi unachotaka kuwekeza
- Thibitisha malipo
Wasilisha Fomu na Stakabadhi za Malipo
Baada ya malipo, wasilisha fomu yako pamoja na nakala ya malipo kwenye ofisi za UTT AMIS au kupitia benki washirika.
5. Pokea Cheti cha Umiliki wa Vipande
Baada ya maombi yako kushughulikiwa, utapokea Cheti cha Umiliki wa Vipande (Statement of Unit Holdings), kinachothibitisha uwekezaji wako katika mfuko husika.
Faida za Kujiunga na UTT AMIS
- Urahisi wa Kuwekeza: Unaweza kuwekeza kupitia simu yako kwa kutumia huduma ya UTT SIMINVEST.
- Uwazi na Uwezo wa Kufuata Maendeleo: UTT AMIS inatoa taarifa za mara kwa mara kuhusu thamani ya vipande vyako na salio la akaunti yako.
- Faida Shindani: Uwekezaji katika mifuko ya UTT AMIS unakupa nafasi ya kupata faida nzuri kutokana na uwekezaji wako.