JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

Je Unafanya Biashara ya chakula na unawama katika kufanya matangazo au Matngazo yako hayaleti mrejesho Mzuri Basi hapa kupitia hii makala tumekuwekea vipengele vya kufuata unapotaka kuandaa Tangazo la kuvuta wateja na mfano wa Tangazo la Biashara ya Chakula.

Vipengele Muhimu vya Tangazo la Biashara ya Chakula

  1. Kichwa Kinachovutia (Headline)

    • Kiguse hisia au matamanio ya mteja. Chakula kinahusiana sana na ladha, harufu, na hisia. Mfano: “Ladha Halisi ya Nyumbani Unayoikosa!”

  2. Maelezo ya Bidhaa au Huduma

    • Eleza aina ya chakula unachouza (kitamaduni, fast food, vyakula vya afya, n.k), mahali kilipoandaliwa, au ubora wake.

  3. Ofa au Faida ya Kipekee

    • Wateja huvutiwa na ofa maalum kama punguzo, usafirishaji wa bure, au huduma ya haraka. Toa sababu ya kwanini wachague chakula chako.

  4. Picha ya Kuvutia

    • Katika matangazo ya chakula, picha nzuri ya chakula husababisha mteja kuhisi njaa mara moja! Ikiwezekana, tumia picha halisi za vyakula vyako.

  5. Mwito wa Kuchukua Hatua (Call to Action)

    • Mfano: “Agiza sasa!”, “Tembelea mgahawa wetu leo!”, “Pata menu kupitia WhatsApp.”

  6. Taarifa za Mawasiliano na Mahali

    • Hakikisha mteja anaweza kujua unapatikana wapi na jinsi ya kuwasiliana na wewe.

Mfano wa Tangazo la Biashara ya Chakula

Mfano wa Tangazo la Biashara ya Chakula

 LADHA HALISI YA NYUMBANI – JIKONI TAMU CATERING

Soma Hii : Mfano wa Tangazo la Biashara Linalovutia Wateja

Unakumbuka ile ladha ya chakula cha nyumbani kilichoandaliwa kwa upendo? Jikoni Tamu inakurudisha hapo!

Tunapika vyakula vya Kitanzania vilivyopikwa kwa viungo halisi na kwa usafi wa hali ya juu!

 Pilau ya nyama laini yenye harufu ya karafuu
 Maharage ya nazi yaliyopikwa kwa muda muafaka
 Chapati laini na za moto kila siku
 Saladi safi, sambusa na mapochopocho

OFa KABAMBE!: Agiza kwa watu 3 au zaidi upate juice ya bure!

 Tunatoa huduma ya usafirishaji ndani ya Dar es Salaam
 Agiza kupitia WhatsApp: 07xxxxxx
Tunapatikana Kinondoni, karibu na Shekilango

Jikoni Tamu – Kula kama uko nyumbani!

JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA
Share.

Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati

Leave A Reply