Kuanzisha kampuni ni ndoto ya wengi wanaotamani kujiajiri au kuanzisha biashara rasmi inayoweza kukua na kuaminika kisheria. Tanzania, mchakato wa kusajili na kuanzisha kampuni umeboreshwa kwa kiasi kikubwa, na sasa unaweza kufanyika kwa urahisi zaidi kwa njia ya mtandao kupitia taasisi kama BRELA (Business Registrations and Licensing Agency)
Aina za Kampuni Tanzania
Kabla ya kusajili kampuni, ni muhimu kuelewa aina mbalimbali za kampuni zinazotambulika kisheria:
Private Company Limited by Shares (Ltd) – Kampuni ya binafsi yenye wanahisa wachache.
Public Company Limited by Shares (PLC) – Kampuni inayoweza kuuza hisa kwa umma.
Company Limited by Guarantee – Kwa taasisi zisizolenga faida (NGOs).
Sole Proprietorship – Umiliki binafsi (si kampuni, ila ni biashara rasmi).
Partnership – Ushirika wa watu wawili au zaidi.
Hatua 8 Muhimu za Kuanza Kampuni Tanzania
1. Weka Wazo la Biashara
Kabla ya mchakato wowote wa usajili, hakikisha una wazo imara la biashara unayotaka kuanzisha, soko lako, washirika (ikiwa wapo), na malengo ya muda mrefu.
2. Tafuta Jina la Kampuni
Tumia tovuti ya BRELA ORS – Online Registration System kuangalia kama jina unalotaka kutumia lipo au halijatumiwa. Ukipata jina linalopatikana, unaweza kulihifadhi (name reservation) kwa siku 30.
3. Tengeneza Hati za Kampuni (Memorandum & Articles of Association)
Hati hizi zinaelezea malengo ya kampuni, muundo wake wa ndani, majukumu ya wanahisa, na jinsi kampuni inavyoendeshwa.
4. Jaza Fomu za BRELA Mtandaoni
Fomu muhimu ni:
Fomu 14a – Maelezo ya kampuni
Fomu ya wanahisa (Particulars of Shareholders)
Fomu ya wakurugenzi
Fomu ya Registered Office
5. Lipa Ada ya Usajili
Malipo yanategemea aina ya kampuni na ukubwa wake. Kwa kampuni ndogo, ada ya kawaida ni kati ya Tsh 95,000 hadi 300,000. Malipo yote hufanyika kupitia control number utakayopata kwenye mfumo wa BRELA.
6. Pokea Cheti cha Usajili (Certificate of Incorporation)
Baada ya kulipa na nyaraka kukaguliwa na kukubaliwa, utapewa cheti rasmi cha usajili – ishara kuwa kampuni yako imesajiliwa kisheria.
7. Jisajili na Mamlaka Nyingine Muhimu
TRA – Kwa ajili ya kupata TIN ya Kampuni na ya Wakurugenzi
NSSF – Ikiwa unaajiri wafanyakazi
OSHA – Kwa usalama wa mahali pa kazi
WCF – Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi
TBS/TFDA – Ikiwa biashara inahusisha bidhaa zinazodhibitiwa
8. Fungua Akaunti ya Benki ya Kampuni
Baada ya kupata TIN na cheti cha usajili, unaweza kufungua akaunti ya benki kwa jina la kampuni yako. Hii itasaidia kusimamia fedha kwa uwazi na kisheria.
Faida za Kuanzisha Kampuni Rasmi
Kuaminika zaidi kwa wateja na wawekezaji
Uwezo wa kupata mikopo ya kibiashara
Ulinzi wa mali binafsi (limited liability)
Nafasi ya kukua na kushindana kitaifa na kimataifa
Kisheria, unalindwa dhidi ya madhara ya kibiashara
MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA (FAQs)
Je, kampuni ndogo inaweza kusajiliwa na mtu mmoja?
Ndio. Kampuni binafsi (Private Company Limited) inaweza kuwa na mkurugenzi mmoja na mwanahisa mmoja.
Usajili wa kampuni huchukua muda gani?
Kwa kawaida, siku 3–7 baada ya kuwasilisha nyaraka zote sahihi.
Je, lazima kuwa na ofisi ya kudumu?
Ndio, unapaswa kuwa na registered office address, hata kama ni ya muda.
Je, kuna gharama nyingine baada ya kusajili?
Ndio. Kuna gharama za kupata TIN, leseni ya biashara, na usajili na taasisi nyingine kama TRA, OSHA n.k.