Jinsi ya Kuangalia Salio NSSF Kwa njia ya Simu & Online

Jinsi ya Kuangalia Salio NSSF Kwa njia ya Simu & Online
Jinsi ya Kuangalia Salio NSSF Kwa njia ya Simu & Online

Wanachama wa NSSF Sasa wanaweza kufuatilia michango yao kujua salio la michango yao Wakiwa nyumbani kwa kutumia simu zao ,Wanaweza kufuatilia Kwa njia ya simu.

Kuhakikisha kuwa unafuatilia salio la akaunti yako ya NSSF (National Social Security Fund) ni muhimu ili kujua jinsi michango yako inavyoendelea na vile vile kujipanga kwa ajili ya mafao yako ya baadaye. NSSF ni mfuko wa hifadhi ya jamii ambao unatoa huduma muhimu kwa wafanyakazi nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na pensheni, matibabu, na faida nyinginezo. Kuangalia salio lako la NSSF kutakusaidia kujua ni kiasi gani umewekeza kwa ajili ya kustaafu na faida zingine zinazotolewa na mfuko huo.

Umuhimu wa Kujua na Kufuatilia Salio la Michango yako NSSF

Kufuatilia salio lako la NSSF ni muhimu kwa sababu:

  • Kujua michango yako: Kuangalia salio la NSSF kutakusaidia kufahamu kama michango yako inafanyika ipasavyo.

  • Kupanga kwa ajili ya kustaafu: Kujua salio lako kutakuwezesha kupanga mipango yako ya baadaye na kufanya maamuzi bora kuhusu fedha zako za kustaafu.

  • Kufuatilia mafao yako: Unaweza kutambua kama unastahili kupata mafao na kuona kama unakubaliana na taarifa za michango yako.

1. NSSF Taarifa – Mobile App

Kwa kutumia programu hii utapata taarifa za michango, salio na huduma mbalimbali.

Jinsi ya Kutumia:

• Pakua “NSSF Taarifa” kutoka “Google Play Store”.

• Utapata taarifa binafsi za uanachama.

• Kuangalia taarifa za michango iliyowasilishwa kwenye Shirika bofya “Statements”.

2. NSSF Taarifa – WhatsApp

Jinsi ya Kutumia:

• Hifadhi namba maalum ya 0756 140 140 kwenye simu.

• Fungua Programu ya WhatsApp kisha tuma ujumbe wa salamu “Hello” au “Habari”.

SOMA HII :  Jinsi ya Kuingia Ulaya: Mwongozo Kamili kwa Wasafiri

• Utapokea ujumbe wenye maelekezo ya jinsi ya kutumia huduma hii.

• Andika neno “Statement” kupata taarifa ya michango yote iliyowasilishwa, au tuma neno “Balance” kupata ujumbe wenye salio la michango iliyowasilishwa.

3. NSSF Taarifa – SMS

Jinsi ya Kutumia:

Ingia ingia kwenye programu ya Ujumbe Mfupi (SMS) kisha tuma ujumbe kwenda namba 15200 kupata huduma zifuatazo:

Kwa Salio/Balance ya michango tuma ujumbe

NSSF SALIO (Namba ya Mwanachama) (Mwaka)

Au

NSSF BALANCE (Member Number) (Year)

Kwa Taarifa/Statement ya michango tuma ujumbe

NSSF TAARIFA (Namba ya Mwanachama) (Mwaka)

Au

NSSF STATEMENT (Member Number) (Year)

4 .Kupitia Huduma za NSSF kwa Wateja (Call Center)

NSSF pia ina huduma ya wateja ambapo unaweza kupiga simu na kuongea na mtumishi wa huduma kwa wateja ili kuangalia salio lako.

  1. Piga simu kwa namba ya huduma kwa wateja: Piga simu kwa namba ya NSSF: 0800 75 00 00.

  2. Zungumza na mtumishi wa huduma kwa wateja: Wafanyakazi wa huduma kwa wateja watakuuliza taarifa za akaunti yako, na kisha watakupa taarifa za salio lako.

5. Mfumo wa ‘Member Portal’

Jinsi ya Kuangalia Salio NSSF Kwa njia ya Simu & Online

Kupitia Mfumo ambao unapatikana katika tovuti ya Shirika yaan www.nssf.go.tz utaweza:

• Kuangalia taarifa za michango yote iliyowasilishwa na Mwajiri wako katika Shirika au michango iliyowasilishwa na mwanachama kwa wanachama wa hiari.

• kupata taarifa za michango (Statements).

Ili upate kuona taarifa zako unatakiwa kuwa namba ya simu ambayo uliisajili NSSF endapo ulibadilisha au haukuiweka tunaomba ufike katika ofisi ya

NSSF iliyojirani yako ili kuweza kuboresha Taarifa zako na kuendelea kufurahia huduma zetu

“NSSF Tunajenga Maisha yako ya Sasa na Baadaye”

SOMA HII :  Jinsi ya Kupata Visa ya Passport

 

About Burhoney 4809 Articles
Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati