Fahamu utaratibu na Hatua unazopaswa kuziuata ili Kuangalia Matokeo ya mtihani wa Taifa Darasa La Saba, Matokeo ya darasa la saba yana umuhimu mkubwa kwa wanafunzi na wazazi nchini Tanzania. Matokeo haya yatatoa picha ya jinsi wanafunzi walivyofanya katika mtihani wa kitaifa na ni hatua muhimu kuelekea shule ya sekondari. Ili kuhakikisha unapata taarifa sahihi, ni muhimu kujua tarehe za kutangazwa kwa matokeo na jinsi ya kuyapata.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba
Matokeo ya Mtihai wa Kitaifa wa Darasa la saba unaosimamiwa na Necta yanaweza kuwa accessed kwa njia Mbalimbali lakini kwenye hii makala tumejadili njia mbili za muhimu ambazo ni kuangalia matokeo ya la saba kwa njia ya Mtandao yani kwenye Website ya Necta na njia ya pili ni kwa njia ya simu sms.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba Kupitia Tovuti ya NECTA
Hatua ya 1: Kutembelea Tovuti Rasmi ya NECTA
- Fungua kivinjari cha intaneti katika simu yako au kompyuta
- Andika moja kwa moja anwani ya tovuti ya NECTA, ambayo ni www.necta.go.tz.

Hatua ya 2: Chagua Kipengele cha Matokeo:
- Mara tu baada ya kuingia kwenye tovuti ya NECTA, Nenda kwenye Menyu kuu na tafuta sehemu iliyoandikwa “Matokeo” au “Results.”
- Bonyeza kwenye kipengele cha “Results”.
- Menyu ndogo ya kushuka chini itajitokeza, Bonyeza kwenye kiungo kilichoandikwa PSLE kitakachokupeleka kwenye ukurasa rasmi wa matokeo darasa la saba (PSLE Results).

Hatua ya 3: Chagua Mtihani wa Darasa la saba kwa Mwaka 2024
- Ukurasa wa matokeo ya darasa la saba utakupa orodha ya mitihani kwa miaka mbalimbali.
- Bonyeza au chagua linki ya mtihani wa mwaka 2024

Hatua ya 4: Tazama matokeo kwa mikoa yote
- Baada ya kuchagua na kubonyeza linki ya mwaka husika,
- Utapelekwa kwenye ukurasa rasmi wa matokeo yote ya darasa la saba kwa mwaka 2024
- Hapa utaweza kupata matokeo ya darasa la saba kwa ngazi ya miko yote
- Tafuta na bonyeza kwenye kiunganisho cha Jina la mkoa husika ili kuatazama matokeo katika mkoa husika

Hatua ya 5: Angalia Matokeo yako
- Mara baada ya kubonyeza linki ya mkoa husika,
- Ukurasa mwingine wa matokeo katika mpangilio wa wilaya katika mkoa huo utafunguka
- Bonyeza linki au kiunganishi cha matokeo ya wilaya husika ili kuangalia matokeo katika wilaya hiyo
- Baada ya kubonyeza linki au kiunganishi cha wilaya husika, utaona orodha ya shule zote katika wilaya hiyo
- Tafuta shule uliyofanyia mtihani wako, na bonyesha kwenye linki ya shule hiyo
- Baada ya kufanya hivyo, ukurasa mwingine wenye matokeo ya shule hiyo utafunguka, kuangalia matokeo yako tafuta jina mwanafunzi
- Matokeo ya mtahiniwa yatatokea kwenye skrini, yakionyesha alama zake katika masomo mbalimbali.

Hatua ya 6: Pakua na Chapisha matokeo yako
Ikiwa unahitaji kuwa na nakala ya matokeo yako kwa ajili ya matumizi ya baadaye, unaweza kupakua matokeo hayo au kuchapisha matokeo moja kwa moja kutoka katika tovuti kwa kubonyeza kitufe cha “Print” au “Save as pdf.”

Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba Kwa SMS
Piga *152*00# Chagua Namba 8 Elimu
kisha Bonyeza namba 2 NECTA
Kisha fuata Maelekezo yaliopo Kupata Matokeo yako
Hatua Baada ya Kupata Matokeo
Mara baada ya kupata matokeo, ni muhimu kwa wazazi na wanafunzi kufanyia kazi matokeo haya kwa njia chanya. Hapa kuna hatua kadhaa za kuchukua:
- Kujadili Matokeo: Wazazi wanapaswa kukaa na watoto wao na kujadili alama walizopata. Hii itasaidia kuelewa nguvu na udhaifu wa mwanafunzi.
- Kuchagua Shule Bora: Wanafunzi wenye alama nzuri wanaweza kuchagua shule za sekondari zinazofaa. Tafiti shule zenye sifa nzuri na ambazo zinawapa wanafunzi fursa nzuri za kujifunza na kukuza vipaji vyao.
- Msaada wa Kiakademia: Ikiwa mwanafunzi amepata alama za chini katika masomo fulani, ni muhimu kutafuta msaada wa ziada ili kumsaidia kuboresha. Hii inaweza kuwa katika mfumo wa darasa la ziada au masomo ya nyumbani.
Maana ya Alama na Madaraja Katika Matokeo ya Darasa la saba
GREDI | ALAMA | MAELEZO |
A | 75-100 | Bora sana (Excellent): Hii ina maanisha kiwango bora zaidi ambacho mwanafunzi ameonyesha uelewa wa hali ya juu na uwezo wa kutumia maarifa kwa usahihi. |
B | 65-74 | Vizuri sana (Very Good): Hii inamaanisha uelewa mzuri ambapo mwanafunzi ameonyesha uwezo wa kutosha katika somo husika. |
C | 45-64 | Vizuri (Good): Kiwango hiki kinaonyesha uhusiano wa wastani wa uelewa na utekelezaji katika somo. Ni kiwango kinachokubalika lakini kuna nafasi ya kuboresha |
D | 30-44 | Inaridhisha (Satisfactory): Mwanafunzi ameonyesha kiwango cha kawaida cha uelewa katika somo husika. Mwanafunzi amefanikiwa kufikia kiwango cha chini kinavyohitajika katika ufaulu, lakini bado hajaonyesha umahiri au uelewa wa kina. |
F | 0-29 | Feli (Fail): Hii inaonyesha kuwa mwanafunzi amepata alama ya chini ya kiwango kinachohitajika na huenda akahitajika kurudia mtihani au kushiriki masomo ya ziada |
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kuhusu Matokeo ya Darasa la Saba
1. Je, matokeo ya darasa la saba 2024 yanatoka lini?
Matokeo haya kwa kawaida hutangazwa katika kipindi cha robo ya mwisho ya mwaka, mara nyingi kuanzia mwezi wa Oktoba hadi Novemba. Hata hivyo, tarehe rasmi itatolewa na NECTA, unashauriwa kufuatilia kwa ukaribu tovuti ya NECTA kwa taarifa rasmi na habari zenye uhakika kuhusu matokeo hayo.
2. Inachukua muda gani baada ya mtihani hadi matokeo kutangazwa?
Kwa kawaida, matokeo hutangazwa takriban miezi miwili (2) hadi mitatu (3) baada ya mitihani kufanyika. Katika Kipindi hiki NECTA hujipatia muda wa kutosha kukusanya, kusahiisha, na kuchakata matokeo kabla ya kuyatangaza rasmi.
2. Je, matokeo yanaweza kubadilika baada ya kutangazwa?
Mara nyingi matokeo yanayotangazwa huwa ni ya mwisho, hata hivyo kuna uwezekano wa mabadiliko kufanyika ikiwa kuna makosa yalitokea wakati kusahisha au uchakataji wa matokeo ya mitihani. NECTA inaweza kukagua upya matokeo yako iwapo kutakuwa na maombi maalum na lenye sababu za msingi na zenye mashiko.
3. Je, kuna ada yoyote katika kuangalia matokeo darasa la saba 2024 mtandaoni au kupitia simu?
Hakuna gharama au ada yoyote inayohitajika Ili kutazama matokeo yako kupitia tovuti rasmi ya NECTA. Hata hivyo, matumizi ya huduma za USSD kupitia simu za mkononi yanaweza kuhusisha gharama za mawasiliano (Gharama kwa kila SMS ni Tshs 100/= kwa huduma za USSD)