Kama unamiliki gari au unapanga kununua gari lililotumika, ni muhimu kuhakikisha halina madeni yoyote ya trafiki. Mfumo wa TMS (Traffic Management System) ni jukwaa rasmi linalotumiwa na mamlaka husika kukusanya na kuhifadhi taarifa za magari, ikiwa ni pamoja na faini na madeni ya trafiki. Katika makala hii, tutakuelekeza jinsi ya kuangalia deni la gari kupitia mfumo wa TMS Traffic Check kwa haraka na kwa urahisi.
Umuhimu wa Kuangalia Deni la Gari
Kuangalia deni la gari ni muhimu kwa sababu:
- Husaidia kuepuka ununuzi wa gari lenye madeni.
- Hukuruhusu kulipa faini mapema na kuepuka ongezeko la gharama.
- Huwezesha umiliki wa gari kuwa safi kisheria.
- Hupunguza usumbufu wa kusimamishwa na polisi kwa madeni yasiyojulikana.
Bonyeza Hapa Kujua deni la gari – TMS TRAFFIC CHECK
Jinsi ya Kulipa Deni la Trafiki
Ikiwa gari lako lina deni la trafiki, unaweza kulilipa kupitia:
- Mfumo wa malipo wa mtandaoni kwenye tovuti ya mamlaka husika.
- Benki zilizoidhinishwa zinazoshirikiana na serikali.
- NBC
- NMB
- CRDB
- Huduma za simu za mkononi kama Mpesa, Tigo Pesa, au Airtel Money. Kupitia mitandao ya simu Lipa kwa kutumia namba ya kampuni 001001 kisha weka kumbukumbu namba yako iliyopo kwenye TMS au receipt uliyopatiwa
- Ofisi za TRA au Polisi wa Trafiki kwa malipo ya moja kwa moja.