Fahamu hatua unazopaswa kuzifuata ili kutuma Maombi ya Mkopo kwa Elimu ya juu Tanzania ili kufadhili Gharama za masomo yako endapo utakidhi vigezo na Masharti.
Jinsi Ya Kuomba Mkopo Wa Elimu Ya Juu HESLB
Kufanya Utafiti wa Sifa za Uhitimu
Kabla ya kuanza mchakato wa kuomba mkopo, ni muhimu kujua vigezo vya uhitimu vilivyowekwa na HESLB. Vigezo hivi vinaweza kuwa vinahusu sifa za kitaaluma, kikomo cha umri, au programu za masomo. Ni muhimu kupitia na kufahamu masharti haya ili kuhakikisha kuwa unakidhi vigezo vinavyotakiwa.
Kukusanya Nyaraka Zinazohitajika
Ili kukamilisha maombi yako ya mkopo, utahitaji kutoa nyaraka kadhaa muhimu. Hizi nyaraka ni pamoja na:
- Vyeti vya Masomo: Nakala rasmi za vyeti vya shule, stakabadhi za matokeo, na nyaraka nyinginezo za kitaaluma.
- Hati za Utambulisho: Kitambulisho cha taifa, cheti cha kuzaliwa, au pasipoti.
- Barua ya Udahili: Barua rasmi ya udahili kutoka chuo kikuu unachotarajia kujiunga nacho.
Kuanza Maombi Mtandaoni Kupitia OLAMS
Tembelea tovuti ya OLAMS kwa kufungua kivinjari chako cha mtandao na kuingia kwenye HESLB OLAMS kupitia kiungo “https://olas.heslb.go.tz“. Kwenye ukurasa wa mwanzo, bonyeza “Omba Mkopo” na uchague kama wewe ni mwanafunzi wa NECTA au si mwanafunzi wa NECTA.
Mara tu unapochagua kati ya “NECTA” au “Non-NECTA,” utaona fomu ya kujisajili. Hakikisha kuwa umejaza taarifa zote muhimu kwa usahihi. Weka nyaraka zote zinazohitajika katika muundo unaotakiwa na hakikisha umezipitia kabla ya kuzituma.
Kulipa Ada ya Maombi
Wanafunzi wanatakiwa kulipa ada ya maombi isiyorejeshwa ya TZS 30,000.00 kupitia GePG kwa kutumia NMB, CRDB, TPB, Vodacom M-PESA, TIGO PESA, au AIRTEL MONEY. Baada ya kufanya malipo, hakikisha umebaki na risiti ya malipo kwa ajili ya kumbukumbu.
Kusubiri Uidhinishaji na Utoaji wa Mkopo
Baada ya kuwasilisha maombi yako, HESLB itachambua uhitimu wako na tathmini mahitaji yako ya kifedha. Ikiwa maombi yako yatakubaliwa, utapokea taarifa juu ya kiasi cha mkopo na jinsi utakavyopokea mkopo huo. Kawaida, fedha za mkopo zitaingizwa moja kwa moja kwenye akaunti ya taasisi ya elimu husika.
SOMA HII :Hivi Hapa Viwango Vya Mishahara Ya Watumishi wa Serikali (TGS salary Scale)
Jinsi ya Kuangalia Hali ya Maombi Yako
Orodha ya waombaji waliofanikiwa pamoja na kiasi walichopewa itachapishwa kwenye tovuti rasmi ya HESLB HESLB.
Mawasiliano na HESLB
Kama una maswali zaidi au unahitaji msaada wa ziada, tafadhali wasiliana na HESLB kupitia kituo cha simu kwa namba +255 22 286 4643 au barua pepe info@heslb.go.tz.
Ili kupata fomu ya mkopo elimu ya juu, Maombi ya mkopo elimu ya juu huanzia mtandaoni katika mfumo wa kutuma maombi ya Mkopo Elimu ya juu ijulikanayo kama OLAMS (Online Loan Applications and Management System).
SIFA KUU ZA KUPATA MKOPO WA ELIMU YA JUU
- Awe mtanzania
- Awe ameomba mkopo kwa utaratibu ulioelekezwa.
- Awe amepata udahili (admission) kwenye chuo kinachotambuliwa na jina lake kuwasilishwa Bodi ya mikopo.
- Asiwe na chanzo kingine cha kugharamia masomo yake ya chuo kikuu (mfadhili, ZHELB n.k).
Sifa za Jumla Kwa Wanafunzi wanaojiunga na Vyuo
- Uraia: Mwombaji ni lazima awe raia wa Tanzania.
- Umri: Mwombaji ashindwe miaka 35 wakati wa kuomba mkopo.
- Udahili: Ni sharti mwombaji awe amedahiliwa katika taasisi ya elimu ya juu nchini Tanzania inayotambuliwa.
- Maombi kupitia OLAMS: Maombi yote ya mkopo yanafanywa kupitia Mfumo wa Maombi na Usimamizi wa Mikopo (OLAMS).
- Ukosefu wa kipato: Mwombaji hapaswi kuwa na chanzo kingine cha mapato, kama vile ajira au mkataba serikalini au sekta binafsi.
- Kurejesha mkopo uliopita: Kwa wale ambao wameshawahi kupokea mkopo wa HESLB, ni lazima wawe wamerejesha angalau asilimia 25 ya mkopo huo kabla ya kuomba tena.
- Ufaulu wa masomo: Waombaji wanatakiwa wawe wamehitimu elimu ya kidato cha sita au stashahada ndani ya miaka mitano, kuanzia mwaka 2020 hadi 2024.
Sifa za Msingi kwa Wanafunzi Wanaondelea na Masomo
Kwa wanafunzi ambao tayari wako vyuoni na wanataka kuendelea kupata mkopo, au wale wanaotaka kuomba mkopo kwa mara ya kwanza wakiwa wanaendelea na masomo, wanatakiwa kutimiza yafuatayo:
- Ufaulu: Ni lazima wawe wamefaulu mitihani yao ili waweze kuendelea na mwaka unaofuata wa masomo.
- Barua ya kurejea (kama inafaa): Kwa wale waliowahi kuahirisha masomo, wanapaswa kuwa na barua ya kurejea masomoni kutoka chuo husika.
- Kurudia mwaka: Wanafunzi hawaruhusiwi kurudia mwaka wa masomo zaidi ya mara moja katika kipindi chote cha masomo yao.
- Kuahirisha masomo: Hairuhusiwi kuahirisha masomo kwa zaidi ya miaka miwili mfululizo.
- Namba ya Utambulisho ya Taifa (NIN) na namba ya usajili: Lazima wawasilishe namba hizi kabla ya kupokea fedha za mkopo katika mwaka wao wa tatu wa masomo.
Nyaraka Za Kuambatisha Wakati Wa Maombi Ya Mkopo
Zifuatazo ni nyaraka muhimu za kuambatisha kwenye maombi ya mkopo: –
- Cheti cha kuzaliwa kutoka mamlaka husika, ZCSRA kwa waombaji kutoka Zanzibar au Namba ya Uhakiki (verification number) kutoka RITA kwa waombaji kutoka Tanzania Bara;
- Vyeti vya vifo vya wazazi kuthibitisha uyatima kutoka mamlaka husika, ZCSRA kwa waombaji waliozaliwa Zanzibar au Namba ya Uhakiki (verification number) kutoka RITA kwa waombaji waliozaliwa Tanzania Bara;
- Barua kutoka RITA au ZCSRA kuthibitisha taarifa za kuzaliwa kwa waombaji waliozaliwa nje ya nchi. Kwa mwombaji ambaye mzazi wake amefariki nje ya nchi anapaswa kuwasilisha barua kutoka RITA au ZCSRA kuthibitisha taarifa za kifo.
- Fomu ya Kuthibitisha Ulemavu wa mwombaji au mzazi wake iliyoidhinishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) au Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO);
- Namba ya kaya ya Mnufaika kutoka kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuthibitisha ufadhili wa kiuchumi alioupata mwombaji wakati wa elimu yake ya sekondari.
Maswali na Majibu Kuhusu Utoaji Wa Mikopo
Zipi ni sifa kuu za kupata mkopo wa elimu ya juu?
Mwombaji;
- Awe mtanzania
- Awe ameomba mkopo kwa utaratibu ulioelekezwa (online)
- Awe amepata udahili (admission) kwenye chuo kinachotambuliwa na jina lake kuwasilishwa Bodi ya Mikopo
- Asiwe na chanzo kingine cha kugharamia masomo yake ya chuo kikuu (mfadhili, ZHELB n.k)
- Maelezo ya kina kuhusu sifa na vigezo hutolewa na Mwongozo
Mkopo wa elimu ya juu unaombwaje?
- Maombi yote yanafanywa kwa njia ya mtandao wa Bodi ya Mikopo
- Kila mwombaji anapaswa kusoma kwa makini mwongozo unaotolewa ndani ya mwaka husika wa masomo
- Mwombaji atumie namba ya mtihani wa kidato cha nne kujisajili
Ni nyaraka gani muhimu zinatakiwa wakati wa kuomba mkopo?
- Cheti cha kuzaliwa cha mwombaji kilichothibitishwa na RITA/ZCSRA
- Cheti cha kifo ikiwa umepoteza mzazi kilichothibitishwa na RITA/ZCSRA
- iKitambulisho cha mdhamini (NIDA, Mpiga Kura, Leseni ya Udereva au Pasi ya Kusafiria). Unaweza kutumia kimoja kati ya vitambulisho hivi
- Fomu ya ufadhili iliyojazwa kwa usahihi ikiwa ulifadhiliwa katika masomo ya sekondari
- Barua ya Mganga Mkuu wa Wilaya au Mkoa ikiwa mwombaji au mzazi wake ana ulemavu vii.
- Picha (passport size) za mwombaji wa mkopo na mdhamini wake (mdhamini anaweza kuwa mzazi au mlezi)
Iwapo mwanafunzi/Mwombaji wa mkopo hajaridhika na kiwango cha mkopo alichopatiwa au hajapangiwa mkopo anatakiwa kufanya nini?
- Fursa ya kukata rufaa hutolewa baada ya kukamilisha zoezi la kupanga mikopo
- Ikitokea mwombaji akakosa kwenye rufaa, atapata fursa ya kuomba tena kwa mwaka unaofatia
Mambo gani muhimu yanapaswa kuzingatiwa wakati wa kuomba mkopo?
- Hakikisha umesaini fomu ya maombi ya mkopo
- Hakikisha mdhamini wako amesaini fomu yako katika eneo lake
- Hakikisha fomu yako imesainiwa na kugongwa mihuri na Serikali ya Mtaa au Kijiji chako
- Hakikisha fomu yako imesainiwa na mwanasheria au hakimu kuthibitisha taarifa zako na za mdhamini wako
Mkopo unatolewa kwenye vipengele (Loanable Items) vipi?
- Chakula na malazi
- Ada ya mafunzo
- Vitabu na viandikwa
- Mahitaji maalumu ya kitivo
- Utafiti
- Mafunzo kwa vitendo
Nifanye nini ikiwa na nina swali kuhusu mkopo wa Elimu ya Juu?
- Taarifa zote kuhusu mikopo ya elimu ya juu hupatikana kupitia tovuti ya Bodi ya Mikopo
- Kwa wanafunzi waliopo vyuoni, kila chuo kina afisa anayesimamia masuala ya mikopo.Ulizia, ofisi yake na atakuhudumia
Wajibu wa mwanafunzi mwenye mkopo akiwa chuoni ni upi?
- Kuwasilisha taarifa zake kwa afisa mikopo (Namba ya usajili na taarifa za benki)
- Kusaini malipo yanayotumwa chuoni kwake ndani ya muda uliopangwa
- Kutoa taarifa kwa afisa mikopo wa chuo chake mapema, kama kuna tatizo lolote linalohusiana na mkopo wake
- Kutembelea tovuti ya HESLB ili kupata taarifa mbalimbali za mikopo ya elimu ya juu