Gharama za Bima ya Afya NHIF kwa Mtu Binafsi ,Gharama za vifurushi hivi hutofautiana kulingana na kipato cha mtu na aina ya huduma zinazotolewa.
Gharama za Bima ya Afya kwa Mtu Binafsi
Kwa mwaka 2025, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeandaa vifurushi mbalimbali vya bima ya afya kwa ajili ya watu binafsi. Vifurushi hivi vinalenga kutoa huduma bora na za uhakika kwa wateja wake kulingana na mahitaji yao. Vifurushi vya bima ya afya vinavyotolewa na NHIF kwa watu binafsi ni pamoja na Ngorongoro Afya na Timiza Afya.
Gharama na Huduma za Kifurushi cha Ngorongoro Afya
Ngorongoro Afya ni kifurushi kinacholenga kutoa huduma muhimu za matibabu kwa gharama nafuu, ikiwa na mpangilio unaofaa kwa watu binafsi na familia. Hiki ni kifurushi kinachowezesha wanachama kufurahia huduma za afya kwa uhakika, hata katika changamoto za kifedha.
Huduma Zinazotolewa kwa Ngorongoro Afya
- Huduma za kumuona daktari: Inajumuisha daktari wa kawaida, bingwa, na bingwa bobezi.
- Vipimo vya kiafya: Vipimo vya maabara, CT-scan, MRI, Ultrasound, X-ray, ECHO, na ECG.
- Huduma za magonjwa yasiyoambukiza: Dawa kwa ajili ya kisukari, shinikizo la juu la damu, selimundu, magonjwa ya moyo, na figo.
- Huduma za kulazwa: Upatikanaji wa wodi ya kawaida na vyumba vya wagonjwa mahututi (ICU na HDU).
- Huduma za uzazi: Kujifungua kwa njia ya kawaida au kwa upasuaji.
- Upasuaji mkubwa na mdogo: Upasuaji wa magonjwa ya tumbo, mifupa, na tezi dume.
- Huduma za kuchuja damu: Peritoneal Dialysis.
- Huduma za saratani: Mionzi tiba na baadhi ya dawa za saratani.
- Huduma za dharura: Matibabu ya haraka katika hali za dharura.
- Huduma za mazoezi tiba na utengamao: Huduma za kuwasaidia wagonjwa kupona baada ya matibabu.
Gharama za Kifurushi cha Ngorongoro Afya
Kifurushi hiki kinapatikana kwa viwango tofauti kulingana na umri wa mchango:
- Miaka 0-17: TZS 240,000 kwa mwaka.
- Miaka 18-35: TZS 432,000 kwa mwaka.
- Miaka 36-59: TZS 540,000 kwa mwaka.
- Miaka 60+: TZS 708,000 kwa mwaka.
Gharama na Huduma za Kifurushi cha Serengeti Afya
Serengeti Afya ni kifurushi cha juu zaidi cha bima ya afya kinachotoa huduma bora na za kina kwa wanachama wanaohitaji uhakika wa huduma za kibingwa na bingwa bobezi.
Huduma Zinazotolewa kwa Serengeti Afya
- Huduma za kumuona daktari: Huduma za daktari wa kawaida, bingwa, na bingwa bobezi.
- Vipimo vya kiafya vya hali ya juu: Vipimo vya maabara, CT-scan, MRI, Ultrasound, X-ray, ECHO, na ECG.
- Huduma za magonjwa yasiyoambukiza: Huduma za kisukari, shinikizo la juu la damu, selimundu, magonjwa ya moyo, na figo.
- Huduma za kulazwa: Upatikanaji wa wodi ya kawaida, ICU, na HDU.
- Huduma za uzazi: Kujifungua kwa njia ya kawaida au upasuaji.
- Upasuaji mkubwa na mdogo: Upasuaji wa magonjwa ya tumbo, mifupa, mishipa ya fahamu, na tezi dume.
- Huduma za kuchuja damu: Huduma za Peritoneal Dialysis.
- Huduma za saratani: Dawa za saratani na tiba ya mionzi.
- Huduma za kinywa na meno: Kung’oa, kuziba, kusafisha, na meno bandia.
- Huduma za vifaa tiba pandikizi: Inajumuisha baadhi ya vifaa tiba maalum vinavyohitajika.
- Huduma za mazoezi tiba na utengamao: Huduma za kuwasaidia wagonjwa kuimarisha viungo vya mwili baada ya matibabu.
- Huduma za dharura: Huduma za matibabu ya haraka na ya dharura kwa wakati wote.
Gharama za Kifurushi cha Serengeti Afya
Serengeti Afya kinapatikana kwa viwango tofauti vya mchango kulingana na umri wa mchango:
- Miaka 0-17: TZS 660,000 kwa mwaka.
- Miaka 18-35: TZS 792,000 kwa mwaka.
- Miaka 36-59: TZS 1,620,000 kwa mwaka.
- Miaka 60+: TZS 3,336,000 kwa mwaka.
Bei na Gharama za Vifurushi
Umri (Miaka) | Kifurushi | Bei (TSh) |
---|---|---|
18 – 35 | Najali Afya Premium | 192,000 |
Wekeza Afya | 384,000 | |
Timiza Afya | 516,000 | |
36 – 59 | Najali Afya Premium | 240,000 |
Wekeza Afya | 444,000 | |
Timiza Afya | 612,000 | |
60+ | Najali Afya Premium | 360,000 |
Wekeza Afya | 660,000 | |
Timiza Afya | 984,000 |
Gharama ya vifurushi hivyo inaongezeka kwa familia kulingana na idadi ya watu wanaounganishwa, mfano mtu binafsi na watoto wanne kwa umri wa miaka 18 hadi 35:
Kifurushi | Bei (TSh) |
---|---|
Najali Afya Premium | 636,000 |
Wekeza Afya | 1,092,000 |
Timiza Afya | 1,548,000 |
Kwa familia yenye watoto wanne na umri wa miaka 36 hadi 59, gharama ya vifurushi vya Timiza Afya ni Sh1,644,000.
Kwa mujibu wa NHIF, vifurushi hivi vimeundwa kwa kuzingatia mahitaji mbalimbali ya wateja, na hivyo kutoa uhuru kwa mtu binafsi kuchagua kifurushi kinachomfaa zaidi kulingana na uwezo wake wa kifedha na mahitaji ya kiafya.