Azam TV inatoa vifurushi mbalimbali vya televisheni Ambavyo ni Vifurushi vya Antena na vya Dishi vinavyokidhi mahitaji tofauti ya wateja nchini Tanzania.Vifurushi hivi unaweza ukalipia kwa siku ,wiki au Mwezi.
Bei Mpya Vifurushi vya Azam 2025 (Vifurushio vya DTH)
Jina la Kifurushi | Bei ya Zamani (TZS) | Bei Mpya (TZS) |
Azam Lite | 10,000 | 12,000 |
Azam Pure | 17,000 | 19,000 |
Azam Plus | 25,000 | 28,000 |
Azam Play | 35,000 | 35,000 |
Azam Lite Weekly | 3,000 | 4,000 |
Azam Pure Weekly | 6,000 | 7,000 |
Bei Mpya Vifurushi vya Azam 2025 vya DTT
Jina la Kifurushi | Bei ya Zamani (TZS) | Bei Mpya (TZS) |
Saadani | 10,000 | 12,000 |
Mikumi | 17,000 | 19,000 |
Ngorongoro | 25,000 | 28,000 |
Serengeti | 35,000 | 35,000 |
Saadani Weekly | 3,000 | 4,000 |
Mikumi Weekly | 6,000 | 7,000 |
Saadani Daily | 500 | 600 |
Mikumi Daily | 1,000 | 1,200 |
Kwa maelezo zaidi kuhusu vifurushi vya Azam TV, unaweza kutembelea tovuti yao rasmi au kuwasiliana na huduma kwa wateja wao.
Jinsi ya Kulipia King’amuzi cha Azam kwa Urahisi
Kuna njia kadhaa za kulipia king’amuzi cha Azam kwa urahisi. Hapa chini ni baadhi ya njia maarufu ambazo unaweza kutumia:
1. Kulipa Kwa Mpesa
- Hatua 1: Ingia kwenye huduma ya M-Pesa kupitia simu yako.
- Hatua 2: Chagua Lipa Bill.
- Hatua 3: Chagua Azam TV kutoka kwenye orodha ya makampuni.
- Hatua 4: Ingiza namba yako ya mteja ya Azam TV.
- Hatua 5: Ingiza kiasi cha kulipa na thibitisha malipo yako.
2. Mixx By YAS
- Hatua 1: Fungua Mixx By YAS kwenye simu yako.
- Hatua 2: Chagua Lipa Bill.
- Hatua 3: Tafuta Azam TV.
- Hatua 4: Ingiza namba yako ya mteja.
- Hatua 5: Ingiza kiasi cha malipo na thibitisha.
3. Airtel Money
- Hatua 1: Fungua Airtel Money kwenye simu yako.
- Hatua 2: Chagua Lipa Bill.
- Hatua 3: Tafuta Azam TV kwenye orodha.
- Hatua 4: Ingiza namba yako ya mteja.
- Hatua 5: Ingiza kiasi cha malipo na thibitisha.
4. Kulipia kwa Kadi ya Benki
- Azam pia inakubali malipo kupitia kadi ya benki. Hii inaweza kufanywa kwa kutumia huduma ya POS au Online Payment kwenye tovuti ya Azam TV. Ingiza maelezo ya kadi yako na thibitisha malipo yako.
5. Mikono ya Azam TV (Azam Shops)
- Unaweza pia kwenda moja kwa moja kwenye ofisi za Azam au maduka yao yaliyopo sehemu mbalimbali ili kulipia huduma ya king’amuzi.
6. Kulipia kwa Mifumo ya Kielektroniki (E-Wallet)
- Azam TV pia inatoa njia za malipo kupitia mifumo ya kielektroniki kama vile PayPal na Visa ikiwa utakuwa unatumia njia hizi.
Hakikisha unakuwa na maelezo sahihi ya akaunti yako ya Azam TV wakati wa kufanya malipo ili kuepuka matatizo yoyote.
Wauzaji wa King’amuzi Cha Azam
Wateja wanaweza kununua king’amuzi cha Azam kutoka kwa mawakala walioidhinishwa kote nchini Tanzania. Baadhi ya maeneo maarufu ni pamoja na:
- Dar es Salaam: Maranatha Electronics (Kariakoo), Kalam General Supplies (Gongo la Mboto), na maeneo mengine mengi.
- Tanga: Abdalhamani Ramadhani Athumani (Lushoto).
- Mwanza: Yahya Mussa Faraji (Nyerere Road), Robbin Star Company LTD (Misungwi).
- Kigoma: Kashindi Mahala Toragu (Munanila, Manyovu), Kahili Bushize Kahili (Kibondo Market).
- Dodoma: Emmanuel Masila Matewa (Bahi Stendi).
- Arusha: Vunja Bei Electronics (Levolosi street), Sunlight Power Supplies (Stand kuu ya Zamani).
- Mikoa Mingine: Azam ina mawakala wengi katika mikoa mingine kama vile Pwani, Kilimanjaro, Morogoro, Mbeya, Mtwara, Iringa, Mara, Kagera, Geita, Katavi, Tabora, Rukwa, Singida, Manyara, Njombe, Ruvuma, Shinyanga, na Simiyu.
Kwa orodha kamili ya mawakala walioidhinishwa, tembelea tovuti rasmi ya Azam TV au wasiliana na huduma kwa wateja kwa maelezo zaidi kupitia tovuti (https://www.azamtv.co.tz/contact-us).