Fangasi ukeni ni moja ya matatizo ya afya ya wanawake ambayo mara nyingi husababisha usumbufu mkubwa, ikiwa ni pamoja na muwasho, kutokwa na uchafu wenye harufu, na maumivu wakati wa kujamiiana. Ingawa kuna matibabu mengi ya kibiashara yanayotolewa kwa ajili ya fangasi ukeni, baadhi ya wanawake wanapendelea kutumia dawa za asili kutibu tatizo hili.
Fangasi Ukeni:
Fangasi ukeni ni muwasho sehemu ya ndani ya uke ambao unaweza kuambatana pia na kuvimba kwa uke. Maambukizi ya fangasi sehemu za siri imekuwa ni tatizo kubwa sana duniani, 75% ya wanawake wote duniani wanaosumbuliwa na tatizo hili wanatafuta dawa ya fangasi ukeni kila siku. Maambukizi haya ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa kwa kiasi kikubwa na fangasi aina ya candida albicans na maambukizi haya pia hujulikana kama vaginal yeast infection au vaginal thrush.
SOMA HII :Madhara ya kufanya mapenzi kipindi cha hedhi Kwa Wanaume Na Wanawake.
Chanzo Cha Fangasi Ukeni:
Chanzo cha fangasi ukeni ni fangasi wajulikanao kwa kitaalamu kama “candida albicans,” ambao kwa kawaida huishi kwenye sehemu za siri bila kusababisha madhara, lakini wanapoongezeka kupita kiasi, husababisha maambukizi hayo. Fangasi ukeni ni maambukizi ya kawaida sana kwa wanawake na yanaweza kumuathiri mwanamke wa umri wowote.
Mambo Yanayoongeza Hatari Ya Kupata Fangasi Ukeni:
Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayomuweka mwanamke katika hatari ya kupata fangasi ukeni;
- Ujauzito.
- Kushuka kwa kinga ya mwili kutokana na kuugua magonjwa mbalimbali kama vile kisukari, UKIMWI.
- Matumizi yaliyokithiri ya dawa hasa zile za kuua bakteria (antibiotics).
- Wanawake wenye umri wa miaka 20-30 wapo katika hatari ya kupata maambukizi haya wakati wale ambao wamekoma hedhi (menopause) na wale ambao hawajaanza kupata hedhi hawako katika hatari kutokana na mazingira au vitu wanavyotumia.
- Matumizi ya mara kwa mara ya vidonge vya majira (oral contraceptive pills).
- Msongo wa mawazo uliokithiri.
- Kujamiiana kwa njia ya kawaida mara tu baada ya kujamiiana kupitia haja kubwa (anal sex).
- Matumizi ya vilainishi wakati wa kujamiiana husababisha maambukizi pia.
- Kuwa na historia ya kupata matibabu ya homoni (hormonal replacement therapy).
- Kuwa na utapiamlo (malnutrition).
- Kuvaa nguo za ndani zisizokauka vizuri na kuvaa mavazi yanayoleta sana joto sehemu za siri.
- Matumizi makubwa ya mipira wakati wa ngono mfano condoms.
Dalili Za Fangasi Ukeni:
Zifuatazo ni baadhi ya dalili za fangasi ukeni ambazo ni pamoja na;
- Kuwashwa sehemu za siri.
- Kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana.
- Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri mara baada ya kutoka kufanya tendo la ndoa au kutoka kukojoa (burning sensation).
- Kuvimba na kuwa mwekundu katika mdomo wa nje ya uke (labia minora).
- Kupata vidonda ukeni (soreness).
- Kupata maumivu wakati wa kukojoa na kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au kijivu unaoweza kuwa mwepesi, mzito au majimaji.
- kutoa harufu mbaya ukeni.
Matibabu Ya Fangasi Ukeni:
Dawa Ya Fangasi Ukeni Ya Vidonge:
Klotrimazole (clotrimazole) ni dawa ya vidonge ya kuua fangasi ukeni (antifungal). Dawa hii ina majina mengi ya kibiashara ikiwemo Cruex, Desenex, Fungoid, Lotrimin, Mycelex, Clotrimazole, Canesten, Clotrimaderm, Myclo, FungiCURE na Candistat. Hupatikana pia kama dawa ya vidonge vya kuweka ukeni (vaginal pessaries).
Jinsi Ya Kutumia Klotrimazole (Vaginal Pessaries) Kutibu Fangasi Ukeni;
Tumia dawa hii wakati unaenda kulala. Hakikisha mikono yako ipo safi, kisha lala chali, panua magoti ukiwa umeyainua. Ingiza dawa ukeni kwa kutumia kifaa chake maalum. Kama haina kifaa maalum, baada ya kuitoa kwenye gamba lake, ingiza kidonge hicho kwenye uke na kisha kisukumize kwa kidole cha kati mpaka kifike mwisho. Baada ya hapo nawa mikono yako. Tumia kwa muda uliolekezwa na daktari.
Madhara Ya Fangasi Ukeni:
Madhara yafuatayo yanaweza kutokea ikiwa mgonjwa mwenye fangasi ukeni atashindwa kupata tiba mapema;
1. Mimba Kuharibika.
Hii hutokea kwa mama mjamzito ambaye hakupata tiba ya maambukizi ya fangasi ukeni mapema ambapo maambukizi hayo huenea sehemu mbalimbali za via vya uzazi na kuharibu mji wa mimba (uterus), sehemu ambapo mimba hujishikiza (fetal implantation) na kupelekea mimba kuharibika kabla ya wakati wake.
2. Kupata Homa Na Kizunguzungu.
Hali hii hutokea kwa sababu ya kubadilika kwa hali ya kawaida ya mwili na kuharibika kwa sehemu mbalimbali za mwili kutokana na maambukizi ya fangasi hali ambayo husababisha kubadilika kwa joto la mwili pia.
3. Kuongezeka Kwa Miwasho Sehemu Za Siri.
Madhara ya fangasi ukeni husababisha kuwepo kwa miwasho kwenye sehemu za siri ambapo mwathirika hujikuna kila wakati, hali hii huongeza uwezekano mkubwa wa kuenea kwa ugonjwa wa fangasi ukeni kwa sababu mwenye maambukizi kama anajikuna na anawagusa wengine wanaomzunguka basi anaweza kusambaza maambukizi hayo kwa wanaomzunguka kwa urahisi.
4. Maumivu Makali Wakati Wa Kukojoa.
Hali hii hutokea kwa mgonjwa Mwenye tatizo la fangasi ukeni, pale ambapo maambukizi yameenea sehemu mbalimbali za via vya uzazi na kusababisha michubuko. Hivyo wakati wa haja ndogo, mgonjwa akikojoa na mkojo ukagusa sehemu ya michubuko maumivu makali hutokea na kusababisha kukosa raha.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA: