Fahamu Namna unaweza Jiunga na Mfumo wa Ajiraportal ili kuweza Ku Apply ajira zinazotangazwa kila siku na Taasisi mbali mbali za kiserikali,Tutakuongoza Hatua kwa hatua Kukamilisha Usajili wako Ajiraportal.
Ajiraportal Ninini?
Ajira Portal ni jukwaa la mtandao lililozinduliwa na Serikali ya Tanzania linalolenga kurahisisha mchakato wa ajira za umma. Ni sehemu ambapo watu wanaweza kupata nafasi za kazi za serikali na kuwasilisha maombi yao kwa njia ya mtandao. Ajira Portal inahusisha taasisi mbalimbali za umma zinazotangaza nafasi za kazi, na pia inasaidia watu kujiandikisha, kusajili, na kufuatilia maendeleo ya maombi yao.
Hii ni portal rasmi ambayo inawaruhusu:
- Waombaji kazi: Kujisajili na kutuma maombi kwa nafasi za kazi zinazotangazwa na serikali.
- Serikali: Kutangaza nafasi za ajira na kuendesha mchakato wa uchaguzi wa watumishi.
- Wahusika katika mchakato wa ajira: Kufuatilia na kusimamia mchakato wa uteuzi, usaili, na ajira za watumishi wa umma.
Jinsi ya Kufungua Account Ajira Portal

Ili kufungua akaunti kwenye Ajira Portal ya Tanzania, tafadhali fuata hatua hizi:
Mahitaji ya Kujisajili kwenye Mfumo wa Ajira Portal
Kabla ya kuanza mchakato wa kujisajili, hakikisha una vitu vifuatavyo:
- Maarifa ya Msingi ya Kompyuta – Utakuwa na urahisi kutumia mfumo huu ukiwa na uelewa wa namna ya kutumia kompyuta.
- Muunganisho wa Mtandao – Hakikisha kompyuta yako, simu janja, au kifaa chochote unachotumia kimeunganishwa na mtandao wa intaneti.
- Vifaa vya Kisasa – Tumia kivinjari kilicho na toleo jipya kama vile Mozilla Firefox, Google Chrome, Safari au Internet Explorer.
- Anwani Halali ya Barua Pepe – Utahitajika kuwa na barua pepe inayofanya kazi ambayo utaweza kufikia.
Nyaraka Zilizohitajika Wakati wa Kujisajili Ajira Portal
Kwa ajili ya kujisajili kwenye Ajira Portal, utahitajika kuwa na nakala za nyaraka zifuatazo zilizothibitishwa na kuhusishwa kwa mfumo wa kielektroniki:
- Cheti cha Kuzaliwa
- Vyeti vya Elimu (Kidato cha Nne/Sita)
- Cheti cha Uhakiki wa NECTA (kwa waliofanya masomo nje ya Tanzania)
- Vyeti vya Taaluma
- Cheti cha Uhakiki wa TCU (kwa waliosomea taaluma nje ya Tanzania)
- Wasifu (CV)
- Picha ya Hivi Karibuni ya Passport Size
- Namba ya NIDA (ikiwa inapatikana)
- Barua ya Maombi
- Leseni ya Taaluma (kwa wale wenye leseni za kitaaluma)
- Cheti cha Usajili wa Taaluma (kwa wataalamu waliosajiliwa rasmi)
- Cheti cha Kufanya Kazi ya Utaalamu (kwa waliohitimu mafunzo ya vitendo)
- Hati ya Mabadiliko ya Jina (kwa walio na majina tofauti kwenye nyaraka zao)
Hatua za Kujisajili kwenye Ajira Portal
Ili kufungua akaunti kwenye Ajira Portal, fuata hatua hizi:
- Tembelea Tovuti Rasmi Ya Ajira Portal: Fungua tovuti ya Ajira Portal kwa kufuata kiungo hiki http://portal.ajira.go.tz.
- Bonyeza Kitufe cha “Register”: Kwenye ukurasa wa mwanzo, utaona sehemu ya kujiandikisha, bofya kwenye kitufe cha “Register”.
- Jaza Taarifa Muhimu: Ingiza barua pepe yako na neno la siri (Password) unalotaka kutumia.
- Thibitisha Barua Pepe: Baada ya kujaza taarifa hizo, utapokea ujumbe kwenye barua pepe yako. Fungua barua pepe hiyo na thibitisha usajili wako.
- Ongeza Maelezo Yako: Baada ya kuthibitisha, ingia tena kwenye akaunti yako mpya na uongeze taarifa zaidi. Hii ni pamoja na:
- Maelezo ya Elimu
- Taarifa Binafsi
- Sifa za Kimwili
- Uzoefu wa Kazi
- Ujuzi Mwingine
- Marejeo ya Kazi
- Mapendeleo yako ya kazi
- Jaza Taarifa kwa Usahihi: Hakikisha umejaza taarifa sahihi ili Sekretarieti ya Ajira iweze kupata maelezo yako kamili kabla ya hatua za ajira.
Namna ya Kutafuta Nafasi za Kazi kwenye Ajira Portal
Baada ya kufanikiwa kujisajili na kuongeza taarifa zako zote, sasa unaweza kuanza kutafuta kazi kwa kufuata hatua hizi:
- Fungua Ukurasa wa Nyumbani wa Ajira Portal: Tembelea tena tovuti ya Ajira Portal.
- Chagua Aina ya Kazi: Angalia kazi zinazopatikana kulingana na taaluma yako au sekta unayotaka kufanya kazi.
- Tuma Maombi: Bofya kwenye nafasi ya kazi unayotaka, kisha tuma maombi yako moja kwa moja kupitia mfumo huu.
SOMA HII : Orodha ya Vyuo Vinavyotoa Kozi Za Hotel Management Tanzania
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQs)
- Kwa nini napata ujumbe “The email address you are trying to register with is not the same as in your HCMIS profile”?
- Hii inamaanisha barua pepe unayotumia haifanani na ile iliyopo kwenye taarifa zako za HCMIS. Tafadhali wasiliana na Afisa Utumishi wako ili afanye marekebisho.
- Nimekosea barua pepe yangu ya usajili, nifanye nini?
- Iwapo barua pepe yako ya usajili ina matatizo, wasiliana na Afisa Utumishi ili kusahihisha barua pepe yako kwenye mfumo wa HCMIS.
- Ninaambiwa “weak password”, nifanye nini?
- Neno la siri linapaswa kuwa na mchanganyiko wa herufi kubwa, ndogo, namba, na alama maalum.