Je wewe n Muathirika wa Punyeto au kujichua kama ambavyo mtindo huu umepewa majina mengi kama Vile Kujichukulia sheria mkononi ,kukwea mnazi na adharika tumekuandalia makala hii itakayokusaidia kuweza kuushinda huu mchezo na kuacha punyeto.
KUJICHUA NI NINI HASA?
Kwa Kiingereza tendo hili linaitwa Masterburtion‘’ likiwa na maana ya kupiga punyeto. Hapa nimetumia kwa ulaini kabisa; kujichua. Lugha nyepesi na rahisi kufikika kwa wengi ni kujiridhisha! Ni kitendo cha mtu kujichezea kimahaba huku akivuta hisia za mapenzi kwa mtu ambaye yupo mbali naye hadi anapomaliza haja zake.
Namna ya ufanywaji inategemea zaidi na jinsi ya mazoea. Wapo wanaotumia vifaa bandia (artificial) na wengine vifaa halisi kama aina mbalimbali za matunda ambazo zinafanana na sehemu pacha!
Wengine wanatumia njia wanazojua wenyewe, lakini wanaume wengi wanatumia sabuni lengo hapa ni moja tu, unatakiwa kufahamu kwamba namaanisha kujiridhisha.
INAWEZEKANAJE KUJIRIDHISHA?
Ni rahisi sana kumaliza tendo la huba kwa kujifanyisha mwenyewe. Silaha kubwa inayotumiwa na waathirika ni kuwavutia hisia watu wa jinsi pacha wakati tendo husika likiendelea kufanyika.
Habari mbaya kwa watu wenye mchezo huu ni kwamba, kwanza wakishaanza, inakuwa vigumu sana kuacha. Inashindikana kwa sababu ni jambo la aibu. Si rahisi kupata ushauri kutoka kwa watu maana ni aibu pia kumweleza rafiki yako juu ya mchezo huo.
Kutokana na hilo sasa, kinachotokea ni kwamba ‘waumini’ wa mchezo huu wanaendelea kuwa watumwa kwa maisha yao yote. Hapa chini tutaona kwa undani jinsi tatizo hili linavyoumiza vichwa vya wengi.
Ni kweli hutaki kuwa mtumwa wa mchezo huu hatari? Zipo athari nyingi sana rafiki yangu ambazo nitazieleza hapa chini.
CHANZO NI NINI HASA?
Jambo la kushangaza ni kwamba, hakuna mdau wa mchezo huo ambaye amefundishwa jinsi unavyofanywa. Wengi wameanza wenyewe, tena wengine bila kujua nini kitakachotokea, lakini baada ya matokeo kuonekana, ndiyo mwanzo wa kutopea huko.
Kwa vijana wa kiume, wengi huanza tabia hii wakiwa kwenye umri wa kubalehe. Mara nyingi hutokea asubuhi wakati wa kuamka, usiku wakati wa kulala au bafuni wakati wa kuoga.
Kwa kawaida, mtu anapokuwa katika sehemu ya utulivu kwa maana ya kupumzika, wakati mwingine mkono unaweza kutembea huku na huko kwenye mwili na mwisho wake bila kutegemea mhusika anajikuta ameshaingia kwenye mchezo huo.
Huwa kama mzaha, akiwa hajui hatma yake, lakini msisimko anaoupata ndiyo unaomchanganya na mwisho wake anashangaa kila kitu kimemalizika. Unajua atakachosema? Sikia: “Mh! Kumbe ndiyo mwisho wake ni hivi? Lakini kama nimesikia starehe hivi…”
Hiyo hutokea pia wakati wa kuoga, ambapo wakati wa kujisugua kwa dodoki, msisimko ukitokea, madhara yanakuwa kama nilivyoeleza hapo juu.
Wenye umri mkubwa au wa kati, huanza tabia hii hasa baada ya kuanza mchezo wa kuangalia video za kikubwa wakiwa peke yao. Kwa sababu wanachotazama kinahusisha msisimko wa mapenzi, basi bila kutarajia hujikuta tayari!
Hii inafanana pia na kwa watoto wa kike, vyanzo nilivyoeleza hapo juu pia husababisha kwa karibu sana.
Sababu nyingine ni kunyimwa au kutotoshelezwa kimahaba na mwenzake.Wengi imewagusa, lakini kuna makundi mawili; wapo waathirika ambao wanatamani kuachana na utumwa huu na wengine wameathirika zaidi, kiasi kwamba hawana mpango wa kuacha.
Wengine wameenda mbali zaidi, kwa vile hawafikirii kuachana na mchezo huu, wamefikia hatua wanasema kwamba hakuna madhara kwa mtu anayejichua! Watu wanatetea wazi wazi, kwamba kujichua hakuna madhara. Sikia rafiki yangu, hata anayevuta sigara anajua kwamba ina madhara kwa afya yake, lakini ili kujifariji, atajenga hoja kwamba, haimdhuru na badala yake inamsaidia sana kuondoa baridi na haina kilevi.
Wakati mvuta sigara akisema hivyo, mlevi naye atakuja na hoja kwamba, pombe inamsaidia sana kupunguza mawazo. Kila mmoja atatetea upande wake. Ni jambo la kawaida kabisa.
Nikiwa naelekea kuendelea na mada yetu, rafiki yangu mpendwa kama wewe ni ‘muumini’ wa tabia hiyo, unatakiwa kufahamu kwamba unafanya jambo HATARI sana, si tu kwa afya yako, kisaikolojia na dhambi ya uzinifu ambayo hiyo itatokana na uhusiano wako mwema na imani ya dini yako, NDOA yako ipo/itakuwa hatarini.
Nadhani mnakumbuka wiki iliyopita nilieleza maana ya kujichua, namna tendo linavyofanyika na jinsi mtu anavyoanza mchezo huo bila kutegemea. Sasa rafiki, hebu tuendelee kwenye namna tatizo linavyokua.
Kuelewa Madhara ya Punyeto
Kabla ya kujua jinsi ya kuacha punyeto, ni muhimu kuelewa madhara yanayoweza kutokea:
1. Huzuni na Hofu: Watu wanaopiga punyeto mara kwa mara wanaweza kuhisi huzuni au hofu. Hali hii ni mara nyingi kutokana na hisia za hatia au aibu kuhusu tabia zao. Huzuni na hofu hizi zinaweza kusababisha upungufu wa furaha na kuathiri hali ya kiakili ya mtu.
2. Kujitenga na Jamii: Mara nyingine, mtu anaweza kujitenga na shughuli za kijamii au jamii kwa ujumla kwa sababu ya hofu ya kushikwa na wengine au kufichwa kwa tabia hii. Kujitenga hii kunaweza kuongeza hali ya upweke na kuongeza mzigo wa kihisia.
3. Uchovu: Punyeto ya mara kwa mara inaweza kusababisha uchovu wa kimwili na kihisia, hasa ikiwa inafanyika kwa kiwango kikubwa au kwa mfululizo bila mapumziko. Uchovu huu unaweza kuathiri uwezo wa mtu katika shughuli za kila siku.
4. Hali ya Kujiamini: Kwa baadhi ya watu, punyeto ya mara kwa mara inaweza kusababisha hali ya chini ya kujiamini. Tabia hii inaweza kuathiri jinsi mtu anavyojiona mwenyewe na uwezo wake wa kujenga uhusiano mzuri na wengine.
5. Mabadiliko ya Matumizi ya Kijinsia: Kwa baadhi ya watu, punyeto inaweza kuathiri jinsi wanavyopata furaha na ushirikiano wa kijinsia na wenza wao. Mabadiliko haya yanaweza kusababisha matatizo katika mahusiano ya kijinsia.
6. Matatizo ya Afya: Kwa watu wengine, punyeto ya mara kwa mara inaweza kusababisha matatizo ya afya kama vile maumivu ya chini ya tumbo, maumivu ya sehemu za siri, au hata tatizo la kawaida la harufu mbaya inayotokana na usafi wa mwili.
UNATAKA KUACHA?
Hakuwa dawa kubwa sana ya kuacha mchezo huu. Najua wengi walikuwa na hamu ya kutaka kusikia, wataachaje huu mchezo. Ndugu zangu.Usitarajie kwamba nitakuja kuingia kwenye nafsi yako na kukuambia ACHA KUJICHUA! Mimi nitakusaidia kuondoa athari za kujichua kama uume kuregea kutokana na kudhoofika kwa mishipa katika uume na kurejesha heshima yako ya familia. Ndugu zangu, nitawapa dondoo chache sana, lakini kubwa ni kwamba ATHARI nilizotaja hapo juu zinatosha kabisa kukubadilisha!
Hebu nikuulize, utakuwa na hamu ya kuendelea na haya mambo kama ndoa yako itakuwa hatarini? Nani atakubali kufedheheka? Nani atakubali kupoteza heshima yake? Bila shaka hakuna. Pitia dondoo zifuatazo;
(i) Badilisha utaratibu wa kulala, lala kifudifudi, badala ya chali (rejea maelezo yangu ya awali kuhusu chanzo cha tatizo)
(ii) Acha kuangalia mikanda ya kikubwa ukiwa peke yako.
(iii) Kaa mbali na simulizi zinazohamasisha mapenzi, mazungumzo ya aina hiyo na kampani za watu wanaopenda kusimulia mambo ya faragha.
(iv) Acha mazoea ya kujishika sehemu zako za siri.
(v) Fanya mazoezi ya viungo angalau robo saa tu kwa siku.
(vi) Juu ya yote haya, FUTA kabisa mawazo ya jambo hilo. AMUA kwa dhati ya moyo wako, tambua na ogopa athari ambazo unaweza kuzipata, kisha ACHA KABISA mchezo huo ili kulinda heshima yako na kujipa furaha ya maisha
Njia za Kusaidia Kuacha Punyeto kwa Wanawake
Wanawake wanaweza kutumia mbinu hizi maalum:
1. Kushiriki katika Tiba ya Mhemko: Wanawake wanaweza kupata faida kubwa kwa kushiriki katika tiba ya mhemko ili kujifunza jinsi ya kudhibiti tamaa zao na kuboresha hali yao ya kihisia. Tiba ya mhemko inaweza kusaidia kwa kutoa mbinu za kuzingatia na kudhibiti hisia.
2. Kutumia Mazoezi ya Kimsingi: Mazoezi ya kimsingi kama vile yoga au meditation yanaweza kusaidia kupunguza tamaa na kuimarisha hali ya kihisia. Mazoezi haya yanaweza kupunguza msongo wa mawazo na kuongeza hisia za utulivu.
3. Kujenga Mahusiano: Kujenga mahusiano yenye afya na kukutana na watu wapya kunaweza kusaidia kupunguza hali ya upweke na tamaa ya punyeto. Mahusiano haya yanaweza kuimarisha hali ya kijamii na kutoa msaada wa kihisia.
4. Kujitolea kwa Jamii: Kushiriki katika shughuli za kujitolea kunaweza kutoa hisia ya kuwa na thamani na kupunguza tamaa ya punyeto. Kujitolea kunaweza kusaidia kujenga hisia ya malengo na kuimarisha mtazamo wa maisha.