Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni chama kikongwe na kikubwa zaidi cha siasa nchini Tanzania, kikiwa na historia ndefu ya kushiriki katika uongozi wa nchi na maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi. Ili kuwa mwanachama halali wa CCM, ni muhimu kuwa na kadi ya uanachama na kuhakikisha michango ya kila mwaka imelipwa. Sasa, kwa urahisi zaidi, chama kimerahisisha mfumo wa malipo ya kadi kwa kutumia simu za mkononi kupitia mitandao kama Airtel Money, M-Pesa, Tigo Pesa, T-Pesa na hata kupitia benki kama CRDB.
Sifa za Kuwa Mwanachama wa CCM
Ili kuwa mwanachama wa CCM, mtu anatakiwa kutimiza masharti yafuatayo:
Raia wa Tanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea.
Kukubali itikadi, sera, na katiba ya CCM.
Awe tayari kushiriki shughuli za chama na kuchangia maendeleo ya jamii.
Asiwe mwanachama wa chama kingine cha siasa.
Awe tayari kulipa ada na michango mbalimbali ya chama kwa mujibu wa katiba.
Jinsi ya Kupata Kadi ya Uanachama wa CCM
Kadi ya CCM hutolewa kwa mwanachama mpya kupitia taratibu rasmi za chama. Hatua za kufuata ni:
Tembelea Ofisi ya CCM ya Tawi, Kata au Wilaya iliyo karibu nawe.
Jaza fomu ya maombi ya uanachama.
Toa nakala ya kitambulisho cha uraia (NIDA) au nyaraka nyingine zinazotambulika.
Lipia ada ya usajili (huwa ni kiasi kidogo cha fedha).
Subiri kupata kadi ya muda, kisha baada ya mchakato kukamilika, utapewa kadi rasmi ya plastiki yenye jina na namba ya uanachama.
Jinsi ya Kulipia Kadi ya CCM kwa Airtel Money
1 Piga *150*60#
2 Chagua 1 ‘Tuma Pesa’
3 Chagua 4 ‘Tuma Kwenda Benki’
4 Chagua 2 ‘CRDB’
4 Chagua 2 ‘Lipa kwa Namba ya Malipo’
4 Ingiza namba ya Kumbukumbu
5 Weka namba yako ya kielektroniki
6.Thibitisha malipo kwa PIN yako ya Airtel Money.
- 7.Utapokea ujumbe wa kuthibitisha malipo.
Jinsi ya Kulipia Kadi ya CCM kwa M-Pesa
1 Piga *150*00#
2 Chagua 6 ‘Huduma za kifedha’
3 Chagua 2 ‘Mpesa kwenda Benki’
4 Chagua 1 ‘Kwenda CRDB’
5 Chagua 2 ‘Weka Control Number’
6 Ingiza namba yako ya Kielektroniki
Mfano: C0000000102301
Jinsi ya Kulipia Kadi ya CCM kwa Tigo Pesa au Mix by Tigo/Yas
1 Piga *150*01#
2 Chagua 4 ‘Lipa Bili’
3 Chagua 3 ‘Ingiza Namba ya kampuni’
4 Namba ya Kampuni ni 900600
6 Weka Kumbukumbu Namba [Namba yako ya kielektroniki
Mfano: C0000000102301 ]7 Ingiza kiasi cha malipo (k.m. TZS 2,000).
Weka namba yako ya siri ya Tigo Pesa.
9. Malipo yatakamilika na utapokea ujumbe wa uthibitisho.
Watumiaji wa Mix by Tigo/Yas wanaweza kutumia Tigo Pesa ndani ya app au menyu hiyo hiyo ya USSD.
Jinsi ya Kulipia Kadi ya CCM kwa T-Pesa (TTCL)
1 Piga *150*71#
2 Chagua 5 ‘Huduma za kifedha’
3 Chagua 1 ‘TTCL Kwenda Benki’
4 Chagua 2 ‘Orodha ya Benki’
5 Chagua 2 ‘CRDB’
6 Ingiza namba ya malipo
Mfano: C00000001023017 Weka kiasi
8 Weka namba ya Siri
Thibitisha malipo kwa kuweka PIN ya T-Pesa.
- Utaona ujumbe wa mafanikio.
Soma Hii : Jinsi ya kujiunga na Kulipia Mange Kimambi App (Android & ios /Iphone)
Jinsi ya Kulipia Kadi ya CCM kwa CRDB (SimBanking/Matawi)
Kupitia SimBanking App:
1 Malipo
2 Malipo Zaidi
3 CCM Payment
4 Ingiza Namba ya Malipo
Mfano: C00000001023015 Pata Taarifa
6 Weka Kiasi
7 Endelea
8 Thibitisha
Kupitia Tawi la CRDB:
Tembelea tawi la CRDB karibu nawe.
Mwambie afisa benki kuwa unataka kulipa ada ya uanachama wa CCM.
Toa namba ya uanachama au jina lako.
Lipia kiasi kinachotakiwa.
Hifadhi stakabadhi ya malipo kwa kumbukumbu.