Kufunga dishi la Azam TV nyumbani si jambo la kutisha kama unavyoelezwa mara nyingi. Kwa uelewa wa msingi, vifaa sahihi na uvumilivu kidogo, unaweza kulifanikisha mwenyewe na kuokoa gharama ya fundi.
Vifaa Unavyohitaji
Kabla hujaanza, hakikisha unayo:
Dish la satellite (Azam au lolote linalolingana)
LNB (Low Noise Block converter)
Decoder ya Azam TV
Cable ya coaxial (inayounganisha dish na decoder)
Kompas au app ya “Satellite Finder” kwenye simu
TV yenye HDMI au AV
Spanner au kifaa cha kufunga bolts
Screwdriver
Hatua kwa Hatua za Kufunga Dish la Azam TV
1. Tafuta eneo sahihi la kufunga dish
Hakikisha dish linaelekezwa mashariki kidogo (Azam inatumia satellite ya Eutelsat 7A/7B).
Hakuna vizuizi kama miti, paa au kuta kwenye mwelekeo huo.
2. Funga dish kwenye ukuta au nguzo
Tumia bolts kuhakikisha umelifunga imara kabisa.
Dish liwe kwenye usawa mzuri, lisiyumbe kwa upepo.
3. Weka na rekebisha LNB
LNB iwekwe kwenye mkono wa dish na ilenge katikati.
Tumia cable ya coaxial kuunganisha LNB hadi kwenye decoder kupitia “LNB IN”.
4. Washa TV na Decoder
Unganisha decoder ya Azam kwenye TV kwa kutumia HDMI au AV.
Weka TV kwenye mode sahihi (HDMI au AV kulingana na ulivyoiunganisha).
5. Ingia kwenye “Signal Status” kwenye menyu ya decoder
Nenda Menu > Installation > Signal Status.
Hapo utaona “Signal Strength” na “Signal Quality”.
6. Anza kurekebisha dish hadi upate signal nzuri
Polepole geuza dish kushoto/kulia (horizontally) huku ukitazama kwenye TV signal inavyobadilika.
Ukiona signal imeanza kuonekana (angalau 50%-70%), fungia bolts za dish.
Sasa rekebisha dish juu/chini (vertically) hadi uone “Signal Quality” inafika juu zaidi.
Kidokezo: Unaweza kutumia mtu mwingine asimame kwenye TV huku wewe uko nje – atakuambia unapopata signal nzuri.
7. Fanya “Channel Search”
Nenda kwenye Menu > Installation > Auto Scan au “Blind Scan”.
Subiri decoder ijaze chaneli zote za Azam TV.
8. Hakikisha Chaneli Zinafunguka Vizuri
Baada ya kuchunguza list ya chaneli, angalia baadhi kufahamu kama zinafunguka bila tatizo.
Chaneli kama Azam Sports HD, Sinema Zetu, Sinema Swahili, na Azam Two ndizo za kuanza nazo.
Vidokezo vya Ziadi kwa Mafanikio
Hakikisha cable haina mikato wala kutu.
Usifunge dish kwenye paa la bati bila ulinzi – upepo unaweza kuliburuta.
App ya “Satellite Pointer” au “Dish Align” inaweza kusaidia kuelekeza sahihi.
Signal nzuri ni kati ya 60% – 90% ya quality.
Msaada wa Video Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kufunga Dish la Azam mwenyewe kuokoa Gharama
Video Credit: Youtube DMG info 2