Tumbaku ni mojawapo ya mazao ya biashara muhimu yanayochangia pato la taifa nchini Tanzania. Zaidi ya hapo, tumbaku ni chanzo kikuu cha ajira kwa maelfu ya wakulima wa vijijini na huchangia kwa kiasi kikubwa katika mapato ya kigeni kupitia mauzo ya nje. Tanzania ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa tumbaku barani Afrika, huku uzalishaji wake ukiwa wa kiwango cha juu, hasa aina ya Flue-Cured Virginia (FCV).
Aina za Tumbaku Zinalimwa Tanzania
Kabla ya kuangazia mikoa inayolima tumbaku, ni muhimu kufahamu kuwa kuna aina kuu mbili za tumbaku zinazolimwa nchini:
Flue-Cured Virginia (FCV) – Hii ndiyo aina maarufu zaidi na hutumika kutengeneza sigara. Inahitaji maandalizi mazuri ya shamba na michakato maalum ya kukausha.
Dark Fire-Cured – Aina hii inatumika zaidi katika kutengeneza tumbaku ya kunusa au kutafuna.
Historia ya Uzalishaji wa Tumbaku Nchini Tanzania
Uzalishaji wa tumbaku nchini Tanzania ulianza rasmi mwaka 1930, wakati ambapo zao hili lililetwa kutoka Nyasaland (sasa Malawi) hadi Songea. Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, uzalishaji wa tumbaku ulienea katika maeneo mengine kama vile Urambo katika Mkoa wa Tabora. Kwa sasa, tumbaku inalimiwa katika mikoa 13 nchini, ikiwa ni pamoja na:
- Tabora (Urambo, Tabora Municipal)
- Katavi (Tanganyika, Mlele)
- Shinyanga (Kahama)
- Geita (Chato)
- Kagera (Biharamulo)
- Kigoma (Uvinza)
- Iringa (Iringa Municipal)
- Singida (Manyoni)
- Mbeya (Chunya)
- Ruvuma (Songea Rural)
- Songwe
- Mara
- Morogoro (Kilosa)
Mikoa hii inajulikana kwa uzalishaji mkubwa wa tumbaku na inategemea sana wakulima wadogo ambao hutumia mbinu za jadi na kisasa katika kilimo chao.
Soma Hii:Simu za infinix na bei zake (aina za simu za infinix)
Fursa za Kilimo cha Tumbaku Tanzania
Soko la ndani na la nje: Tumbaku ya Tanzania inauzwa ndani na nje ya nchi, hasa Ulaya na Asia.
Ajira kwa vijana na wanawake: Kilimo cha tumbaku kinatoa ajira nyingi vijijini.
Ushirikiano na makampuni binafsi: Makampuni yanatoa mbegu, mafunzo, na mikopo ya pembejeo.
Uwekezaji katika viwanda vya kuchakata tumbaku: Hii ni fursa kwa sekta binafsi kuongeza thamani ya zao kabla ya kuuza.
Changamoto Zinazokabili Wakulima wa Tumbaku
Mabadiliko ya hali ya hewa huathiri uzalishaji.
Mabadiliko ya sera za kimataifa dhidi ya matumizi ya tumbaku.
Bei kutopangwa na wakulima — wanategemea wanunuzi wakuu.
Matumizi ya nguvu kazi ya watoto ambayo hayaruhusiwi kisheria.