Dawa za Kutoa Mimba na za Kusafisha Baada ya Kutoa Mimba

Dawa za Kutoa Mimba na za Kusafisha Baada ya Kutoa Mimba
Dawa za Kutoa Mimba na za Kusafisha Baada ya Kutoa Mimba

Zipo Njia nyingi za Utoaji wa Mimba changa ,za mwezi ,miezi miwili ,mitatu au zaidi ambazo  za asili na za kisasa Makala hii Inajadili Jinsi ya Kutoa mimba kwa kutumia Vidonge na kusafisha.

Vifahamu Vidonge vya kutoa Mimba na Vya kusafisha baada ya kutoa

Mifepristone na Misoprostol ni nini? Mifepristone, pia inajulikana kwa jina la chapa RU-486, ni steroid sintetiki inayofanya kazi kama kinza projestojeni. Kwa kuzuia progesterone ya homoni, mifepristone inaleta mabadiliko katika endometriamu na laini ya kizazi, ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya ujauzito.

Jinsi ya Kutumia mifepristoni na misoprosto Kutoa Mimba

Jinsi ya Kutumia mifepristoni na misoprosto Kutoa Mimba

Kama utoaji mimba haujakamilika baada ya kutumia dozi
3, unaweza kutumia vidonge 4 tena kwa utaratibu uleule,
angalau saa 3 baada ya dozi ya tatu. Kwa taarifa kama
utoaji mimba umekamilika, Kama hakuna utokaji damu baada ya dozi hizo 3, tafuta
vidonge vingine kutoka chanzo kingine na kuanza upya.

SOMA HII KUTOKA BBC : Mifepristone: Vidonge vya uavyaji mimba ni salama kiasi gani?

Kutumia mifepristoni na misoprosto
Katika zoezi hili, unameza mifepristoni,
unasubiri masaa 24 hadi 48, halafu unatumia
misoprosto.
Kwa mimba za chini ya wiki 12
Meza mg 200 za mifepristoni na subiri masaa 24 hadi
48. Baada ya hapo ruhusu vidonge 4 vya misoprosto
kuyeyuka aidha chini ya ulimi au kati ya shavu lako
la ndani na fizi, kwa dakika 30. Meza kitakachokua
kimebaki mdomoni na maji.
Kama unadhani zoezi la utoaji mimba haliendelee au
halijafanikiwaI, tumia vidonge 4 tena vya misoprosto kwa
njia ile angalau saa 3 baadae. Kwa taarifa ya kujua kama
utoaji mimba umekamilika,

Utoaji mimba kwa vidonge
Utoaji mimba kwa vidonge,kwa mimba za wiki 13 ni niia
yenye gharama nafuu Zaidi. Inaweza kufanyika kwa
usalamanyumbani, na ni rahisi kupatikana kuliko njia
zingine sehemu utoaji mimba hauruhusiwi.
Misoprosto ni dawa ya kawaida ambayo inaweza kutoa
mimba kwa usalama na ufanisi, katika hali inayofanana
na mimba ilioharibika. Inaweza kutumika peke yake,
na hufanya kazi vizuri zaidi inapotumika pamoja na
mifepristoni. Misoprosto pia hutumika kutibu vidonda
vya tumbo, na huuzwa kwenye maduka ya dawa katika
nchi nyingi. Mifepristoni ni kwa ajili ya utoaji mimba tu,
haipatikani sehemu zote.

SOMA HII :  Jinsi Ya Kumtongoza (Kumshawishi) Mwanamke Chini Ya Dakika 2

Kama utafuta msaada wa kitabibu

Dalili za maumivu na damu kutoka baada ya utoaji
mimba ni kama zile za kawaida mimba inapoharibika.
Hakuna anayeweza kujua ulitumia vidonge kuitoa
isipokuwa kama mabaki yatagundulika ukeni au
ukiwambia mwenyewe.
Kama unaweza, mtafute mtu wa kukusindikiza kwa
msaada zaidi.

Kutumia misoprosto peke yake

Kwa mimba za wiki 13 au chini, unahitaji kutumia
vidonge vya misoprosto 4 vya mcg 200 kila kimoja, kila
baada ya masaa 3 hadi utoaji mimba utakapokamilika.
Kwa mfano, kama utatumia vidonge 4 vya kwanza saa
12 asubuhi, tumia vidonge vingine 4 saa 3, na vidonge
vingine 4 saa 6 mchana. Watu wengi huhitaji kutumia
angalau vidonge 12 kukamilisha utoaji mimba. Baadhi ya
watu huhitaji zaidi.
Vidonge vya Misoprosto havimezwi kama dawa zingine.
Vidonge vinapaswa kuyeyuka kwa dakika 30 taratibu,
aidha chini ya ulimi au kati ya shavu la ndani na fizi.
Mahali utoaji mimba unaruhusiwa, vidonge vinaweza
kuingizwa ndani kabisa ukeni kwa dakika 30. Kawaida
Vidonge haviyeyuki kabisa ukeni na daktari anaweza
kuona masalia utakapokwenda kutafuta msaada wa
kitabibu.

Kama utaamua kuitoa mimba, unaweza kusimama
imara juu ya uamuzi wako. Utoaji mimba kwa vidonge ni
salama na njia hii hutumiwa na:
• watu wenye umri wote
• watu wanaonyonyesha
• watu wenye uzito tofauti
• watu ambao wamewahi kuzaa watoto
• watu ambao hawajawahi kuzaa
• watu wenye VVU
• watu wanaotumia homoni kama vile testosterone
Utoaji mimba salama hausababishi ugonjwa wowote,
wala madhara kwa mimba za baadaye au kwa mwili
wako.
Uamuzi wa kutoa mimba ni uamuzi binafsi mno.
Ni wewe tu anayeweza kuamua lipi sahihi katika hali
yako. Amini kwamba utafanya uamuzi sahihi na kujitahidi
kuufanya uamuzi huo kuwa salama.

SOMA HII :  Mambo Ambayo Wanaume Hawayapendi kutoka kwa Wake zao

Utoaji mimba kwa vidonge-hadi mimba za wiki 13

Watu duniani kote hutoa mimba.
Utoaji mimba unaweza kufanyika
kwa usalama kabisa. Hatari
inayoambatana kawaida ni kidogo
ukilinganisha na hali ya ujauzito na
matukio ya kujifungua.
Kuelewa jinsi ya kutumia vidonge
hivi na utarajie nini kunaweza
kukusaidia kufanya uamuzi wa
busara na kupita katika zoezi hili
vizuri.

Jiandae kwa ajili ya utoaji mimba

• kuwa na mtu unayemuamini.
• pata msaada kutoka kwa mtu mzoefu juu ya utoaji
mimba.
• tafuta mtu wa kukusaidia na shughuli au majukumu
ya nyumbani, kwani zoezi linaweza kuchukua masaa
48.
• panga namna utakavyondoa kwa usalama ujauzito
utakaotolewa.
Kuwa na vifuatavyo karibu:
• simu ya mkononi yenye salio la chaja
• fedha taslimu kwa ajili ya vidonge zaidi kama
vitahitajika, au dharura
• dozi kamili ya misoprosto (vidonge 12 vya mcg 200 kila
kimoja)
• padi 10 au zaidi kwa ajili ya utokaji damu
• ibuprofeni, naproxen, au diklofenaki kwa ajili ya
maumivu
• kipimajoto

Wakati wa utoaji mimba—Tarajia
• Damu kutoka na mkakamao tumboni. Tumia dawa za
kupunguza maumivu kama ibuprofeni au chupa ya
maji ya moto kupunguza maumivu tumboni.
• Kutoa damu ilioganda na tishu, hali ambayo hutoweka
ndani ya saa 6 hadi 15 baada ya dozi ya kwanza ya
misoprosto lakini huweza kuendelea siku kadhaa.
• Kichefuchefu, kutapika, kuharisha, baridi, na homa
(chini ya 38°C/100.4°F). Hii ni kawaida.
• Angalia dalili za tahadhari (uk. 10).
Baada ya mimba kutoka
• Kwa siku 7, epuka shughuli ngumu.
• Kwa siku 5, epuka ngono na usingize chochote ukeni
(sabuni, vitambaa nk).
• Kula vyakula vyenye afya.
• Anza uzazi wa mpango. Unaweza kupata mimba mara
baada ya kutoa mimba Angalia https://bit.ly/swFPweb
• Ongea na mtu unayemuamini, au watoa huduma
husika kwa ajili ya msaada wa kisaikolojia.
• Dalili za mimba hasa kichefuchefu huondoka ndani
ya siku chache. Kuthibitisha, pata kipimo cha17
ultrasound baada ya wiki 2, au kipimo cha mimba cha
nyumbani baada ya wiki 4.

SOMA HII :  Maswali ya Kumuuliza Mwanamke Anayekupenda

Dalili za hatari Wakati wa Utoaji Mimba

Kama una dalili zifuatazo, tafuta msaada wa kitabibu
haraka.
Kutokwa damu nyingi ikiwa na mabonge
• kulowesha zaidi ya padi au vitambaa 2 ndani ya saa
2 mfululizo
• mabonge ya damu yanazidi ngumi yako
• kujisikia kizunguzungu au kupepesuka
Homa kali (zaidi za 38°C/100.4°F) kama:
• huanza zaidi ya saa 24 baada ya kutumia misoprosto
Maumivu makali tumboni, hata baada ya kutumia
ibuprofeni au dawa nyingine ya maumivu
Kutokwa maji yenye harufu mbaya ukeni

Nani hapaswi kutumia vidonge vya utoaji mimba

Utoaji mimba kwa vidonge hauruhusiwi kama:
• umekuwa na maumivu na kutokwa na damu wakati
waujauzito huu.
• una ugonjwa wa moyo, anemia kali, hemophilia, au
tatizo sugu la matezi ya adrenali.
• una mzio na dawa ya mifepristoni au misoprosto.
• unatumia dawa za kulainisha damu isigande.
• umefungwa kitanzi (IUD) kwenye kizazi chako.
Kama una tatizo lolote kama hayo, utoaji mimba kwa
vidonge huenda usifanikiwi au unaweza kukusababishia
matatizo mengine makubwa ya kiafya. Ongea na
mfanyakazi wa afya au mtu mweledi mzoefu juu ya njia
zingine za utoaji mimba salama.
Kwa mimba za zaidi ya wiki 13, tafuta msaada
Kama mimba imekua kiasi hiki, dozi za misoprosto
zinakuwa ndogo, hutolewa mara kadhaa, na utokaji mimba
huchukua muda mrefu zaidi. Tafuta ushauri na msaada
kutoka kwa mkunga, mfanyakazi wa afya mwingine au mtu
mwenye uzoefu kuhakikisha unakuwa salama na kujisikia
vizuri kadri itakavyowezekana.

Onyo Kali: Utoaji wa mimba kiholela ni kosa kiimani na kisheria za nchi Mimba pekee ambazo zinaruhusiwa kutolewa ni zie zilizopata kibali cha Daktari kwamba zinaweza kuhatarisha uhai wa mama kama Vile zilizojitunga nje ya Mfuko wa Uzazi.

About Burhoney 4806 Articles
Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati