AzamTV Max ni huduma ya kidigitali inayokupa fursa ya kutazama chaneli mbalimbali za AzamTV moja kwa moja kupitia simu janja, tablet, au kompyuta. Ikiwa unapenda burudani, michezo, habari, na vipindi vya Kiswahili, basi AzamTV Max ni chaguo bora kwako. Katika makala hii, tutaelezea hatua kwa hatua jinsi ya kupakua na kujisajili kutumia AzamTV Max.
Hatua za Kupakua AzamTV Max
Ili kuanza kutumia AzamTV Max, unahitaji kupakua programu kwenye kifaa chako cha mkononi au kompyuta. Fuata hatua hizi:
1. Kwa Watumiaji wa Android:
- Fungua Google Play Store kwenye simu yako.
- Tafuta “AzamTV Max” kwenye sehemu ya utafutaji.
- Bonyeza kitufe cha “Install” ili kuanza kupakua na kusakinisha programu.
2. Kwa Watumiaji wa iOS (iPhone/iPad):
- Fungua App Store kwenye kifaa chako.
- Tafuta “AzamTV Max” kisha bonyeza “Download” au “Get”.
- Subiri hadi programu ikamilishe kusakinishwa.
3. Kwa Watumiaji wa Kompyuta:
- Tembelea tovuti rasmi ya AzamTV kupitia www.azamtvmax.com
- Jisajili au ingia kwa akaunti yako ili kuanza kutazama.
Jinsi ya Kujisajili kwenye Azam Max
Mara baada ya kupakua na kuinstall App ya AzamTv Max sasa hatua inayofuata ni kujisajili kwenye App ili uanza kugurahia maudhui ya vipindi vinavyorushwa na channel za Azam Tv
Ili kujisajili kwa mtumiaji wa mara ya kwanza fuata hatua hizi hapa chini
1. Nenda kwenye simu yako na ufungue App ya AzamTV Max
2. Kisha itakutaka ujaze tarifa fuata maelekezo
3. Ingiza namba ya kisimbuzi chako ili kuunganisha kisimbuzi chako na App yako
4. Kumbuka wakati wa kujisajili utahitaji namba ya simu au email
5. Tengeneza neno siri ambalo utalikumbuka kwa urahisi
6. Hifadhi neno siri na namba ya simu au email uliyotumia kujisajili kwani vitatumika kama login details hapo baadae
7. Ingia kwenye App na ufurahie maudhui ya channel za Azam TV kupitia AzamTV Max
Njinsi ya Kuingia (login) kwenye Azam Max
Baada ya kupakua na kujisajili kwenye AzamTv Max sasa utahitaji kuweza kulogin kwenye App yako ya AzamTv Max, hapa chini ni hatua za kulogin kwenye AzamTV Max
1. Ili kuweza kulogin kwenye App ya AzamTV Max ingia kwenye simu yako na usungue App
2. Kisha itakupa chaguzi za kuweza kutumia kuingia kwenye akaunti yako ya AzamTV MAX,
- Unaweza kulogin kwa kutumia email yako
- au unaweza kuingia kwa kutumia namba yako ya simu ulioitumia wakati wa kujisajili
3. Kisha utaweka neno siri na utabonyeza INGIA
4. Utakua umesha ingia kwenye akaunti yako ya AzamTV MAX.
Jinsi ya Kuweka Malipo kwa Ajili ya Kifurushi
Baada ya kujiandikisha, unaweza kujiunga na vifurushi mbalimbali vya kulipia ili kufurahia vipindi vyote vilivyopo kwenye AzamTV Max.
Njia za Malipo:
- Tigo Pesa, M-Pesa, Airtel Money, Halopesa
- Kadi za Benki (Visa/MasterCard)
- AzamPay
Fuata maelekezo kwenye programu ili kuchagua na kulipia kifurushi unachotaka.
Faida za Kutumia AzamTV Max
- Uwezo wa kutazama chaneli za AzamTV popote ulipo.
- Maudhui ya moja kwa moja (Live) kama mechi za mpira, tamthilia, na filamu.
- Ubora wa juu wa picha na sauti.
- Inapatikana kwa vifaa vyote vya kidigitali.
AZAM MAX APP HUDUMA KWA WATEJA
Mpendwa mteja,
Kwa mawasiliano ya App yako ya AzamTV MAX tafadhali wasiliana nasi kwa njia zifuatazo:
WhatsApp pekee: 0677 99 66 44
Email: appsupport@azam-paytv.com
Instagram: @azamtvmaxapp
Namba za Huduma kwa Wateja:
●0784 108 000
●0764 700 222
●0659 072 002
Karibu tukuhudumie!