Mahitaji ya Kujiunga
Kipengele | Mahitaji |
---|---|
Mchangiaji | Hati ya mshahara, picha ya pasipoti |
Mwenza | Cheti cha ndoa, picha ya pasipoti |
Watoto | Vyeti vya kuzaliwa, picha za pasipoti |
Wazazi/Wakwe | Cheti cha kuzaliwa cha mchangiaji, picha za pasipoti |
Malipo | TZS 340,000 kwa kaya ya watu sita kwa mwaka |
Hatua za Kujiunga na NHIF
Kujaza Fomu za Maombi: Tembelea ofisi ya NHIF iliyo karibu au tovuti yao ili kupata fomu za maombi. Jaza fomu kwa usahihi, ukijumuisha taarifa za mchangiaji, mwenza, na wategemezi.
Viambatanisho Muhimu: Andaa viambatanisho vifuatavyo:
- Mchangiaji: Hati ya kupokelea mshahara (salary slip) yenye makato ya bima ya afya na picha ya hivi karibuni ya ukubwa wa pasipoti.
- Mwenza: Nakala ya cheti cha ndoa na picha ya hivi karibuni ya ukubwa wa pasipoti.
- Watoto: Nakala ya vyeti vya kuzaliwa na picha za hivi karibuni za ukubwa wa pasipoti.
- Wazazi/Wakwe: Cheti cha kuzaliwa cha mchangiaji na picha za hivi karibuni za ukubwa wa pasipoti.
- Malipo: Lipa ada ya kujiunga kupitia benki au njia nyingine zilizowekwa na NHIF. Kwa kaya ya watu sita, ada ni TZS 340,000 kwa mwaka.
Utaratibu wa ujazaji wa Fomu za Bima ya Afya (NHIF).
Utaratibu wa ujazaji wa Fomu za Bima ya Afya (NHIF)
Idadi ya watu wanaotakiwa kujazwa kwenye fomu ya bima ya afya ni 16 kwa mtiririko ufuatao;
Mchangiaji mwenyewe na mwenza wake(mke au mme)
Faili ya watoto wasiozidi 4 chini ya miaka 18,au wazazi/wakwe katika idadi hiyo ya watu wane(40 maana unaweza ukawajaza watoto wawili(2) na wazazi (2).
1. VIAMBATANISHO
Mchangiaji:
1.Hati ya kupokelea mshahara(salary slip) yenye makato ya bima ya afya.
2.Picha zenye ukubwa wa pasipoti(passport size) moja ya hivi karibuni.
Mwenza(Mke au mme)
1.Nakala ya cheti cha ndoa (copy)
2.Picha zenye ukubwa wa pasipoti(passport size) moja ya hivi karibuni.
Watoto:
1.Nakala ya Vyeti vya kuzaliwa(copy).
2. Picha zenye ukubwa wa pasipoti(passport size) moja ya hivi karibuni.
Wazazi:
1.Cheti cha kuzaliwa cha mchangiaji (mtumishi).
2 Picha zenye ukubwa wa pasipoti(passport size) moja ya hivi karibuni
Wakwe:
- Cheti cha ndoa
- Picha zenye ukubwa wa pasipoti(passport size) moja ya hivi karibuni
•Kuongeza mtegemezi:
Viambatanisho ni vilevile saraly slip,picha pasporti size na nakala ya cheti cha kuzaliwa.
Utalipia benki Tzsh 20,000/=kwa kila kadi iliyopotea kwa akaunti namba 61010016954 yenye jina Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Baada ya hapo utamwona Mratibu ukiwa na loss Report ya polisi,pay slip ya benki uliyolipia na picha passport size ili ujaze fomu nyingine uweze kupata kadi nyingine.
Kwa wastaafu:
Viambatanisho
1.Nakala ya kibali cha kustaafu
2.Unarudisha kodi ulizopewa pamoja na wategemezi wako.
3.Picha yako passport size pamoja na ya mwenza wako ya hivi karibuni ili uandaliwe kadi nyingine.
4.Kama kuna kadi zimepotea kati ya kadi sita(6) ulizopewa,utaripoti kwa mratibu wa Bima ya Afya au Afisa Utumishi ili uandikiwe barua ya kwenda nayo polisi.
Kupata Kadi ya Bima: Baada ya kukamilisha malipo na kuwasilisha viambatanisho vyote, utapokea namba ya kitambulisho ambayo itakuruhusu kupata huduma za afya. Mfuko hautatoa vitambulisho halisi.
Aina ya Vifurushi Vya Bima ya Afya NHIF kwa Mtu Binafsi na Gharama zake
Aina ya Vifurushi Vya Bima ya Afya NHIF kwa Mtu Binafsi na Gharama zake