Jinsi ya Kukata tiketi ya bus online

Jinsi ya Kukata tiketi ya bus online
Jinsi ya Kukata tiketi ya bus online

Kwa wasafiri wa Mabasi ya Mkoani siku hizi Huna haja ya kuhangaika kwenda stendi ukasumbuane na wapiga debe sasa unaweza kata Tiketi ukiwa nyumbani kwako kwa kutumia simu yako Hapa tunakupa muongozo kamili.

Hatua za Kukata Tiketi Online

  1. Tembelea Tovuti au Programu: Chagua jukwaa kama OtappTiketi.com, au Shabiby.
  2. Ingiza Taarifa za Safari: Chagua jiji la kuanzia na kushukia, tarehe, na idadi ya abiria.
  3. Chagua Basi: Linganisha muda wa kuondoka, bei, na aina ya basi (kwa mfano, na A/C au choo).
  4. Malipo: Tumia njia kama M-Pesa, benki, au kadi ya mkopo.
  5. Pokea Tiketi: Tiketi itatuma kwenye simu au barua pepe yako.

Umuhimu wa Huduma Ya Kukata Tiketi Mtandaoni

  1. Kuepuka foleni ya ukataji wa tiketi
  2. Huchukua mda mfupi zaidi
  3. Usalama wa kifedha
  4. uchaguzi wa siti ya basi
  5. Kuepusha gharama

Jinsi Ya Kukata Tiketi Ya Basi Mtandaoni

Makampuni baadhi ya usafirishaji kwa njia ya basi wameweza kurahisisha mchakato wa ukataji wa tiketi za mabasi kwa kuanzisha mifumo ya mdandaoni ya ukataji wa tiketi. Hapa tutaenda kuangazia baadhi ya makampuni na jinsi unavyoweza kukata tiketi kupitia makampuni hayo

Jinsi Ya Kukata Tiketi Ya Basi Mtandaoni

1. Abood Bus Service

Abood ni moja kati ya kampuni za mabasi kubwa na za muda mrefu kama wewe ni msafiri kwenye mkoa ambao basi za Abood zinafanya safari zake basi habari njema ni kua kwa kutumia simu au kifaa chako chenye uwezo wa kuindia mtandaoni unaweza kukata tiketi ya safari yako. Cha kufanya fuata hatua zifuatazao;

  1. Ingia kwenye tovuti rasimi ya kampuni ya Abood Bus Service kwa kutumia link hii hapa – https://aboodbus.co.tz/
  2. Kwenye ukrasa wa tovuti ya Abood jaza taarifa zako za safari kama vile, Unakotoka, Unako kwenda na siku ya safari
  3. Baada ya kujaza taarifa bonyeza neno “Search”
  4. Baada ya kubonyeza orodha ya mabasi itafunguka na taarifa zake kama muda wa safari na bei ya nauli
  5. Kisha bonyeza neno “Book Tiket”
  6. Ukrasa wa mpangilio wa siti utafunguka na utachagua siti uipendayo kulingana na maelekezo ya mfumo kisha utabonyeza “proceed”
  7. Mfumo wa tiketi utafunguka na utajaza taarifa kutokana na maelekezo na kisha mbonyeza “Endelea” ili kumaliza hatua na kukata tiketi yako.
SOMA HII :  Bei ya TV za Samsung Inch 65 Tanzania

2. Shabiby Line

kwa wasafiri wa kampuni ya Shabiby  line, kampuni hii pia inamfumo wa ukataji tiketi kwa njia ya mtandao kupitia tovuti yao, cha kufanya fuata hatua zifuatazo hapa chini ili kukata tiketi ya basi ya Shabiby Line.

Jinsi Ya Kukata Tiketi Ya Basi Mtandaoni

  1. Ingia kwenye tovuti rasimi ya kampuni ya Shabiby Line kwa kutumia link hii hapa – https://shabiby.co.tz
  2. Kwenye ukrasa wa tovuti ya Shabiby Line nenda kwenye upande wa NUNUA TIKETI na ujaze taarifa zako za safari kama vile, Unakotoka, Unako kwenda na siku ya safari
  3. Baada ya kujaza taarifa bonyeza neno “Angalia Ratiba”
  4. Baada ya kubonyeza orodha ya mabasi itafunguka na taarifa zake kama muda wa safari na bei ya nauli na daraja la basi
  5. Kisha bonyeza neno “Nnua Tiketi”
  6. Ukrasa wa mpangilio wa siti utafunguka na utachagua siti uipendayo kulingana na maelekezo ya mfumo kisha utabonyeza “Hifadhi Tiketi”
  7. Mfumo wa tiketi utafunguka na utajaza taarifa kutokana na maelekezo na kisha mbonyeza “Endelea” ili kumaliza hatua na kukata tiketi yako.

3. Happy Nation

Kampuni ya mabasi ya Happy Nation nayo ni miongoni mwa kampuni za usafirishaji zenye kutoa huduma ya ukataji wa tiketi kwa njia ya mtandao, ili kuweza kukata tiketi ya basi katika kampuni ya Happy Nation kwa njia ya mtandao tafadhari fuata hatua zifuatazo;

Jinsi Ya Kukata Tiketi Ya Basi Mtandaoni

  1. Ingia kwenye tovuti rasimi ya kampuni ya Shabiby Line kwa kutumia link hii hapa – https://www.happynation.co.tz/
  2. Kwenye ukrasa wa tovuti ya Happy Nation jaza taarifa zako za safari kama vile, Unakotoka, Unako kwenda na siku ya safari
  3. Baada ya kujaza taarifa bonyeza neno “Tafuta Basi”
  4. Baada ya kubonyeza orodha ya mabasi itafunguka na taarifa zake kama muda wa safari na bei ya nauli na daraja la basi
  5. Kisha bonyeza neno “Nnua Tiketi”
  6. Ukrasa wa mpangilio wa siti utafunguka na utachagua siti uipendayo kulingana na maelekezo ya mfumo kisha utabonyeza “Hifadhi Tiketi”
  7. Mfumo wa tiketi utafunguka na utajaza taarifa kutokana na maelekezo na kisha mbonyeza “Endelea” ili kumaliza hatua na kukata tiketi yako.
SOMA HII :  Nauli za Air Tanzania Mwanza to Dar es salaam

Video: Jinsi Ya Kukata Ticket Za Mabasi Online

About Burhoney 4806 Articles
Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati